Bashungwa :Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara kuhakikisha zinashiriki katika Maonesho ya wakulima

Na Amina Hezron,
 Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa amezitaka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Viwanda na
Biashara kuhakikisha zinashiriki katika maonesho mbalimbali ya wakulima ili kuonesha Teknolojia zinazoweza kuwasaidia
wakulima katika kuongeza thamani ya mazao.
Mhe. Bashungwa amezungumza hayo alipotembelea katika Naenesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki yanayoendelea
kufanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere mkoani Mororogo amesema kuwa, ni vyema kama Taasisi hizo
zitashiriki kwakuwa endapo wakulima wataweza kuongeza thamani ya   mazao itasaidia kutengeneza ajira nchini na
kupeleka nje bidhaa ambazo zimekwishasindikwa tayari.
Aidha Mhe. Bashungwa amelitaka Jeshi la Kujenga Taifa JKT kuhakikisha linatafuta masoko ya kutosha ya nnje ya nchi ili
kuongeza kipato cha jeshi kitakachosaidia kuongezeka kwa ajira kwa vijana.
Mhe. Bashungwa amesema kuwa Jkt itumie fursa iliyopo ya baadhi ya  Mashirika yanayotafuta wazalishaji wa mazao
ya chakula kwaajili ya misaada katika nchi nyingine hivyo itaweza jiongezea kipato kupitia miradi yake.
 “Sasa JKT mkipata masoko kupitia miradi ambayo nimeiona hawa vijana mutawapa uhakika wa ajira  na hizi intake ambazo
zinaenda JKT zikifuzu zinaingia kwenye hiyo miradi”, amesema Mhe. Bashungwa.
Aidha Mhe. Bashungwa amewaahidi JKT kuwakutanisha na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani
(WFP) kwaajili ya ununuzi wa zao la mtama pamoja na Taasisi ya Tanzania Horticultural Association (TAHA) kwaajili ya
masoko ya Horticultural ulaya  huku akiwataka na wao kuangalia fursa zingine zilizopo.

Mhe. Bashungwa ameipongeza kamati ya maandalizi ya nane nane Kanda ya Mashariki kwa kuonyesha namna

tunavyoweza kufungamanisha kilimo na ujenzi wa viwanda. 

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner