SUA YATAMANI WATANZANIA KUJITOSHELEZA KWA KITOWEO CHA SAMAKI

WhatsApp Image 2019 10 08 at 6.35.19 AM

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa ICE Dr. Babili (katikati),Prof. Sebastian Chenyambuga na washiriki wa mafunzo katika picha ya pamoja baada ya kufungua mafunzo ya ufugaji wa samaki ambayo yanafanyika Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo SUA .(PICHA NA GERALD LWOMILE)

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kupitia Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza ICE kimesema kinatamani kuona watanzania wanajitosheleza katika upatikanaji wa kitoeo aina ya samaki.

Hayo yamesemwa leo Octoba 7, 2019, na Dkt. Innocent Babili ambaye amemuwakilisha Mkurugenzi ICE Prof. Dismas Mwaseba wakati akifungua mafunzo ya ufugaji wa samaki ambayo yanafanyika Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo SUA .

Dkt. Babili amesema wafugaji wa samaki Tanzania ambao wamepata fursa ya kujifunza ufugaji wa samaki   kama watayaweka kwa vitendo nchi inaweza kujitosheleza kwa kitoweo na kukuza uchumi wa nchi na kipato katika jamii.

Dkt.Babili ameongeza kuwa ya ICE ambayo ndiyo imeandaa mafunzo hayo ni kiunganishi kati ya chuo na jamii kwa lengo la kusaidia kupata matokeo mbalimbali ya tafiti, ubunifu na teknolojia mbalimbali na kuweza kuziweka kwa vitendo.

Nae mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo Prof. Sebastian Chenyambuga kutoka Idara ya Sayansi za Wanyama,Ufugaji wa Viumbe Majini na Nyanda za Malisho amewashauri wadau wa mafunzo hayo kutumia mbinu bora za ufugaji wa samaki kwa kutumia vyanzo mbalimbali kama vile mabwawa ya asili, mabwawa ya kuchimbwa na vizimba ili kupata mavuno yaliyo bora ya samaki.

Wakizungumzia mafunzo hayo baadhi ya washiriki akiweno Bw.Albert Lusekelo na Bibi Debora Twebe wote kutokea jijini Dar-es-salaam wamesema wengi wao wamezoea kufuga samaki kienyeji hivyo, mafunzo hayo yanaenda kupelekea kufuga samaki kisasa kwa ajili ya biashara ili ufugaji wa samaki uwe endelevu kutokana na kuongeza kwa watumiaji wa samaki.

Naye, Bi.Debora Twebe kutoka Dar-es-salaam ameeleza kuwa mafunzo hayo yatamsaidia kuweza kupata fursa ya biashara ndani na nje ya nchi kutokana na mbinu mbalimbali za kuzitumia ambazo amezipata katika mafunzo hayo ya ufugaji wa samaki

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner