WABUNGE, MADIWANI WATEULE WAASWA KUSHIRIKIANA NA RAIS

      

Na: IRIMINA MATERU

Wabunge pamoja na Madiwani wametakiwa kushirikiana bega kwa bega na Rais Mteule Dr. John Pombe Magufuli huku wakiondoa  tofauti za vyama vyao kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia  kufanya kazi kikamilifu ikiwemo kutekeleza ahadi wa yale waliyoyaahidi katika kampeni zao

Bofya hapa kwa Habari zaidi.......

 

 

Hayo yamebainishwa na  Wananchi wa Manispaa ya Morogoro wakati wakizungumza na SUAMEDIA huku wakisema kuwa wamapokea  vizuri matokeo ya nafasi ya Urais, ubunge,na udiwani nawamesema kuwa wanacho hihitaji kwa sasa ni mabadiliko na pia viongozi waliochaguliwa wafanye kazi kwa uadilifu ili kuleta mabadiliko makubwa hapa nchini.

Aidha wananchi hao wamemtaka Rais mteule  Dk. Magufuli kuhakikisha kauli mbiu aliyokuwa akijinadi nayo kipindi cha kampeni ya “HAPA KAZI TU”aitumie kukomesha ufisadi kwani hilo ndilo tatizo linalorudisha nyuma maendeleo ya wananchi walio wengi na kusababisha pia  vijana wengi kukosa ajira na hivyo kurudisha nyuma  uchumi wa nchi.

“Nimefurahi sana kumpata Rais mchapa kazi, mwenye msimamo na ana uamuzi mzuri, hivyo  kwa upande wangu namshauri rais, akague kazi atakazoagiza yeye kama yeye kwa mfano katika hospitali,wakati dawa zinavyopelekwa  ahakikishe anakwenda mwenyewe kukagua tena bila kutoa taarifa na siyo  kuunda tume ya kwenda kukagua”. Alieleza Kazai Mahamudu Kazai, Mkazi wa Morogoro mjini.

Kwa upande wao wanasiasa katika Manispaa ya Morogoro wamesema uchaguzi wowote lazima uwe na lawama hivyo wamewataka wananchi kuyapokea matokeo kama yalivyotangazwa na kuwataka wananchi kuacha kuanza kulalamika na badala yake wasubiri zile ahadi walizo ahidiwa zitekelezwe.

“Duniani kote uchaguzi lazima uwe na changamoto mbalimbali, watanzania hatuna budi kusubiri yale yaliyoahidiwa na viongozi wetu je! yatatekelezeka? Nasema hivyo kwa kuwa kuna vyama vya upinzani na wanalalamika, tusubiri pia ahadi alizoahidi Rais kama elimu, kuboresha viwanda na kuimarisha miundombinu na visipofanyika wananchi tuna haki ya kudai kwani sisi ndiyo tuliowachagua”. Alieleza Ustadhi Jabir Muhimbamti.

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner