SUA YATAKIWA KUENDELEZA VIWANGO VYA ELIMU BORA

Na, Catherine Mangula Ogessa.

Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es salaam Mhe. Jaji Mstaafu Damian Lubuva amekitaka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)  kuendeleza viwango vya ubora wa elimu ambayo imekuwa ikitolewa na chuo hicho, lakini pia akikipongeza chuo hicho kwa kuwa na muonekano wa nje  unaoakisi kuwa chuo hicho ni chuo cha Kilimo.

PICHA JANA NA LEO

Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es salaam Jaji Mstaafu Damian Lubuva akizungumza na Menejimenti ya SUA. 

 

Jaji Mstaafu Lubuva ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika Chuo Kikuu SUA, ziara ambayo imekuwa na lengo la kujifunza sanjari na kuimarisha urafiki uliopo baina ya vyuo hivyo viwili, huku akisisitiza vyuo hivyo kila kimoja kutaka kujifunza toka kwa mwenzake kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma.

Amevitaka vyuo hivyo kuendeleza ushirikiano ikizingatiwa kuwa mbali na vyuo hivyo kuwa ni vya umma lakini pia historia iko wazi kuwa chuo cha SUA kimezaliwa toka Chuo cha Dar es salaam, hivyo mahusiano mazuri ya vyuo hivyo sio tu kwa manufaa yao bali ni kwaajili ya Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Makamu wa Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es salaam Prof. William Andley Lazaro Anangisye  amewataka watumishi wa vyuo kuhakikisha wanaweka mbele kwanza maslahi ya vyuo na Taifa kwa ujumla hivyo wasitangulize pesa mbele kwani kwa nafasi zao wanadhamana ya kuleta mabadiliko chanya.

Amefafanu kuwa ni muhimu kila mmoja kuhakikisha anatimiza wajibu wake katika kuhakikisha malengo ya chuo husika yanafikiwa na baadae kunakuwa na kitu kwaajili ya Watanzania ambacho kimefanyika. Lakini pia amebainisha kuwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kimekuwa kinajifunza  mambo mengi kutoka SUA.

Aidha katika ziara ya Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es salaam  pia ameweza kutembelea shamba la mfano, Apopo, Hospitali ya Rufaa ya Wanyama, Maabara ya Sayansi ya udongo, SUA AIC, Hospitali ya Mazimbu pamoaja na Makaburi ya Mazimbu.

 picha tena zipo

Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Prof. William Andley Lazaro Anangisye.

 

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner