TANAPA YAMPA TUZO MTAFITI WA SUA KWA UTAFITI BORA WA WANYAMAPORI

Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi TANAPA,  Bw. Godwell Ole Meing’ataki amekishukuru  Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo,SUA kwa mchango
mkubwa wanaoutoa kwa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi  TANAPA,Bw. Ole Meing’ataki akimkabidhi tuzo   Prof. Rudovick Kazwala kutoka Ndaki ya Tiba ya
wanyama na sayansi za afya yaChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo,SUA
 
Kamishna Ole Meing’ataki ameyasema hayo katika hafla fupi ya kukabidhi tuzo kwa   Prof. Ludovick Kazwara kutoka Ndaki ya Tiba ya wanyama na sayansi za
afya ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo,SUA iliyofanyika chuoni hapo.
Akikabidhi tuzo hiyo Kamishna Msaidizi wa uhifadhi  TANAPA,Bw. Ole Meing’ataki amekipongeza Chuo pamoja na Uongozi  kwa kupata tuzo hiyo, Pia kwa
mapokezi waliyofanya ambayo yameweka alama ya ushirikiano na umoja katika utendaji kazi nchini.
Amesema Tuzo hizo zinazotambulika kama TANAPA TOURISM AWARDS na ndio mara ya kwanza kutolewa zikiwa na vipengele mbalimbali
ikiwemo  cha kushindania Utafiti uliofanyika kwa muda mrefu ambao umebeba taarifa nyingi zilizosaidia katika Utalii. 
Amesema  kipengele hicho ndicho ambacho   Prof. Rudovick Kazwala ameibuka kinara kutoka kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, SUA. 
Akipokea tuzo hiyo Prof. Kazwala amesema amefurahi sana  kupata tuzo hiyo na hivyo kushauri wadau na wananchi kulinda hifadhi na vivutio mbalimbali
vya Taifa ili vizazi vijavyo viweze kunufaika na rasilimali hizo.
Amesema Tuzo hiyo ni ishara kwamba Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kina mchango mkubwa katika kusaidia uhifadhi wa wanyama na vivutio
vingine vya taifa.
Pia mshindi huyo wa tuzo hiyo  ameomba tafiti zinazolenga kuboresha afya za Wanyamapori na mimea zipewe kipaumbele ili kuweza kuleta tija kwenye
uhifadhi na  utalii nchini.
Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu kamishna huyo Makamu wa Mkuu wa Chuo Prof. Raphael Chibunda amesema tuzo hiyo ni heshima kwa
Mtafiti mwenyewe lakini pia ni hehima kwa Chuo.
Amewapongeza TANAPA kwa kutoa zawadi hizo kwa watu waliochangia kwenye kazi mbalimbali za kutunza na kuhifadhi utalii wa Tanzania kwani inaongeza
chachu ya watafiti na watu wengine kushiriki kwenye kutunza maliasili hizo za taifa.

Prof. Kazwara  ni mtafiti mzawa aliyebobea  ambaye amefanya tafiti ndani ya hifadhi za wanyamapori hasa  tafiti zinazolenga afya za wanyamapori nchini amepata tuzo hiyo kutokana na mchango wa tafiti hizo kwenye masuala ya utalii nchini. 

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner