Rais Mstaafu Jakaya Kikwete afurahishwa na hatua ya Watafiti wa SUA katika kuwasaidia wakulima kutatua changamoto

Na Amina Hezron,Morogoro

Raisi Mstaafu wa awamu ya nne Mh.Jakaya Mrisho Kikwete amewataka watafiti wa kilimo nchini kuongeza juhudi na ufanisi katika kufanya utafiti katika mazao ya kilimo na mifugo ili kuwawezesha wakulima kupata mbegu bora zitakazo wawezesha kuzalisha Kwa tija na kuongeza kipato katika mazao yao.

Hayo ameyasema leo alipotembelea katika banda la chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Sua katika maonesho ya nane nane ambapo pamoja na mambo mengine amewataka wakulima kufuata maelekezo ya wataalamu wa kilimo ili kuweza kwenda na ukuaji wa teknolojia na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Hata hivyo Mh. Kikwete amesema Maonesho ya nanenane ya mwaka huu yameboreshwa tofauti na miaka iliyopita hasa katika mabanda ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Sua hali inayobainisha ukomavu wa watafiti wa chuo hicho kwenye nyanja ya kilimo na mifugo.

IMG 2663

Aidha Mh.Kikwete ameeleza kufurahishwa na hatua waliofikia watafiti wa SUA katika kuwasaidia wakulima kutatua changamoto zinazowakabili zikiwemo mabadiliko ya tabia ya nchi.

Awali Mh Kikwete kabla ya kutembelea banda la Sua, alipata nafasi ya kutembelea
Mabanda mbalimbali ndani ya viwanja vya maonesho ili kujionea ukuaji wa Teknolojia mbalimbali za kilimo na mifugo.

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner