Zaidi ya shilingi bilioni 11 zimetolewa kama mikopo kwa wadau mbalimbali kwenye Sekta ya uvuvi

Na: Calvin E. Gwabara
Zaidi ya shilingi bilioni 11 zimetolewa kama mikopo kwa wadau mbalimbali kwenye Sekta ya uvuvi katika mwaka
wa fedha wa 2018/2019 katika benki ya TADB  ili kusaidia kuboresha miundombinu na mitaji baada ya kuanzishwa
kwa dawati la sekta binafsi katika wizara hiyo.

 
  Katibu Mkuu wizara ya Mifugo na uvuvi anayeshughulikia sekta ya uvuvi akifafanua jambo kuhusu mradi huo
 
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi Dkt. Rashid
Tamatama  wakati akizungumza na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA waliokuwa wanafanya
Utafiti kupitia Mradi wa  Ubunifu wa teknolojia mbalimbali na Masoko ya Uvuvi kwa Ziwa Victoria (IMLAF).
Amesema katika kipindi cha miaka miwili hadi mitatu iliyopita hakuna fedha zozote zilizotolewa na benki hiyo ya
TADB kama mikopo kwenda kwenye sekta ya uvuvi lakini bada ya kuanzishwa kwa dawati hilo kumesaidia
kupatikana kwa fedha hizo kwa wadau wa uvuvi na sasa kuna fedha zingine zaidi ya shilingi bilioni 22 zipo kwenye
hatua mbalimbali ili ziweze kukopeshwa kwa wadau.
”Matokeo mazuri ya Utafiti wa  mradi huu uliofanywa na watafiti wa SUA  yatasaidia kuweka kwenye mikakati
mbalimbali ya wizara yangu ili kuinua Sekta ya Uvuvi na hivyo nitoe pongezi zangu na za wizara kwa SUA kwa kazi
hii nzuri iliyofanywa na watafiti hao kupitia mradi huo wa IMLAF“ Alisema Dkt. Tamatama.
Katibu Mkuu huyo anayeshughulikia sekta ya Uvuvi ameongeza kuwa hivi sasa wanaendelea na zoezi la
kuhamasisha wavuvi kujiunga kwenye vikundi ili iwe rahisi wao kokopesheka na tayari wamefanikiwa
kuishawishi benki ya Posta kuanzisha akaunti maalumu inayoitwa Mvuvi  akaunti kwaajuili ya vikundi vya wavuvi nchini.
Amesema wachakataji hao wa dagaa endapo wataweza kutumia fursa hiyo ya mikopo wataweza kujenga
miundombinu bora nay a kisasa ya kukaushia dagaa haoa na hivyo kusaidia kuongeza thamani ya dagaa kwa
kutokuanika kwenye mchanga ambapo soko la Zambia wananunuliwa kilo moja kwa dolla 6 kwa sasa.
Akizungumzia utafiti huo uliofanywa na watafiti katika Chuo chake Makamu wa mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine
cha Kilimo SUA Prof.Raphael Chibunda amesema uvuvi wa dagaaa ni wa siku nyingi katika Ziwa Victoria na hawa
Samaki sio kama wanatumiwa na binadamu pekee  lakini pia wanatumika kwenye kutengeneza chakula cha mifugo.
Prof. Chibunda amesema Utafiti huo kupitia  Mradi wa Ubunifu wa teknolojia mbalimbali na Masoko ya Uvuvi
kwa Ziwa Victoria (IMLAF)  ulilenga kuboresha mazao ya samaki kutoka kwenye ziwa hilo ili wavuvi wanufaike
zaidia kwenye kazia mbayo wamekuwa awakiifanya.
”Kwa taarifa tulizonazo matokeo ya utafiti huu yamepokelewa vizuri na kwa sehemu kubwa hasa utumiaji wa
vichanja na neti umeenea na wavuvi wengi wanatumia na zao la dagaa limeboreka kwahiyo ni matumaini yetu
kuwa mradi unapokaribia mwisho, viongozi wa serikali na wale wa kijamii ambao mradi huu umefika kwenye
maeneo yao wataendelea kuwahimiza wavuvi kutumia njia hizi ambazo ni bora zitakazowaongezea kipato na
kipato cha nchi yetu” Alisisitiza Prof. Chibunda.
Ameongeza kuwa  pamoja na ziwa kuwa na Samaki mbalimbali watafiti wake walijikita zaidi  kwenye Samaki
wanaopendwa na kutumika Zaidi nchini Tanzania hasa Dagaa ambao soko lake limepanuka na kufika kwenye
nchi mbalimbali za jirani Kongo, Burundi na Zambia na kusaidia nchi kupata fedha za kigeni na kupunguza
Umasikini katika kaya za Wavuvi.
 
Katibu Mkuu akizungumza jambo na watafiti wa mradi wa IMLAF nje ya ofisi yake jijini Dodoma
katibu mkuu akiwa kwenye picha ya pamoja na watafiti wa mradi wa IMLAF kutoka SUA
katibu mkuu akiwa kwenye picha ya pamoja na watafiti wa mradi wa IMLAF kutoka SUA
SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner