RAIS MAGUFULI APONGEZA MFUMO WA MAWASILIANO UTAKAOWASAIDIA WAKULIMA KUPATA TAARIFA ZA KILIMO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL kwa kuanzisha mfumo wa mawasiliano utakaowasaidia wakulima kupata taarifa mbalimbali za kilimo nchini.

Rais Magufuli ametoa pongezi hizo leo, May 21 wakati wa hafla ya kupokea gawio la Serikali kwa mujibu wa sheria kutoka Shirika hilo ambapo limetoa jumla ya shilingi bilioni 2.1.
Akizungumza katika hafla hiyo Rais Magufuli amesema wakulima kupata taarifa mbalimbali ni jambo la msingi ambalo kwa kiasi kikubwa litasaidia wakulima hao kuwa na mafanikio ukizingatia hivi sasa zaidi ya watanzania milioni 23 nchini wanatumia huduma za mawasiliano na hapana shaka wakulima ni miongoni mwao.
Aidha Rais Magufuli ameonyeshwa kushangazwa na Shirika hilo kuendelea kukodisha minara ya mawasiliano katika mikoa mbalimbali wakati linatakiwa kuwa na minara yake na kumwagiza Waziri wa Ujenzi, Mawasilino na Uchukuzi Injinia Isack Kamwelwe kuhakikisha wanatoa fedha ili kujengwa minara watakayopewa TTCL
Rais Magufuli amelipongeza shirika hilo kwa kuendelea kutoa gawio kwa serikali na kuagiza mashirika mengine ambayo hayawezi kutengeneza faida na kutoa gawio ni afadhali yakafungwa
Awali akimkaribisha Mhe. Rais, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Injinia Isack Kamwele amesema mapato ya Shirika la TTCL yameongezeka na ndiyo maana Shirika hilo limefanikiwa kutoa gawio kwa Serikali.
Naye Mkrugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Bw. Waziri Kindamba amesema wamefanikiwa kutoa gawio hilo la bilioni 2.1 ikiwa ni ongezo la shilingi milioni mia sita walizotoa mwaka jana na hii ni kutokana na kuongezeka kwa wateja wanaotaka huduma bora kutoka shirika hilo

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner