WAZIRI WA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA PROF. JOYCE NDALICHAKO AMEZITAKA TAASISI ZA ELIMU NCHINI KUWA MSTARI WA MBELE KATIKA KUIMARISHA SEKTA YA MICHEZO

Na AYOUB MWIGUNE NA AMINA HEZRON

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amezitaka Taasisi za Elimu nchini kuwa mstari wa mbele katika kuimalisha sekta ya michezo kwenye Taasisi  kwani kutaimalisha afya pamoja na kuinua viwango vya elimu na uwajibikaji  nchini.

WhatsApp Image 2019 11 01 at 9.12.19 PM

Waziri huyo ameyasema hayo wakati wa kufunga michezo ya Wafanyakazi wa wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA na kuzindua uwanja wa mchezo wa kikapu katika Kampasi Kuu ya Chuo hicho ambapo amesisitiza kuwa michezo ni chanzo cha afya bora kwa watu wote na kuzitaka taasisi kuhakikisha zinatambua umuhimu wa michezo na kuipa kipaumbele

WhatsApp Image 2019 11 01 at 9.10.06 PM

Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA  Pro. Raphael Chibunda amesema kukamilika kwa mashindano hayo kumeboresha mahusiano kati ya wafanyakazi wa chuo hicho pamoja na wanafunzi huku pia akishukuru Benki ya CRDB kwa kuendelea kushirikia na na chuo hicho katika nyanja mbalimbali huku akiwaomba kuendelea kushirikiana na chuo cha sokoine ili kuweza umoja na kuwa karibu na wateja wake ambao ni wanajumuiya hiyo 

WhatsApp Image 2019 11 01 at 9.14.30 PM

Kwa upande wake Mkurugenzi wa wateja wa Benki ya CRDB Morogoro Prosper  Nambaya kama mdau ambaye pia amejitokeza katika kuhakikisha uwanja wa michezo wa mpira wa kikapu unakamilika amesema wao kama benki watahakikisha wanaendelea kutoa sehemu ya faida katika kusaidia jamii na miradi mbalimbali     

 

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner