Wakulima nchini bado wanahitaji kutumia mbinu za kisasa za kilimo, ufugaji, na uhifadhi mazingira

Na: Bujaga I. Kadago

Pamoja na Tanzania kujitosheleza kwa kiasi kikubwa katika suala la uhakika wa chakula, lakini wakulima nchini bado wanahitaji kutumia mbinu za kisasa za kilimo, ufugaji, na uhifadhi mazingira.

Kauli hiyo imetolewa asubuhi hii na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Waziri Mkuu {mstaafu} na Jaji {mstaafu}, mhe. Joseph Sinde Warioba alipozungumza na Menejimenti ya chuo mwanzoni mwa ziara yake ya siku 2 chuoni SUA.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Waziri Mkuu {mstaafu} na Jaji {mstaafu}, mhe. Joseph Sinde Warioba akikaribishwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda katika ziara yake ya siku mbili chuoni hapo,kulia wa pili ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Jaji Mkuu (mstaafu), Mhe. Mohamed Chande Othman, na wa kwanza kulia ni Naibu wa Makamu wa Mkuu wa Chuo Prof. Petter Gillah.(Picha na Tatyana Celestine)

Amesema lengo la ziara hii ni kukijua chuo kwa undani ili awe na uelewa mzuri kuhusu chuo na hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kutekeleza, kushauri na kutatua changamoto zilizopo chuoni.

Mapema akimkaribisha Mhe. Warioba, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Jaji Mkuu (mstaafu), Mhe. Mohamed Chande Othman alipongeza ushirikiano uliopo kati ya Chuo, Wizara mama ya Elimu na Serikali Kuu na hivyo kuwezesha baadhi ya changamoto kutatuliwa na kufanya chuo kuwa na maendeleo

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner