Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kimeomba Serikali kuongeza fedha kwa ajili ya kufanyia Tafiti

Na. Bujaga I Kadago

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kimeomba Serikali kuongeza fedha kwa ajili ya kufanyia Tafiti na hivyo kuwa na uhuru wa kufanya tafiti zinazolenga kutatua changamoto za wakulima wetu.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine  Kilimo SUA Jaji mstaafu Mhe. Joseph Sinde Warioba akipata maelezo toka kwa Mtaalam wa Udongo toka  Idara ya Sayansi ya Udongo Bw. Alphonce Mgina katika ziara yake chuoni hapo.(Picha na Tatyana Celestine)

Rai hiyo imetolewa na Makamu wa Mkuu wa Chuo cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda alipokuwa akitoa taarifa ya shughuli za chuo kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine  Kilimo SUA Jaji mstaafu Mhe. Joseph Sinde Warioba wakati wa kuanza ziara ya siku mbili chuoni

Prof. Chibunda amesema tafiti zinazofanyika kutokana na fedha za wafadhili kwa kiasi fulani zinakuwa hazizingatii mahitaji ya wakulima wa Tanzania.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine  Kilimo SUA Jaji mstaafu Mhe. Joseph Sinde Warioba akielezea jambo alipotembelea Duka la Mboga na Matunda katika Chuo Kikuu cha Sokoine  Kilimo SUA .(Picha na Tatyana Celestine)

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine  Kilimo SUA Jaji mstaafu Mhe. Joseph Sinde Warioba, Jaji Mkuu (mstaafu), Mhe. Mohamed Chande Othman katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Chuo na wanafunzi toka nchi mbalimbali.(Picha na Tatyana Celestine)

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner