WAKAZI WA MOROGORO WATOA MAONI YAO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

WAKAZI WA MOROGORO WATOA MAONI YAO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

 Na:AMINA B. MAMBO

Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Morogoro  ambao ni wanachama wa  Chama Cha Mapinduzi wameonekana kuvutiwa na umati wa wananchi waliojitokeza kumpokea mgombea urais wa ukawa kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo chadema huku wakidai kuwa mkusanyiko huo unaonesha ni kwa kiasi gani wananchi wanahitaji babadiliko. 

Bofya kichwa cha habari kwa habari zaidi.......

 Na: Amina Bashir Mambo

Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Morogoro  ambao ni wanachama wa  Chama Cha Mapinduzi wameonekana kuvutiwa na umati wa wananchi waliojitokeza kumpokea mgombea urais wa ukawa kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo chadema huku wakidai kuwa mkusanyiko huo unaonesha ni kwa kiasi gani wananchi wanahitaji babadiliko.

Wakizungumza na suamedia bwana  Jackson Joel na Juma Mohamedi wamesema kuwa  mkusanyiko ambao umekuwa ukijitokeza kumpokea Mh. Edward Ngoyai Lowasa  unaonyesha ni kwa jinsi gani  wananchi walivyochoka kuahidiwa ahadi za uongo zisizotekelezwa kila mwaka  na chama chao hivyo kutafuta mabadiliko kutoka katika vyama vingine.

Kwa upande mwingine wakazi wengine wa manispaa wamesema kuwa uroho wa madaraka unachangia kwa kiasi kikubwa viongozi wa siasa kuhama chama kimoja na kuhamia chama kingine.

Wakizungumza na SUAMEDIA Bi Farida Ramadhani na Bi Mariam  Shabani wamesema kuwa  kuhama kwa viongozi hao kunasababishwa na uroho wa madaraka kutokana  na kukosa vyeo walivyokuwa wakivipigania katika vyama vyao vya awali hivyo kuamua kuhamia vyama vingine ili kujaribu kutafuta vyeo hivyo.

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner