Watafiti nchini wametakiwa kutumia vyombo vya habari nchini katika kufikisha matokeo ya tafiti zao

Watafiti nchini wametakiwa kutumia vyombo vya habari hapa nchini katika kufikisha matokeo ya tafiti zao ili ziweze
kuleta tija badala ya kuzitoa kwenye majarida ya kisayansi ya kimataifa ambayo hayasomwi na watanzania wengi ambao
ndio walengwa wa tafiti hizo.
Kaimu Mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa magonjwa ya binadamu  NIMR Amani cha Jijini
Tanga Dkt. Patrick Tungu wakati akiongea na waandishi wa habari kutoka Kanda ya Mashariki
Wito huo umetolewa Kaimu Mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa magonjwa ya binadamu  NIMR Amani cha Jijini Tanga
Dkt. Patrick Tungu wakati akiongea na waandishi wa habari kutoka Kanda ya Mashariki walitembelea kituo hicho wakiwa
kwenye mafunzo kwa vitendo ya namna ya kuandika habari za sayansi yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya sayansi na teknolo
jia.
Amesema kuna kazi nyingi zinafanywa na watafiti nchini lakini matunda yake hayaonekani vizurio kwa jamii na hivyo
mpango huo wa COSTECH unasaidia kuwezesha tafiti hizo kuweza kutoa mchango wake kwa jamii na taifa.
Kaimu Mkurugenzi huyo amesema NIMR Amani pia ni moja kati ya Taasisi muhimu ambayo imefanya tafiti ntingi lakini
kwa sehemu kubwa matokeo ya tafiti zao zimekuwa zikichapishwa kwenye majarida ya kisayansi ya kimataifa hivyo
kufuatia mafunzo hayo ya COSTECH sasa wataanza kushirikiana na Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini
katika kazi zao.
Kaimu Mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa magonjwa ya binadamu  NIMR Amani cha Jijini Tanga Dkt. Patrick Tungu wakati akiongea na waandishi wa habari kutoka Kanda ya Mashariki
Akizungumzia kituo chake Dkt.Tungu amesema kituo hicho kinasifika sana katika tafiti za udhibiti wa magonjwa yaenezwayo
na wadudu lakini pia kwenye tafiti za tabia,Biolojia mazingira ya wadudu waenezao magonjwa na namna ya kuwadhibiti.
Amesema moja kati ya utafiti muhimu ambao wameweza kuufanya na kuwa na mafanikio makubwa ni pamoja na ule wa
matumizi ya neti za kuzuia Mbu zilizowekwa dawa  (ITN) kwani matokeo yake yameleta faida kubwa na sifa ndani ya nchi
hadi jumuiya za kimataifa na Shirika la afya duniani WHO katika miaka ya 1990 na kuifanya kuwa sera. 
“Tunashinda marelia maana inaporomoka kwa zaidi ya asilimia 20 na ukiangalia hapo awali tulikuwa na asilimia 80 lakini
imeshuka hadi kwenye asilimia 20 hivyo tunajivunia kuona NIMR tunachangia katika kuondoa ugonjwa huu kwahiyo tafiti
zinazotoka hapa zimekuwa sio msaada tu kwa Tanzania pekee bali dunia kwa ujumla” Alisema Dkt. Tungu.
Amesema pia wamekuwa wakifanya tafiti juu ya usugu wa wadudu kwenye matumizi ya dawa ambapo waliwezesha kutoa
mapendekezo ya kubadilishwa kwa dawa mfano za malaria kutoka kwenye klorokwini, SP na  sasa Dawa mseto.
Kaimu Mkurugenzi huyo wa kituo cha NIMR Amani amesema pia wameweza kufanya tafiti ambazo zimewezesha kuboresha
mifumo ya afya hapa nchini na hivyo kusaidia katika eneo hilo muhimu katika sekta ya afya.

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner