Wakazi wa Mkoa wa Morogoro na watanzania ujumla wametakiwa kutembelea SUA kipindi hiki cha nanenane

Wakazi wa mkoa wa Morogoro na watanzania kwa ujumla wanaotembelea maonesho ya
wakulima ya nanenane Kanda ya Mashariki wametakiwa kufika kwenye banda la Chuo Kikuu
cha Sokoine cha Kilimo SUA kujionea teknolojia mbalimbali zikiwemo za panya buku wanaogundua
mabomu yaliyotengwa ardhini.
Shaibu Hamisi Dutilo akionesha  panya mmojawapo aliyepo kwenye banda la SUA kwenye Maonesho ya Wakulima Nanenane Kanda ya Mashariki
Wito huo umetolewa na Mkufunzi wa mafunzo ya panya wa kugundua mabomu ya kutegwa ardhini
na kifua kikuu kwa njia ya kunusa SHAIBU HAMISI DUTILO kutoka kitengo cha APOPO kilichopo SUA wakati akizungumza na SUAMEDIA kuhusu kazi zinazofanywa na panya hao ambao wamepata mafunzo  kwa muda usiopungua miezi 8.
 
Panya Buku aliyepatiwa mafunzo maalum, kwa kusaidia kutegua mabomu na kugundua kifua kikuu
Akizungumzia mafunzo yanayotolewa kwa panya hao DUTILO amesema panya buku wanapata
mafunzo kuanzia hatua za awali hadi kukamilika kwa muda wa miezi minane na kwamba muda
huo unaweza kuongezeka iwapo panya hao watashindwa kufaulu mitihani wanayopewa kama
kipimo cha uelewa wao.
Amesema panya hao ambao wanakadiriwa kuwa na uwezo wa kuishi miaka 7 hadi 8  mpaka sasa
wameshapelekwa kufanya kazi hiyo kwenye nchi ya Cambodia, Angola na Msumbiji ambapo kwa
Msumbiji bado panya hao wapo wakiendelea na oparesheni za kugundua mabomu yaliyotegwa
ardhini.
Aidha Mkufunzi huyo wa Panya wa kugundua mabomu ya kutegwa ardhini na kifua kikuu kwa njia
ya kunusa amesema kwa sasa wana mpango wa kuwapeleka panya hao nchini Israel na Zimbabwe
kwa ajili ya kwenda kufanya kazi hiyo ya kugundua mabomu yaliyotegwa ardhini.
Kuhusu kifua kikuu DUTILO amesema kwa Tanzania wamekuwa wakichukua sampuli za
makohozi  kutoka hospitali mbalimbali na baadae sampuli hizo kupimwa kupitia panya hao na
kwa nje ya Tanzania tayari wanaendelea kugundua sampuli za makohozi yenye kifua kikuu katika
nchi ya Ethiopia na msumbiji.

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner