WAKRISTO WAHIMIZWA KUISHI KATIKA UPENDO WA MUNGU

PICHA NA: ALFRED LUKONGE

   

Na: MNGEREZA MNTAMBO

Mratibu  wa  mkutano  wa   Injili  maarufu kama  Makambi  katika kanisa la Wadventista wa Sabato Misufini mkoani  Morogoro  Thomas Makubi  amesema watu  waliofika  mwaka  huu wamechota  mengi  ikiwemo  namna  ya  kuishi  ndani  ya  upendo  wa  Mungu.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

Akiongea  na SUAMEDIA  Bw.Makubi  ameongeza   kwa  kusema  “mkutano  wa  Makambi ni  kila  mwaka kwa  mujibu  wa  Biblia  kwenda  sawasawa  na   wana  Waisraeli  walivyokuwa  wakienda  Kaanani  walifanya  sikukuu  za  Vibanda”, pia ametoa  wito  kwa  waumini  na  wasio  waumini  kujumuika  nao ili  wapate  chakula  cha  kiroho.    

Mmoja  ya  washiriki  wa  semina  hiyo   mama  Martha  Bwaira   amesema    amefurahishwa na  semina   kuendeshwa  kwa mtindo wa   kuwagawa   watu  katika  makundi  akijitolea  mfano  yeye   mwenyewe  kuwa  amepangwa  katika  kundi la wanandoa   waliofikisha  miaka   kumi  na  sita  na  kuendelea kwenye ndoa zao ambapo  humo  ndani  amejifunza  mambo  yanayotakiwa  kufanywa  na  mwanamke  kwa  mumewe, jinsi  ya  kulea watoto  na   jambo la mapato  lisiwe  siri  kwa  wanafamilia.     

Mshiriki   mwingine   Bw.Jacob   Mshombe  yeye  amejifunza  kwenye  maisha  ya  sasa  watu  wamtegemee Mungu  pekee  na  sio  wanadamu,   vilevile amejifunza jinsi  ya   kujitawala  hususan  kwenye  matumizi  ya  ulimi  kwa kuwa  ukiutawala  ulimi  utakuwa  umetawala  na  akili  mungu  alizokupatia.

Semina   ya  Makambi  katika  Kanisa  hilo  ilianza  Jumamosi  ya   tarehe  31/10/2015  ikibeba  ujumbe  wa “ Tupokee na kuishi  ukarimu pekee wa Mungu”na  itaendelea  kanisani  hapo  kwa  muda   wa  siku  7 toka  tarehe  hiyo ikilenga  kufikisha  ujumbe  wa   kiroho  kwa  watu  wa  dini   zote.

 

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner