MAFURIKO YAMEATHIRI WANANCHI WA KILAKALA MANISPAA YA MOROGORO

PICHA Na: IRIMINA MATERU

 

Na: IRIMINA MATERU

Wananchi wa kata ya Kilakala Manispaa ya Morogoro Wameiomba Serikali kuwapatia msaada ukiwemo wa chakula kutokana na kuathirika kwa mafuriko yaliyotokana na mvua iliyonyesha usiku wa tarehe 30 mwezi uliopita.

Bofya hapa kwa Habari zaidi.......

Wakizungumza na SUAMEDIA wananchi hao wamesema kuwa mafuriko hayo yamewaathiri kwa kiasi kikubwa kutokana na vitu vyao kusombwa na maji hayo na kuwaacha bila ya kitu chochote hivyo kutegemea misaada kutoka kwa wasamaria wema.

Aidha Wananchi hao wamemlalamikia mkandarasi anayetengeneza barabara ya kilakala kwa kuziba mifereji ambayo ilikuwa ikipitisha maji hapo awali na kusababisha maji hayo  ya mvua kuingia katika makazi ya watu baada ya kukosa mwelekeo.

“Mimi ni mkazi wa hapa miaka mingi na sasa nina umri wa miaka 61, juzi kumetokea mvua na kupelekea mafuriko ambayo sijawahi kuona hapa kilakala na hii yote ni kutokana na barabara inayotengenezwa na mvua ilivyonyesha ikapelekea mifereji kuziba, yaani maji yote machafu yanaingia ndani vitu vyote vimesombwa na maji, serikali ituangalie jamani tunaomba” alieleza Sara Raphaeli.

SUAMEDIA ilitaka kupata maoni ya mwenyekiti wa mtaa wa kilakala ambapo alisema “Mvua ni nyingi hadi maji yameingia ndani lakini kwa sasa niwatoe hofu wananchi wangu kuwa tatizo hilo litatatuliwa haraka iwezekanavyo, mimi kama mwenyekiti wa mtaa wa kilakala natoa shukrani kwa hatua za mwanzo za haraka zilizochukuliwa kwa mkandarasi pamoja na viongozi wote” .

Kwa upande wake Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro Abdul Digaga amekiri kuzibwa kwa mifereji hiyo iliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha na kusema kuwa tayari wameshatoa maelakezo kwa mkandarasi juu ya suala hilo.

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner