WAANDISHI SUAMEDIA WASHIKA NAFASI YA PILI TUZO EJAT UPANDE WA TV 2019

Na Ayoub Mwigune

Waandishi wa habari wa SUAMEDIA Gerald Lwomile na Calvin Gwabara wameibuka miongoni mwa washindi katika nafasi ya pili katika mashindano ya Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania EJAT yanayoendeshwa na Baraza la Habari Tanzania MCT kwa mwaka 2018.

Waandishi hao ambao wameshirika katika katika mashindano hayo Calvin Gwabara kwa mara ya pili na Gerald Lwomile kwa mara ya kwanza wameshika nafasi ya pili katika makundi ya uandishi wa habari za Kilimo na Kilimo Biashara, Utalii na uhifadhi na Usalama wa Chakula na Vipodozi upande wa Televisheni.

IMG 7361Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Jaji Mtaafu Joseph Sinde Warioba aliyekuwa mmoja wa wageni mashuhuri katika tuzo za EJAT akiwa katika picha ya pamoja na Gerald Lwomile kushoto na kulia ni Calvin Gwabara.

Gerald Lwomile ambaye ameshiriki kwa mara ya kwanza ameshinda nafasi ya pili katika tuzo mbili na nafasi ya tatu katika tuzo moja, ameshika nafasi ya pili  katika kundi la uandishi wa habari za Utalii na Uhifadhi ambapo alipeleka makala za runinga zinazohusu Msitu wa Hifadhi Kimboza na Mti Vamizi wa Mrushia ambazo zote ni utafiti uliofanywa na Dkt. Charles Kilave mtafiti kutoka SUA huku pia akishika nafasi ya pili katika uandishi wa habari za Usalama wa Chakula na Vipodozi ambapo aliwasilisha makala mbili.

Naye Calvin Gwabara ambaye alikuwa mshindi wa kwanza wa Tuzo ya Uandishi wa Habari za Kilimo na Kilimo Biashara mwaka 2017 upande wa Radio mwaka huu amekuwa mshindi wa pili wa tuzo hizo upande wa Televisheni.

 

 

EJAT

Salome Kitomary( wa pili kulia), mshindi wa jumla wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania, EJAT 2018 iliyofanyika Juni 29, 2019 katika

Hoteli ya Golden Tulip iliyopo Oysterbay Dar es Salaam. Picha  na MCT.

 

Akizungumzia ushindi huo Lwomile amesema ushindi huo unatokana na ushirikiano mzuri baina ya watafiti wa SUA ambao wamekuwa tayari kutoa matokeo ya utafiti wao kwa umma ili kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo wakulima na wananchi kwa ujumla.

Aidha amesema ushirikiano na wafanyakazi wa SUAMEDIA umekuwa chachu ya ushindi huo ambapo wamekuwa wakipeana mawazo mbalimbali namna ya kuzalisha vipindi bora ambavyo vinalenga kuihabarisha jamii juu ya Kilimo na sayansi zingine zinazoendana na kilimo.   

 

Kwa upande  Calvin Gwabara ametoa wito kwa wafanyakazi wengine wa SUAMEDIA pamoja na waandishi wa habari nchini  kujikita katika kuandika na kuandaa habari ambazo zitaweza kutatua changamoto katika jamii inayowazunguka badala ya kuandika habari ambazo hazina msaada katika jamii huku akipongeza SUA kwa ushirikiano wao ambao wamekuwa wakitoa na kuwazesha katika kuandaa vipindi  vyao.

Aidha Gwabara amempongeza  Gerald Lwomile baada ya kujitokeza kwa mara ya kwanza na kuwania tuzo na kufanikiwa kushika nafasi  ya pili ya katika kundi la uandishi wa habari za Utalii na Uhifadhi na akishika nafasi ya pili katika uandishi wa habari za Usalama wa Chakula na Vipodozi akimtaka aendelee kujituma na kuwania tuzo nyingine/

Lwomile pia ameshika nafasi ya tatu katika wapiga picha mahiri wa televisheni huku nafasi ya kwanza ikienda Azam TV

 

Kwa mujibu wa MCT Jumla ya kazi 644 ziliwasilishwa kwa ajili ya kushindanishwa kwenye Tuzo hizi ambazo 176 (27%) kati ya hizo zimeletwa na waandishi wa habari wanawake huku zilizowasilishwa na waandishi wa habari wanaume zikiwa 468 (73%).

TUZO 1 1

Mzalishaji wa vipindi SUAMEDIA Gerald Lwomile mwenye suti akipokea cheti cha mshindi wa pili 

Kazi zilizowasilishwa zimetoka katika vyombo vya habari 67, ambapo Mwananchi Communications Ltd (MCL) ikiongoza kwa idadi ya kazi nyingi zaidi, zikiwa jumla 114 (14.1%) ikifuatiwa na The Guardian Ltd wakiwa na kazi 96 (11.9%).

IMG 7230Mzalishaji wa vipindi SUAMEDIA Calvin Gwabara mwenye suti akipokea cheti cha mshindi wa pili 

EJAT ni tukio la kila mwaka linaloandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa kushirikiana na washirika wake Wakfu wa vyom,bo vya habari (TMF), Taasisi ya habari ya Kusini mwa Afrika - (MISA-Tan) Chama cha Waandishi wa habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Jukwaa la Wahariri Tanzania Chama cha wamiliki wa Vyombo vya habari (MOAT) , (MOAT) Umoja wa Klabu za Habari Tanzania (UTPC), HakiElimu SIKIA and ANSAF.

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner