HAMASISHENI VIJANA KUSHIRIKI KILIMO ILI KISIBAKI KUWA CHA WAZEE- WARIOBA

Na Gerald Lwomile
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde
Warioba ameonya kuwa kama hakutafanyika juhudi za makusudi za kuwahamasisha vijana
kushiriki katika kilimo basi kilimo cha Tanzania kitabaki kwa wazee pekee.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji
Joseph Sinde Warioba akitoa nasaha zake kwa wajumbe wapya katika Baraza la chuo.

Jaji Warioba amesema hayo Septemba 25, 2019 wakati akifungua  Baraza jipya la chuo hicho
baada ya Baraza la awali kumaliza muda wake.
Akizungumza katika hafla hiyo Jaji Warioba amesema hivi sasa kuna wimbi kubwa la vijana
kuhama kutoka katika maeneo ya vijiji ambayo ndivyo vinashughulika zaidi na kilimo na
kukimbilia maeneo ya mijini ambako wanaamini kuna maisha bora zaidi.
Tulilenga chuo hiki kisaidie wakulima kwa maana pana, wakulima, wafugaji, wavuvi na
mambo ya misitu hali imeendelea kubadilika, kilimo chetu ni cha wakulima wadogo wadogo ,
chuo hiki kilipoanzishwa tulikuwa tunawajua wakulima hao walikuwa zaidi ni vijana sasa hivi
mambo yamebadiliki vijana wanakimbilia mjini kilimo chetu kimeanza kuwa cha wazee,
amesema Jaji Warioba.
Adha Jaji Warioba amesema mbali na mabadiliko hayo hata mazingira, sera na mfumo wa
uzalishaji duniani umebadilika hivyo ni muhimu kuwaona wakulima wadogo wadogo katika
jumuiya ya kimatifa. 
Amesema kuwa mabadiliko ya tabia nchi yamekuwa yakileta changamoto kubwa kwa
wakulima na kuwa SUA ndiyo kiongozi wa mawazo ya mafunzo ya namna ya kukabiliana na
changamoto hizo zinazowakabili wakulima, wafugaji na wavuvi
Inabidi tuangalie kwa sasa hivi tukoje na tujiandae vipi, je nini hatma ya mkulima mdogo
mdogo, nini hatma ya mfugaji sasa hivi, tuna wachungaji zaidi kuliko wafugaji huko
tunakokwenda tufanye nini, nini hatma ya mvuvi mdogo mdogo, matatizo yao ni makubwa
sana ukianzia mbegu bora, mbolea mazingira yao na tuone tunaweza kuwa na mawazo gani
kusaidia katika eneo hili, alisema jaji Warioba.
 Naye Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Jaji Mkuu Mstaafu
Othman Chande ameshukuru mamlaka za uteuzi kwa kukamilisha uteuzi wa wajumbe wa
Baraza hilo

Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Mhe. Jaji Mkuu Mstaafu Mohammed Chande Othman akizungumza katika hafla ya kuwakaribisha wajumbe wapya wa Baraza la chuo.
Amesema Baraza hilo lina mseto wa wajumbe wengi wakiwemo wanataaluma, sekta ya umma,
wataalamu na wawakilishi huku mseto huo ukiwa ndiyo hunaosababisha mambo mengi
kutekelezeka na kwamba mambo mengi ndani ya Baraza ni masuala ya majadiliano na kufikia
maamuzi ya pamoja
Awali akitoa taarifa ya Chuo, Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA
Prof. Raphael Chibunda amesema SUA imeendelea kutunza rasilimali zake ikiwa ni pamoja
na majengo, ardhi na misitu yake ya mafunzo ambayo pia hutumika kwa utafiti na mafunzo
kwa wanafunzi na shughuli za ugani kuwafundishia wakulima na wafugaji
Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Raphael Chibunda
akitoa historia ya chuo kwa wajumbe wapya waliochaguliwa katika Baraza la Chuo
katiaka hafla ya kuwakaribisha.
Baraza la Chuo cha SUA lina jumla ya wajumbe 14 na linaongozwa na Mwenyekiti wake
ambaye ni Jaji Mkuu Mstaafu Mohammed Chande Othman, wajumbe ni Prof. Raphael
Chibunda ambaye pia ni Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Prof.
Peter Gillah Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo Taaluma, Prof. Yasinta Mzanila Kaimu Naibu
wa Makamu wa Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha, Prof. Adolph Mkenda Katibu Mkuu Wizara
ya Maliasili na Prof. William Anangisye Makamu wa Mkuu wa Chuo, Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam
Wengine ni Dkt. Abubakar Hoza Mwenyekiti SUASA, Prof. Amelia Kivasi UDSM, Bw. Pius
Mponzi Kamishna Msaidizi Wizara ya Fedha na Mipango, Bibi Gaudensia Donati Mwenyekiti
RAAWU tawi la SUA, Bibi Maryam Saadalla Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili,
Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Bw. Dioniz Zacharia Rais SUASO, Bibi Maimuna Tarishi Katibu
Mkuu (Mst) Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge na Bibi Lunyamadzo Gillah ambaye ni Mwanasheria
wa Chuo na Katibu wa Baraza hilo.
KATIKA PICHA WAJUMBE WAPYA WAKIPATIWA  MIONGOZO NA NYARAKA ZA CHUO ZITAKAZOWASAIDIA KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO (PICHA NA MAWASILIANO NA MASOKO-SUA)

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner