Mahafali ya 34 SUA

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA, Jaji mstaafu Joseph Sinde Warioba ametunuku Shahada mbalimbali kwa wahitimu 2695 huku zaidi ya wahitimu 50 wakipata shahada ya Udaktari wa Falsafa katika Fani mbalimbali.
 
graduu
 
Mkuu huyo wa Chuo ambaye pia ni Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya awamu ya kwanza Mhe. Warioba ametunuku shahada hizo katika ukumbi wa Nelson Mandela (Freedom Square)  uliopo katika Ndaki ya Solomon Mahlangu ya Sayansi na Elimu,  mkoani Morogoro
 
Awali akitoa taarifa ya Chuo hicho Mwenyekiti wa Baraza Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Othuman Chande amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutimiza ahadi alizozitoa wakati wa ziara yake Chuo hapo.
 
 
“ Nimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutimiza ahadi zake alipotembelea SUA, kwa kutoa Matreka 10 kwa ajili ya mafunzo na pia kuongeza fedha za maendeleo kwa kuhamisha kiasi cha shilingi bilioni mbili kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam”.alisema Mhe. Chande.
 
Naye Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda amesema wahitimu wote katika chuo hicho wamefanya kazi ya ziada katika kuhakikisha wanafaulu kwenye masomo yao kwani chuo hicho kimekuwa kikizingatia kutoa elimu iliyo bora kwa wanafunzi wake.
 

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner