Watafiti wa Tanzania wamegundua mbinu ya kukabiliana na Mbung’o kwa wanyama

Na: Calvin Gwabara

Watafiti wa Tanzania wamegundua mbinu ya kukabiliana na Mbung’o wanaosababisha  vimelea vya was  Nagana kwa wanyama na vimelea vya Ugonjwa wa malale kwa binadamu.

IMG 7485

Mtafiti Deusdedit Malulu akiwasilisha mada yake kwa waandishi wa habari na watafiti kwenye mafunzo hayo jijini Tanga.

Haya yamebainishwa na Afisa Utafiti Mifugo kutoka Wakala wa Maabara za Veterinary Kituo cha Tanga Bw. Deusdedit Malulu wakati wa mafunzo ya uandishi wa habari za sayansi,teknolojia na ubunifu yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na teknolojia COSTECH yaliyowakutanisha waaandishi wa habari na watafiti kutoka kanda ya Mashariki.

Bwana Malulu amesema katika kutafuta njia mbadala ya kukabiliana na Mbung’o wamebaini mnyama aina ya Kuro hashambuliwi na mbung’o kama wanyamapori wengine na kubaini kuwa mnyama huyo anatoa harufu ambayo mbung'o  huogopa na hivyo kushindwa kumkaribia.
IMG 7582
Amesema baada ya utafiti wao maabara wamebaini kuwa harufu hiyo inauwezo wa kufukuza Mbung’o kwa zaidi ya asilimia 60 ikilinganishwa na teknolojia zingine zilizopo sasa.

Bwana Malulu ameongeza kuwa baada ya kutambua kemikali zilizopo kwenye harufu hiyo ya Kuro wakachanganya kemikali za aina hiyo ili kuizalisha maabara inayofanana na ile ya Kuro na kuwakinga na kushambulia na Mbung'o hao.

Mtafiti huyo amebainisha kuwa ili kuhakikisha harufu hiyo inawafikia walengwa kwa maana ya wafugaji na hivi sasa wanatengeneza kifaa maalum ambacho kitakuwa kinabeba harufu.

“Hivi sasa tunashirikiana na Kiwanda cha A to Z cha Jijini Arusha katika kutengeneza kibebeo hicho cha harufu hiyo kwa mifugo” Alisema Bwana Malulu.

Ameongeza kuwa hatua hiyo ya kubuni kibebeo inakwenda sambamba na hatua za kufanya usajili na majaribio katika maeneo husika

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner