WAKULIMA WAMETAKIWA KUPIMA UDONGO ILI KUJUA ZAO NA MBOLEA INAFOFAA KABLA YA KULIMA

Mtafiti Kiongozi wa Tathimini ya Rasilimali Ardhi  nchini Dkt. Sibawei Mwango kutoka Kituo cha Utafiti wa kilimo TARI Mlingano cha Mkoani Tanga
Wakulima na wale wanaohitaji kuingia kwenye kilimo wametakiwa kuhakikisha wanapima udongo kwanza ili kujua zao na aina ya mbolea inafofaa kwakuwa sio kila zao linastawi kwenye kila udongo na kila mbolea inawekwa kwa kila zao.

Wito huo umetolewa na Mtafiti Kiongozi wa Tathimini ya Rasilimali Ardhi  nchini Dkt. Sibawei Mwango kutoka Kituo cha Utafiti wa kilimo TARI Mlingano cha Mkoani Tanga wakati akiongea na Waandishi wa habari na watafiti waliotembelea kituoni hapo kujifunza kazi mbalimbali zinazofanywa na watafiti wa kituo hicho katika kusaidia wakulima nchini.

Dkt. Mwango amesema watu wengi wanaoingia kwenye kilimo huwa kitu cha kwanza wanaangalia wapi waatapata mbegu, madawa na Mbolea lakini hawaangalii hiyo mbegu na mbolea wanakwenda kuipanda wapi bila kujua kuwa aina ya udongo wa shamba lake unafaa kulimwa zao gani na unahitaji mbolea gani.
“Mafanikio yote ya Kilimo yanaanza kwa mkulima kujua udongo wake kwa sababu si kila udongo unafaa kila zao maana kila zao lina udongo unaofaa lakini pia sio kila mbolea inafaa kwenye kila zao na hapo ndio wakulima wengi wanakwama na kufanya kilimo hakiendi mbele japokuwa kuna tafiti nyingi za mbegu,Mbolea na Madawa zinazalishwa kila siku na watafiti nchini” Alisisitiza Dkt. Mwango.

Dkt. Mwango amesisitiza kuwa Kila udongo una mbolea zake ambazo zikitumika vyema zinaweza kumpatia mkulima tija na pale mkulima napokosea na kuweka mbolea isyofaa kwenye udongo Fulani hupelekea kupunguza tija na hata kupata hasara kabisa.
“Kwa hapa Tanzania tuna mbolea za aina mbili ambazo ndizo zinatumiwa sana na wakulima wengi kitu ambacho sio sahihi maana kila zao lina mbolea yake kutegemeana na nini unachotaka kuzalisha, mfano unalima miwa ili kupata sukari wewe unaweka mbolea ya yurea ambayo kazi yake ni kuzalisha majani wakati wewe unataka sukari ya kutosha na utakapopeleka kiwandani watapima wingi wa sukari na kwenye muwa na sio ukubwa wa muwa” Alifafanua Dkt. Mwango.
Mtafiti huyo Kiongozi wa tathimini ya rasilimali ardhi  katika kituo cha utafiti wa Kilimo cha TARI Mlingano amesema hivi saa watu wengi wanaingia kwenye kilimo maana kimekuwa ni biashara hivyo Wanahabari watumie vyombo vyao kuwaelekeza wakulima wa wadau wengine umuhimu wa kulima kilimo bora cha kisasa na kinachozingatia mbinu zote za kilimo.
Kwa upande wake Mkuu wa kituo hicho ya TARI Mlingano Dkt. Catherine Senkoro amesema kuwa kituo hicho ndicho kilichopewa dhamana ya kitaifa ya kufanya tafiti za rasilimali ardhi kwenye maeneo yanayolimwa na baada ya tafiti hizo wanatoa mapendekezo ya namna ya kutumia vizuri ili kuhakikisha kilimo kinakuwa endelevu.
“Tunatoa matumizi sahihi ya mbolea, Nmana ya kutunza vizuri mazingira kama ni maeneo ya milima na hata haya ya kawaida na kila wakati mapendekezo hayo tunayotoa tunayatathimini upya kwa sababu wakulima wanayatumia kila wakati na hivyo kila baada ya miaka mitatu afya ya udongo  inawezekana ikawa imebadirika”. Alifafanua Dkt. Senkoro.
Mkuu wa kituo hicho ya TARI Mlingano Dkt. Catherine Senkoro akielezea utafiti unaofanywa na kituo chake
kwenye maswala ya udongo kwa Waandishi wa Habari.
Dkt. Senkoro amesema kituo hicho kimewza kutoa ramani inayoonyesha aina za udogo zilizopo Tanzania lakini hivi karibuni pia wameweza kufanya utafiti wa kujua afya ya udongo ilivyo kwa sasa nchini na kutoa ramani mbili, moja ikionyesha hali halisi ya kemikali ya udongo yaani (Soil Ph) na nyingine ni hali halisi ya Mboji au rutuba na hivyo zitasaidia kwenye kuweka mipango mbalimbali kama nchi ya kuboresha na kuinua sekta ya kilimo.
“Lakini pia tumetoa maendekezo mbalimbali ya mbolea maaana kila wakati tunatakiwa kufanya hivyo kwahiyo tunamapenendekezo ya mbolea toka mwaka 1983, tukafanya tena mwaka 1993, alafu tunatoa tena mwaka 2014, na mwaka 2017 tumetoa tena mapendekezo mengine ya mbolea katika mazao 14 na tunayatumia kwenye maeneo mbalimbali na tunafanya vizuri” Alibainisha Dkt. Senkoro.
Amesema na sasa wanashirikiana na wadau wengine maana ile tathimini waliyoifanya wameona upungufu wa virutubisho vingi lakini wakulima wanatumia mbolea aina mbili ya  Yurea na DAP na kwakuwa kila mwaka wakulima wanalima virutubisho vingine vinapungua kwenye udongo maana udongo ni kama stoo ya virutubisho.
Amesema ktika kuonyesha hilo kwa vitendo wameweka mashamba darasa ya matumizi ya mbolea kwenye halmashauri 29 nchini  na OCP Afrika ambao wanafanya nao kazi wanaamini sasa mbolea mbalimbali zinazohitajika kwenye eneo husika zinapatikana maana mahitaji yamekuwa makubwa kwenye maeneo ambayo wameweka mashamba darasa ya matumizi ya mbolea mbalimbali wanazopendekeza.

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner