UDAHILI UNAENDELEA CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA)

    

Na: ALFRED LUKONGE

Udahili   wa   wanafunzi  wapya katika Chuo Kikuu Cha  Sokoine Cha Kilimo ( SUA)  Mkoani  Morogoro  unaendelea  vizuri  na wanategemea kudahili idadi  ya wanafunzi  elfu  mbili na mia tano kwa muhula wa masomo 2015/2016.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

Hayo yamesemwa na  Afisa   Udahili  Mwandamizi Bi. Elizabeth Nanga wakati  wa  mchakato  wa  udahili  wa   wanafunzi  wapya ulioanza  toka  tarehe  2/11/2015  Chuoni  hapo katika  ukumbi  wa New Lecture  Theatre.

Akizungumzia mchakato huo mmoja  ya wanafunzi waliodahiliwa Goodlucky  Matulanya anayetegemea  kujiunga  na  shahada ya  Uchumi Kilimo amesema mchakato  unaendelea  vizuri  na  matarajio yake  Chuoni hapo   ni  kuwa  mweledi  katika  fani  ya  Uchumi  Kilimo na mengine atayajua  masomo  yatakapoanza.

Mdahiliwa  mwingine  anayetegemea  kujiunga  na  Shahada  ya  Misitu Bw. Essau  Mhonda  amesifia  mchakato mzima  wa  udahili  na  matarajio  yake  kwenye  Elimu hiyo ni  kuendeleza  mashamba  yake  aliyoanzisha ili yatoe  matokea  bora kwa  weledi  atakaojifunza  chuoni  SUA.

Naye  Genoveva Alfred aliyejiunga  na  Shahada  ya  Sayansi  ya Chakula pamoja na kusifia mchakato huo pia amesema “ sitapata shida  kwenye  ajira kwa kuwa  Shahada  yangu  kutoka  SUA  itakuwa  na  mashiko”, na kwamba ana Imani atapata  kazi  kwenye  makampuni  makubwa baada ya kumaliza masomo  yake.

Muhula mpya wa masomo 2015/2016 chuoni hapo umeanza 02/11/2015 kwa udahili wa  wanafunzi wapya na wale wanaoendelea kusoma.

 

 

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner