Miaka mitatu Baraza la Chuo SUA kufanikiwa kwa asilimia 80

 

NA;AYOUB MWIGUNE
Wajumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA wamekipongeza chuo hicho kwa kukamilisha maelekezo yote
ambayo wametoa na kutekeleza kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wao
Hayo yameelezwa na Makamu wa mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Esther Mwaikambo
katika ziara ya baraza la chuo hicho  ikiwa na lengo la kutembelea miradi ya maendeleo ili kuweza kuona malengo yaliofanywa na
baraza hilo kwa miaka mitatu.
  Aidha Prof. Esther Mwaikambo amepongeza hatua ambayo imefikiwa ya ujenzi wa maabara  mtambuka inayojengwa
katika kampasi kuu ya chuo hicho akisema kwamba ujenzi wa maabara hiyo utawezesha kuchukua wanafunzi wengi kwa
wakati mmoja .

 

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda amesema chini ya maekezo
ya baraza hilo chuo kilielekezwa kufanya mambo mengi  ikiwemo kuboresha miundo mbinu ya ufundishaji na kujifunzia huku chuo
hicho kikiteleza maelekezo kwa asilimia 80
 Ametolea mifano ya maeneo ambayo chuo kimeweza kufanya maboresho  Prof. Chibunda amesema chuo kimeweza kuboresha
huduma ya afya kwa ununuzi wa x-ray mpya, kitengo cha meno pia kuboresha mafunzo kwa vitendo ,kuboresha shamba la
mafunzo ,ujenzi wa maabara mtambuka  pamoja na maboresho ya hospitali ya mifugo ya wanyama .
Aidha Prof. Raphael Chibunda ametoa wito kwa watanzania ambao wanafuga mifugo mbalimbali kuitumia hopsitali ya taifa
ya wanyama iliyopo chuoni hapo kwani ni hospitali ya kipekee nchini.
Katika picha: Baada ya kupokea Tuzo za shukurani kwa kazi waliyoifanya kwa kipindi cha miaka mitatu ya kutumiakia BARAZA LA
CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO SUA, wajumbe wakifurahia katika hafla ya kuaagana iliyofanyika katika
ukumbi wa ICE ndani ya Chuo hicho.
Makamu wa mkuu wa Chuo Prof. Raphael Chibunda-SUA
Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha-SUA, Prof. Fredrick Kahimba
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi RAAWU -SUA Bi Gaudencia Mchotika
Mkurugenzi Msaidizi wa Uendelezaji wa Mazao Bw. Beatus Malema 

Mkurugenzi Msaidizi wa Uendelezajiwa Mazao Bw. Beatus Malema kulia na Kaimu Makamu wa Mkuu wa Chuo cha Ushirika -Moshi Prof. Alfred Sife

aliyeshika Tuzo

 

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner