WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUFICHUA WALA RUSHWA

Na: Farida Mkongwe
Waandishi wa Habari mkoni Morogoro wametakiwa kuendelea kutoa elimu kuhusu rushwa na madhara yake sanjari na kuwatangaza wale wote wanaojihusisha
na vitendo vya kutoa na kupokea rushwa ambao wamekuwa wakirudisha nyuma maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoo Dkt. Kebwe Steven Kebwe akifungua Semina fupi kuhusu wajibu wa waandishi wa habari katika mapambano dhidi ya Rushwa.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoa wa Morogoro Bi. Janeth Machulya wakati akitoa
mada kwenye semina fupi ya waandishi wa habari iliyolenga kutoa elimu kuhusu wajibu wa waandishi wa habari katika mapambano dhidi ya rushwa nchini.
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Morogoro Bi. Janeth Machulya akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya wanahabari katka mapambano dhidi ya rushwa
 
Bi. Janeth amesema waandishi wa habari ni kiungo na daraja baina ya wananchi na serikali hivyo wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kufichua na kukemea
vitendo rushwa ambavyo vinafanywa na baadhi ya watu wakiwemo watumishi wa umma wasio waadilifu.
Awali akifungua semina hiyo mkuu wa mkoa wa Morogoro Bw.  Kebwe Steven Kebwe amesema katika mkoa huo bado kuna taasisi nne ambazo zimeonekana kuwa tatizo
katika suala la rushwa na kuzitaja taasisi hizo kuwa ni taasisi za kipolisi, mahakama, ardhi na serikali za mitaa na kuahidi kuendelea kuzishughulikia.
 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven Kebwe (wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waandishi wa habari wa Mkoa wa Morogoro
Amesema kwa sasa sehemu nyingi za taasisi za umma kuna mabadiliko katika utendaji kwani huduma nyingi zimeboreshwa hali inayosaidia ongezeko la kodi na
nidhamu ya matumizi ya fedha kwa watumishi wa serikali.

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner