ANSAF YAJA NA MAPENDEKEZO 8 YA MABORESHO YA SERA YA KILIMO

Na: Josephine Mallango
Jukwaa huru la wadau wa kilimo nchini limewasilisha mapendekezo 8 ya maboresho  ya kisera  kwa  mwaka  2019 miongoni mwa mapendekezo hayo ni mkakati wa kitaifa wa KUPUNGUZA  upotevu wa mazao BAADA YA kuvuna  sanjali  na kuweka  msisitizo kwenye mpango mkakati wa  kushirikisha VIJANA kwenye  kilimo biashara  kutokana  na  uwepo wa ardhi ya kutosha  nchini .


tMkurugenzi wa ANSAF Bw. Audax Rukonge akizungumza  na waandishi wa habari  akitoa taarifa ya mapendekezo ya ANSAF  mkoani Morogoro 

 

Mkurugenzi wa  ANSAF Audax Rukonge amesema hayo mkoani Morogoro wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari  ambapo  ameanza kwa kuipongeza Serikali  ya  awamu ya 5 kupitia Wizara ya Kilimo kuweza kuwashirikisha wadau wa kilimo  kwa mapana  kutoa maoni katika  mchakato wa kupitia na kuboresha Sera ya kilimo ya mwaka 2013 pamoja na jitihada mbalimbali zinazoendelea katika kuendeleza  na  kukuza Sekta ya kilimo nchini .

Amesema upotevu wa mazao baada ya  mavuno ni changamoto inayohitaji kufanyiwa kazi kwa ukaribu katika sera ya kilimo ijayo  kwa Serikali na wadau kuweka makazo  katika   mkakati wa kitaifa wa kupunguza upotevu wa mazao katika mnyororo wa thamani  kwa  kuangalia namna ya kuja na Teknolojia rafiki  na rahisi itakayoweza kutumiwa na wadau wa sekta ya kilimo katika kupunguza na kumaliza upotevu wa mazao baada ya mavuno.

“Upotevu wa mazao katika sehemu ya mwisho mara baada ya kuvuna ni kupotevu wa  pesa ambayo ni faida ya mkulima inayopotea mwisho ,unaweza kuona  hii ni changamoto zaidi kwa kuwa mazao ya nafaka yanapotea kwa asilimia 30 - 40 huku kwa upande wa mbogamboga ikiwa ni asilimia 50 na hii ndio sababu tumeona kuweka mkazo katika kuondokana na upotevu huu ili mkulima wetu sasa aone tija, Elimu , teknolojia ya uhifadhi na miundombinu maghara ,vihenge na usafirishaji vinahitajika kwa wadau wa kilimo ’’

Akizungumzia vijana amesema wamependekeza sera iweke mkazo siyo tu kuakikisha vijana wanashiriki kikamilifu katika kilimo hasa kilimo biashara bali kuwepo na sehemu ya kupima utekelezaji wa ushiriki wa vijana  kwenye kilimo na  hiyo itasaidia vijana wengi kujiajiri katika kilimo kutokana na kuwepo kwa ardhi ya kutosha nchini badala ya kusubili kuajiriwa na kukaa mitaani wawe wanaendelea kushiriki katika shughuli za kimaendeleo.

“Tunahimiza kilimo biashara hasa kwa vijana kwa kuwa katika mapendekezo tunashauri mtu asianze  kulima bila kuwa na uhakika wa soko kuanzia katika masoko ya ndani  vilevile sera iangaliwe namna ya mazao yetu kuvutia bei katika masoko mengine kwa kulima kilimo cha mahindi au mazao mengine yatakayopatikana kwa bei ya chini katika masoko  kuliko mahindi kutoka katika nchi zingine huku yakiwa  na  ubora ”

Mkurugenzi huyo wa (ANSAF) ameongeza kuwa sera ya kilimo imesisitiza upatikanaji wa mazao mengi na bora ili kuakikisha usalama wa chakula na lishe kwa taifa na kaya ambapo maboresho ya sera ya kilimo yamelenga kuchochea maendeleo ya viwanda  nchini ambayo yanakuza soko la mazao ya wakulima hivyo ni muhimu sera hii kuweka mazingira rafiki yatakayohakikisha uwepo wa ukuaji wa viwanda vya ndani kama ilivyoainishwa kwenye mpango wa maendeleo ya kilimo (ASDP II)   na muongozo wa kuboresha mazingira ya kibiashara na uwekezaji nchini (BLUEPRINT).

Mapendekezo mengine ni  umuhimu wa upatikanaji wa takwimu sahihi za kilimo ,mbegu na pembejeo  sanjali  na huduma za ugani na utafiti, kutungwa  kwa  sheria ya  kulinda  ardhi ya kilimo kwa kutambua na kuheshimu maeneo yaliyotengwa  mahsusi  kwa kilimo nchini, kuongeza  kwa bajeti ya kilimo na bima ya mazao sambamba na umuhimu wa miundombinu katika maendeleo ya kilimo ambapo  Sera hiyo inatarajia kupitishwa  mwezi  wa tisa na kwa  sasa yanakusanywa  maoni  kutoka kwa wadau mbalimbali nchini .

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner