KKKT USHARIKA WA MAJENGO KUZINDUA SEMINA YA NENO LA MUNGU

          

Na: ALFRED LUKONGE

Mkuu wa Kanisa la Kilutheli jimbo la  Morogoro Mchungaji  Reginald Makule amesema waumini wajiandae  kufunguliwa  kifungo chochote  walichonacho  kama magonjwa, umaskini na  mapepo  kwakuwa wiki hii ni wiki ya kwenda kwa usalama kiroho.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

Mchungaji Makule ameyasema  hayo  wakati akifungua  semina  ya  neno  la  Mungu  katika  usharika  wa  Majengo  kata  ya  Kihonda  mkoani  Morogoro    Jumapili  ya  tarehe 8/11/2015   kwa kubainisha  “ tupo hapa  kama watu wenye njaa na kiu ya neno la Mungu kwakuwa kila siku ni jipya”.

Naye  mwezeshaji  katika  semina  hiyo  Mchungaji  Tamson  Mgala kutoka  Mbeya  amesema    unavyoishi  inaweza ikawa Mungu hataki  uishi namna hiyo hivyo semina hii itakupa njia za  kukutoa  hapo  ulipo”.

Kwa kuongezea Mchungaji Mgala amebainisha nyakati za sasa ni mbaya hivyo watu wanatakiwa kutubu kuepuka adhabu ya upanga kutoka kwa Yesu kristo.

Akiongelea  semina  hiyo  mwenyekiti  wa  kwaya  ya  Sayuni  Usharika wa Majengo Winfred  Ngulo amesema  kupitia semina  hiyo amejifunza katika  kumtumikia  Mungu kuna  roho za  kipepo zinafuatilia  watumishi maisha yao na hivyo  kutoa wito kwa watoa huduma makanisani  wamuangalie  Yesu Kung’oa roho hizo hili waanze  maisha mapya.

Vilevile Bi. Joyce Mongi ameongeza kwa  kusema semina  imemsaidia kumjua Mungu  vizuri kwa kuwa  kwenye  familia  nyingi kumjua  Mungu ni tatizo na  kutoa wito kwa watu wote  wahudhurie semina  hili wapate kufunguliwa.

Awali akizungumzia semina hiyo Mchungaji kiongozi wa Kanisa hilo Simon Loko aliwasihi waumini kuwa semina hiyo si ya wazee wa baraza, Mwinjilisti au wanakwaya bali ni ya watu wote hivyo wanatakiwa kuhudhuria kwa wingi kukuza uchaji wao kwa Mungu.

Semina hiyo itaendelea Kanisani  hapo hadi tarehe 15/11/2015  ikiongozwa na mada isemacho “ vitu vinavyotufanya tuwe hai  ni neno  la  Mungu”.

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner