WATANZANIA WATUMIE MFUMO WA AFYA DATA KUTOA TAARIFA KUHUSU DALILI ZA MAGONJWA

Na:Farida Mkongwe
Wakazi wa Mkoa wa Morogoro na watanzania kwa ujumla wameshauriwa kuutumia mfumo wa
Afyadata ambao unatoa taarifa za dalili za magonjwa mbalimbali kwa haraka na hivyo kuweza
kupata tiba itakayookoa maisha yao.

Ushauri huo umetolewa na Afisa Mtawala wa Mradi wa DODRES- SACIDS uliopo katika Chuo
Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Robert Maduka wakati akizungumza na SUAMEDIA kuhusu
umuhimu wa mfumo wa Afyadata kwa maisha ya binadamu.
Maduka amesema mfumo huo wa Afyadata unapatikana kwenye simu za Android na kwamba
anachotakiwa kufanya mtumiaji ni kupakua programu ya Afyadata na hapo ataweza kupata fomu
atakayojaza namna anavyojisikia na baadae atapata mrejesho wa dalili za ugonjwa alionao.
Akizungumzia changamoto zilizopo katika matumizi ya Afyadata amesema watu wengi na hasa
wanaoishi vijijini bado hawajawa na uelewa na mwamko wa kutosha kuhusu mfumo huo  na wao
wanaendelea kutoa elimu katika maeneo mbalimbali yakiwemo maeneo ya vijijini.
 
“Matumizi ya Afyadata siyo magumu kabisa cha msingi ni watu kuwa tayari kutumia teknolojia
mbalimbali ambazo zinajitokeza kwa sababu hakuna namna ya kuepukana na teknolojia za kisasa
katika karne hii ya sayansi na teknolojia”, alisema Afisa huyo.

 

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner