Watafiti kituo cha Utafiti wa mifugo cha TALIRI Tanga wamegundua aina ya maharage yenye kiwango sawa cha protini na soya

Watafiti kituo cha Utafiti wa mifugo cha TALIRI Tanga wamegundua aina ya maharage meupe (canavaria ensiformis) yenye kiwango cha protini sawa na kile kilicho kwenye soya ili
kusaidia kuongeza upatikanaji wa kirutubisho hicho kwa wazalishaji wa chakula cha mifugo.

Akizungumza na Waandishi wa habari kutoka Kanda ya Mashariki waliokuwa kwenye mafunzo ya Uandishi wa habari za sayansi yaliyoandaliwa

na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH,Mkurugenzi wa kituo hicho Dkt. Zabron Nziku amesema kupatikana kwa aina hiyo ya mbegu

ya maharage ni mkombozi kwa wafugaji nchini.

Amesema kwa miaka mingi waqzalishaji wa chakula cha mifugo na wafugaji wamekuwa wakitumia Soya kama chanzo cha Protini kwenye chakula cha
wanyama lakini pia imekuwa ikitumiwa na binadamu kwa kiasi kikubwa kama chanzo cha protini lakini sasa kupatikana canavalia ensiformis
kutapunguza kutumia soya kwenye chakula cha mifugo.
“Haya ni mbadala wa soya yana kiwango sawa na soya na kwa wale wenye viwanda vya kutengeneza vyakula vya mifugo mbalimbali tunachokifanya ni
kuzalisha kwa wingi na kuwauzia na haya majani yake ambauyo ni chakula pia ambacho ukichanganya na maharage haya unapata pilau kwa mnyama
kama ilivyo pilaukwa binadamu ” Alisistiza Dkt. Nziku.
Dkt. Nziku amesema pamoja na kuwa na  sifa sawa na Soya Kwenye kiwango cha Protini lakini pia Maharage hayo meupe waliyogundua yana umbo kubwa
ikilinganishwa na Soya lakini pia yanaza sana na hivyo kuwezesha wazalishaji wa malisho na chakula cha mifugo kuzalisha kwa wingi katika ekari.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Kwa upande wake Flora Lukindo ambaye ni meneja wa uzalishaji wa teknolojia kituoni hapa amesema kuwa kwa mbegu hizo wafugaji wamezichangamkia
sana na kwakuwa zinaweza kuchangwa kwenye chakula cha kuku na nguruwe ambapo kwa mifugo inayocheua wanakula majani lakini kwa ile isiyocheua
wanakula mbegu hizo.

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner