VIONGOZI WAMEASWA KUKATAA KUTUMIKIWA BALI KUSIKILIZA NA KUTATUA CHANGAMOTO

Na: Mwandishi wetu
Viongozi  wameaswa kukataa kutumikiwa na kuwaogopesha watumishi wao, hivyo wameshauriwa kuwasikiliza
na kutatua changamoto mbalimbali za watumishi na wateja wao pindi wanapoleta shida zao. 

Wito huo umetolewa na Naibu wa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo  (Utawala na Fedha)
Mstaafu, Prof. Yonika Ngaga wakati akipokea zawadi ya Ngao ya Utumishi uliotukuka katika hafla fupi ya
kumkaribisha rasmi  ndani ya Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii iliyofanyika tarehe 02 Oktoba 2019
katika viwanja vya Ndaki hiyo chuoni SUA.
Akitoa shukrani kwa  uongozi na watumishi wote  wa Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii , Prof. Ngaga
amesema amefurahishwa na mapokezi aliyoyapata, hivyo ameahidi kushirikiana vyema na Ndaki hiyo ili kuweza
kuleta tija na maendeleo husika.
Kwa upande wake   Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo (Taaluma) Prof. Peter Gillah amempongeza Rasi wa
Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii, Prof.   John Kessy kwa utaratibu anaoufanya wa kutambua juhudi za
viongozi wanaotoka katika ndaki hiyo na ameshauri utaratibu huo uendelee kwa sababu unaleta faraja na
ushirikiano katika kazi za kimaendeleo chuoni humo.
Na pia amempongeza Prof. Ngaga kwa uongozi mzuri katika  kipindi chote cha uongozi wake akiwa kama
Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo (Utawala na Fedha) 2014-2018.
Kwa upande wa Prof. Kessy ametoa shukrani kwa wote walioshiriki katika kubadhibhi zawadi hiyo na pia
ameahidi kuendeleza utamaduni huo ili kuongeza ushirikiano na maendeleo chuoni SUA.

 

                                                  

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner