Serikali yakanusha kuchoma na kuzui utafiti wa GMO nchini

Na Calvin Gwabara

Dar es Salaam

SERIKALI Imesema Haijawai kuzuia Utafiti wa Mbegu za GMOs wala kuchoma majaribio yake yanayofanyika hapa nchini bali yanaendelea kufanyika kwa Baraka zote za Serikali na kwamba yatakapokamilika maamuzi yatatolewa.

Majaribio ya Utafiti huo wa Mbegu za GMOs yanafanyika katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupola kilichopo Mkoani Dodoma kuhusiana na mbegu za Mahindi  na Mikocheni kilichopo Jijini Dar es Salaam kuhusiana na mbegu za mihogo.

Akizungumza katika mjadala wa wazi wa Siasa za uchumi wa GMOs kwa Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Mratibu wa Utafiti wa Bioteknolojia za kilimo Tanzania kutoka Taasisi ya Kilimo Tanzania (TARI) Dk Fred Tairo,alisema kwa sasa utafiti huo upo katika hatua mbalimbali  katika vituo hivyo.

Dk Tairo, alisema kuwa watu pamoja na vyombo vya habari hapa nchini walielewa vibaya kuhusiana na taarifa zilizotolewa na kwamba Serikali ilitaka Watafiti wafuate utaratibu wa kutoa matokeo walikuwa wanayapata kwenye majaribio hayo ili kuondoa mkanganyiko.

GMO5

Dkt. Fredy Tairo ambaye ni mratibu wa tafiti za Bioteknolojia katika kilimo kutoka TARI Mikocheni akiwasilisha mada

“ Kabla sijaanza kuwasilisha mada yangu kwanza naomba kutoa ufafanuzi kuwa Serikali haikuzuia wala kuchoma moto Utafiti wa mbegu za GMOs nchini na majaribio hayo yanaendelea kwa Baraka zote za Serikali  maana inatambua umuhimu wa tafiti “Alisema Dk Tairo.

Mtafiti huyo alisema msimamo wa Serikali ni kuendelea Utafiti wa GMOs ili uweze kukamilika katika hatua zake muhimu na kisha utakapokamilika katika hatua zote utapeleka katika Mamlaka husika kwajili ya kutoa maamuzi hapa nchini.

GMO3

Washiriki wa mjadala wa wazi juu ya tafiti za kibioteknolojia wakisikiliza mada mbalimbali

Akizungumzia kuhusu utafiti huo katika Taasisi ya  Utafiti ya  Makutupora alisema umelenga kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya ukame na bungua wa mahindi na matokeo ya awali yameonyesha kufanikiwa kupambana na viwavi jeshi vamizi.

Alisema kwa upande wa Utafiti wa zao la mihogo unaofanyika katika Taasisi ya  Utafiti wa kilimo cha Mikocheni nao katika matokeo ya awali umeonyesha kupambana na ugonjwa wa batobato na michilizi ya kawia.

GMO 1

Bw. Mashamba Phillipo mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Nelson Mandela cha Sayansi na Teknolojia akiwasilisha mada

Naye Mtalaam wa mazao kutoka Chuo Kikuu cha Nelson Mandela cha Sayansi na Teknolojia ,Mashamba Phillipo,alisema teknolojia ya GMOs ni nzuri kwakuwa ina faida kwajili ya kupambana na magonjwa na kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali hapa nchini hivyo ni muhimu kwa Serikali,Watafiti,wadau pamoja na wakulima kuona kama muda muafaka kuanza kutumika.

Mtalaam huyo alitolea mfano kwa zao la nyanya ambalo linaweza kuwekea Jeni ya  GMOs inauwezo wa kukaa mpaka mwezi mmoja bila kuharibika na kumuongezea tija mkulima pamoja na kuwa na soko la uwakika tofauti na ile isiyotumia GMOS.

Naye Mtatibu wa tafiti za Bioteknolojia nchini,Dk Raphael Nduguru,alisema walizunguka nchini nzima na kukusanya mbegu za asili na kuanzia utafiti na kuongeza jeni ili kuweza kukabilina na magonjwa yanayohusiana na mihogo.

Aidha Mtafiti wa Mashariki kutoka Chuo Kikuu cha Westein  Cape cha South Afrika,Emmanuel Sulle,alisema Serikali ya Tanzania ili iweze kufanikiwa katika kilimo lazima iongeze fedha kwenye utafiti na Rasilimali watu.

Alisema Watafiti pamoja na kufanya tafiti za mbegu za GMOs lazima wawasaidie wakulima kuboresha mbinu za wanazotumia wakulima ili waweze kuziboresha na kuongeza uzalishaji.

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner