SUA yabaini Samaki katika Ziwa Victoria na walaji wapo salama kufuatia hofu ya matumizi ya sumu wakati wa uvuvi na utunzaji wa Samaki.

Na: Calvin E Gwabara
Utafiti uliofanywa na Watafiti wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kupitia mradi wa Ubunifu wa teknolojia mbalimbali na Masoko ya Uvuvi kwa Ziwa Victoria (IMLAF) kwa
kushirikiana na wadau wengine umebaini  kuwa Samaki katika Ziwa Victoria na walaji wapo salama kufuatia hofu ya matumizi ya sumu wakati wa uvuvi na utunzaji wa Samaki.
 
 
 
 
 
 
 
Hayo yamebainishwa na Dkt. Alex Wenaty Ngungulu kutoka Idara ya Teknolojia  ya Chakula na Sayansi ya Lishe na Mlaji katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo SUA mara baada ya kukamilisha Utafiti wake uliokuwa unaangalia kemikali zinazoweza kuathiri samaki wa ziwa victoria na mlaji.
Dkt. Wenaty amesema mara kwa mara jamii imekuwa ikilalamikia matumizi ya sumu na kemikali zingine zinazotumiwa na wavuvi katika kuua wadudu na
kutunza samaki katika Ziwa Victoria na hivyo kuzua hofu miongoni mwao na hata kuathiri biashara ya samaki ndani na hata nje ya nchi.
Amesema wao kama watafiti kupitia mradi huo wa IMLAF wakaamua kufanya utafiti huo kwa kuangalia viuatilifu 21 vyeye chlorine (yaani organochlorine
pesticides) lakini kati ya hivyo walibaini kuwepo kwa viuatilifu 9 tu kwenye Samaki wanaotoka Ziwa Victoria.
Dkt. Wenaty amesema baada ya kuvipata wakavifanyia uchunguzi wa kina na kubaini kuwa vipo kwa kiasi kidogo sana kwenye Samaki hao ambacho
kinakubalika kimataifa kwani shirika la afya duniani WHO na shirika la chakula duniani FAO wana miongozo yao ambayo inasema ili Samaki afae kuliwa
anatakiwa asiwe na kiwango kinachozidi microgram  300 kwenye kila kilo moja ya samaki.
Amesema kwa Samaki wanaotoka Ziwa Victoria wamekuta kiwango kilichokuwa kikubwa zaidi ni  DDT ambacho kilifikia hadi microgram 13 kwenye kila kilo
moja ya Samaki kiwango ambacho ni kidogo mno ikilinganishwa na kiwango kinachotakiwa Kimataifa.
Hivyo ametumia nafasi hiyo kuwatoa hofu walaji wa Samaki toka Ziwa Victoria kuwa samaki na ziwa hilo lipo salama hivyo wasihofu usalama wa afya zao
huku akiwataka wavuvi na wasafirishaji wa samaki kutotumia kemikali hizo ambazo zinadhaniwa wanazitumia ili kuendelea kulinda samaki na walaji pamoja
na ziwa hilo kwa ujumla.
Mradi huo wa IMLAF ulianza utafiti wake mwaka 2015 na umemaliza muda wake mwaka huu mwaka huu wa 2019 ambapo ulikuwa unafanya kazi kwenye
Ziwa Victoria katika mikoa ya Mwanza,Mara na Kagera kwa ufadhili wa serikali ya Denmark na Tanzania.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
ZIWA VICTORIA KWA HISANI YA MTANDAO
 

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner