Wizara ya Madini haitawavumilia watendaji wanaokuwa  chanzo cha upotevu wa maduhuli

Na:Gerald Lwomile

Wizara ya Madini imesema haitawavumilia watendaji wanaokuwa  chanzo cha upotevu wa maduhuli katika wizara hiyo na kuahidi kutoa msaada wa kila hali katika kuhakikisha watendaji hao wanakusanya maduhuli hayo na kufikia malengo.

mheshimiwaNaibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo akifunga mafunzo yaliyowahusisha wahasibu kutoka mikoa mbalimbali na  Wizara ya Madini leo katika Ndaki ya Solomon Mahlangu Sayansi na Elimu iliyopo Mazimbu mjini Morogoro.(Picha na Tatyana Celestine)

 

Onyo hilo limetolewa hii leo katika Ndaki ya Solomon Mahlangu Sayansi na Elimu iliyopo Mazimbu mjini Morogoro na Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo, wakati akifunga mafunzo yaliyowahusisha wahasibu kutoka mikoa mbalimbali na  Wizara ya Madini.

Mhe. Nyongo amesema kwa kutambua umuhimu wa watendaji hao wizara imeamua kuwawezesha kwa mafunzo ya kutumia mfumo wa kielectroniki wa kukusanya mapato yatakanayo na madini ili kukuza tija na ufanisi katika ukusanyaji wa mapato na kupunguza mianya ya upotevu wa mazao hayo.mkaaka

Wahasibu kutoka mikoa mbalimbali wa  Wizara ya Madini wakisikiliza kwa makini wakati wa mafunzo leo katika Ndaki ya Solomon Mahlangu Sayansi na Elimu iliyopo Mazimbu mjini Morogoro.(Picha na Tatyana Celestine)

Naibu Waziri huyo amesema mfumo wa kielectroniki wa kukusanya mapato ni kwa mujibu wa sheria na lazima utumike katika wizara hiyo, kwani imepewa jukumu kubwa la kufikia malengo ya serikali ya kukusanya shilingi bilioni 310 huku Wizara yenyewe ikiwa na lengo la kukusanya shilingi bilioni 500.

Awali akimkaribisha Naibu Waziri, Mkurugenzi wa Fedha wa Wizara hiyo Bw. Antony Tarimo amesema awali walikuwa wakikabiliwa na chanagamoto katika ukusanyaji wa maduhuli kutokana na kutotumia mfumo wa kisasa wa kielectroniki.

Amesema baada ya mafunzo hayo sasa wanatarajia wahasibu hao watafanya kazi kwa waledi mkubwa na kufikia malengo ya kukusanya maduhuli hayo ya serikali.

pamoj

Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo  katika picha ya pamoja  na wadau na wahitimu wa mafunzo yaliyowahusisha wahasibu kutoka mikoa mbalimbali wa  Wizara ya Madini leo katika Ndaki ya Solomon Mahlangu Sayansi na Elimu iliyopo Mazimbu mjini Morogoro.(Picha na Tatyana Celestine)

 

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner