Serikali inafurahishwa na hatua Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kusimamia Ithibati na Ubora wa Elimu

Na Gerald Lwomile

Dar es Salaam

Serikali imesema inafurahishwa na hatua zinazochukuliwa na Wizara ya Sayansi na Teknolojia katika kusimamia Ithibati na Ubora wa elimu unaotolewa na vyuo vikuu nchini vikiwemo vya umma na binafsi jambo linalosaidia kuwafanya wahitimu kuwa na soko la ajira ndani na nje ya nchi.

Hayo yamesemwa leo julai 17 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa uzinduzi rasmi wa maonesho ya vyuo vikuu wakati akizungumza na washiriki wa maonesho na wananchi katika viwanja vya mnazi mmoja jiji Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema uandaaji wa mitaala mbalimbali katika vyuo umeboreshwa kufuatia mafunzo yaliyotolewa na wizara hiyo na kuwa hatua zinachuliwa na vyuo mbalimbali vya kuhuisha mitaala na kuja na mitaala mipya ni jambo ambalo linainua ubora wa elimu nchini

waziri mkuu 2 min

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na washiriki wa maonesho ya vyuo vikuu katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam (Picha na Mariam Mwayela)

Waziri mkuu amesisitiza kuwepo kwa mitaala ambayo haiwaandai wahitimu kuajiriwa pekee lakini pia kuwepo na mitaala ambayo inawaandaa wahitimu kujiajiri, amesema kutokana na hali hiyo taifa litachochea hali ya ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu

“Bado nieendele kutoa wito kwa vyuo vikuu hapa nchini kuendelea kuhuisha mitaala ya elimu hiyo ili kutoa matokeo tunayoyatarajia”

Akitoa shukrani kwa Waziri Mkuu  baada ya kuzindua rasmi maonesho hayo Mwenyekiti wa Watendaji Wakuu wa Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu Vishiriki nchini ambaye pia ni Makamu wa  Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kutoa ushirikiano katika kuimarisha utendaji katika vyuo vikuu nchini.

Prof Chibunda min

 

Mwenyekiti wa Watendaji Wakuu wa Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu Vishiriki nchini ambaye pia ni Makamu wa  Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda akitoa neno la shukrani kwa serikali (Picha na Tatyana Selestine)

uboreshaji na upelekaji wa mikopo kwa wanafunzi katika vyuo vikuu nchini kwa kiasi kikubwa imeondoa tatizo la migomo katika vyuo vikuu nchini na kuwa Bodi ya Mikopo na Serikali kwa kiasi kikubwa vinatakiwa kupongezwa.

“Kwa niaba ya wasimamizi wa vyuo vikuu napenda kuishukuru sana serikali kwa hili ambalo tume wamelifanya la kumaliza uhakiki katika baadhi ya vyuo vikuu ambavyo vilikuwa vimefungiwa udahili na sasa vimeruhusiwa kuendelea na udahili tunaishukuru sana tume pamoja na serikali na nipende kutoa rai kwa tume kufanya uhakiki katika vyuo vikuu vilivyobaki” amesema Prof. Chibunda

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner