KITUO CHA KUFUNDISHIA WAKULIMA VIJIJINI KUJENGWA NA WAKOREA SUA


Chuo Kikuu  Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) kimeingia Mkataba wa Makubaliano wa miaka mitano  na Chuo Kikuu cha Yeungnam cha Korea  Kusini  ili kujenga kituo cha kufundishia  wakulima   vijijini  lengo likiwa ni kuendeleza na kuinua  kilimo hapa nchini.
Makubaliano hayo yamefanywa May 20 ambapo Makamu Mkuu wa Chuo cha Yeungnam Prof. Changdeog Huh pamoja na Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu  cha Sokoine Cha kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda wamesimamia kutiwa saini Mkataba wa Makubaliano.


Akizungumza mara baada ya makubaliano hayo Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu  cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda amesema kuwa  makubaliano hayo yatasaidia  katika kusambaza teknolojia bora za kilimo vijijini.
 
 
 

Chibunda ameongeza kuwa chuo kitatoa baadhi ya walimu kwenda kusoma shahada ya pili na ya tatu katika Chuo cha Yeungnam cha Korea Kusini ili kuongeza uelewa zaidi katika taaluma zao za kilimo 


Naye Makamu  Mkuu wa Chuo cha Yeungnam Prof. Changdeog Huh  ameipongeza SUA kwa kutoa elimu ya kilimo  na kuhaidi kuendelea kutoa ushirikiano  ili kuhakikisha kilimo kinaendelea kutoa mchango kwa Taifa..

 

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner