VIONGOZI WA SERIKALI, WAFANYABIASHARA, JAMII NA WADAU WAKUMBUKE WALIKOTOKA

   

Na: TATYANA CELESTINE

Viongozi wa Serikali, wafanyabiashara, Jamii pamoja na Wadau mbalimbali nchini wametakiwa kukumbuka walikotoka hasa katika Sekta ya Elimu kwa kutoa msaada na kuboresha miundo mbinu mbalimbali katika mashule na maeneo mengine ya nayogusa jamii moja kwamoja

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

Hayo yamesemwa na Mgeni Rasmi Bi Tatyana Celestine katika mahafali ya watoto wa shule ya awali na hafla ya ufunguzi wa Jiko katika Shule ya Msingi Bungo iliyopo Manispaa ya Morogoro hivi karibuni

Bi Tatyana amesema Selikalini kuna viongozi wengi na wamesoma katika shule mbalimbali ambazo hali yake kimazingira pamoja na miundombinu si nzuri hivyo wanatakiwa kukumbuka walikotoka na kupeleka misaada bila kusubiria mafungu ya bajeti ndio kufanya ukarabati wa baadhi ya maeneo kwani wakati mwingine fedha hizo huchelewa au kutotosheleza kwa shule zote Tanzania

Aidha amewapongeza wanafunzi waliomaliza katika shule ya Msingi Bungo mwaka 1997 kwa moyo wao wakujitolea fedha nyingi na kukamilisha kujenga jiko kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho kitaka chosoma shuleni hapo kwani wamekuwa mfano wakuigwa na jamii

Naye Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Manispaaya Morogoro Bwana Sultan Mzuzuri amesema yeye amehamasishwa sana na kitendo cha vijana waliomaliza shuleni hapo mwaka 1997 na kumfanya nae aende kutoa shukrani zake Shule ya Mshingi Kikundi iliyopo Manispaaya Morogoro aliposoma kwani anajiskia vibaya mpaka umri alionao hakuwahikufikiria kusaidia chochote katika shule hiyo lakini kutokana na mualiko huu katika shule ya Bungo umeamsha hisia zake na kuamua kufanya kitu.

Aidha Mshtahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Bwana Amir Nondo alielezea hisia zake kwa kile kilichofanyika shuleni hapo na kusema kuwa yeye kama Kiongozi katika Kata yake amefarijika kuona kuna watu wanafanya maendeleo katika eneo lake kwa kutumia gharama zao wenyewe hii inaonesha hali ya kujitoa na uzalendo katika nchi yao.

“nilipopata mwaliko huu nilishindwa kuacha kuja kutokana na thamani waliyonipa wanafunzi hawa ambao wanaishi katika mikoa tofauti kwa mapenzi yao na shule hii wameamua kutujengea jiko nimefarijika sana kwani wameonesha uzalendo wa kutosha wanapaswa kuigwa hata na sisi viongozi’’ alisema Nondo.

Kwa upande wao watoto waliohitimu shule ya awali walitoa shukrani zao kwa Mgeni Rasmi na Familia ya Bungo 1997 kuweza kuwaondolea kero ya kupikiwa chakula kwenye mazingira hatarishi hasa kipindi cha mvua kwani ilikuwa ni rahisikupata magonjwa ya mlipuko hivyo wanazidi kuomba kuendelea kuwasaidia kadri Mungu atakavyowawezesha kutokana na shule hiyo bado inamatatizo mengi yanayowakabili

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner