SUA YATEKELEZA AGIZO LA MHE. MAGUFULI KWA KUNUNUA MABASI MAWILI YENYE THAMANI YA SH. MIL .406.

 Na: Sada Mkwizu

Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)  Prof. Raphael Chibunda leo tarehe 23 August, 2019

amepokea na kuzindua rasmi mabasi mawili aina ya TATA yenye thamani ya shilingi. Mil. 406 yaliyonunuliwa

kutokana na mapato ya ndani ya chuo kufuatia agizo la Mhe. Rais  Dkt. John Pombe Magufuli la mwaka 2018.

Prof. Raphael Chibunda akikata utepe kwa kuzindua mabasi aina ya TATA katika Chuo Kikuu cha Sokoine
cha Kilimo SUA.(Picha na Gerald Lwomile) 
Akizindua mabasi hayo Prof. Chibunda amewashukuru wale wote waliohusika kufanikisha kununuliwa kwa
mabasi hayo na kusema kuwa yatasaidia kutatua changamoto ya usafiri kwa wanafunzi  iliyokuwa ikiwakabili
kwa muda mrefu.
Mabasi aina ya TATA yaliyozinduliwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA. (Picha na Gerald Lwomile) 
Aidha amewataka madereva, mafundi, wanafunzi na wafanyakazi kuyatunza mabasi hayo na kuhakikisha
yanatumika kuleta maendeleo na wepesi wa utendaji kazi kwa vitendo kwa wanafunzi na chuo kwa ujumla.
Prof. Raphael Chibunda akizindua mabasi yaliyonunuliwa kwa mapato ya ndani ya chuo Kikuu cha
Sokoine cha Kilimo SUA.(Picha na Gerald Lwomile) 

 
Katika picha ya pamoja Makamu wa Mkuu wa Chuo Prof. Raphael Chibunda katikati pamoja na
Menejiment ya chuo mara baada ya kuzindua mabasi yaliyopokelewa.(Picha na Gerald Lwomile).

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner