USINDIKAJI NI NJIA BORA YA KUOKOA MATUNDA YANAYOHARIBIKA KWA HARAKA

Na:Farida Mkongwe
Wakulima nchini wameshauriwa kusindika mazao yao yakiwemo mazao ya matunda ambayo
hayana uwezo wa kukaa muda mrefu bila kuharibika ili kuyaongezea thamani mazao hayo.
Ushauri huo umetolewa na Afisa Mkuu wa Maabara, Idara ya Teknolojia za chakula, Sayansi za
Lishe na Walaji kutoka Chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo SUA Bi. Gaudencia Mchotika wakati
akizungumza kwenye kipindi cha karibu Mezani kinachorushwa hewani na SUAFM.
Bi. Mchotika amesema mazao mengi ya matunda yakiwemo mapapai hayawezi kukaa muda mrefu
bila kuharibika lakini yakisindikwa yana uwezo wa kumpatia kipato mkulima na pia yanaweza
kuuzwa kwa bei kubwa kwa kuwa yameongezewa thamani.
Akitolea mfano wa mapapai, amesema matunda hayo hayapendwi sana kama ilivyo kwa matunda
mengine lakini kwa njia ya kuyasindika na kutengeneza bidhaa nyingine kama jam au chachandu
watu wengi wamekuwa wakiyapenda na hivyo kununuliwa kwa wingi.
Afisa Mkuu huyo wa Maabara, Idara ya Teknolojia za chakula, Sayansi za Lishe na walaji kutoka
SUA amewataka wakulima kujifunza teknolojia hiyo ya usindikaji na kuitumia mara kwa mara ili
kuepukana na hasara inayosababishwa na mazao ya matunda kuwahi kuharibika.

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner