SUA YAPONGEZWA KWA USHIRIKI WA UIFADHI WA MAZINGIRA NCHINI

 

    

SUA YAPONGEZWA KWA USHIRIKI WA UIFADHI WA MAZINGIRA NCHINI

 

Na:BUJAGA I KADAGO

Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo, SUA, kimepongezwa kwa ushiriki wake katika uhifadhi wa mazingira nchini ambapo kimewezesha kuanzishwa kwa jukwaa la mazingira wilayani kilosa mkoani Morogoro

Bofya kichwa cha habari kwa habari zaidi.......

 

 Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), kimepongezwa kwa ushiriki wake katika uhifadhi wa mazingira nchini ambapo kimewezesha kuanzishwa kwa jukwaa la mazingira wilayani kilosa mkoani morogoro.

 

 Pongezi hizo zimetolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Juma Khatib Chum wakati akizindua rasmi jukwaa la  mazingira la Wilaya ya Kilosa “ Jumaki” wakati mwenge wa uhuru ulipofika  katika kitongoji cha Ihombwe Tarafa ya Mikumi mkoani Morogoro ambapo amesema utaalamu wa uhifadhi uliopatikana kuhusu uhifadhi wa misitu ya asili kutoka sua unabidi uendelezwe kwa vitendo ili kuhifadhi mazingira ya nchi yetu.

 

 mradi huu wa uzalishaji na matumizi endelevu ya miti ya asili inayofaa katika kilimo mseto wilayani kilosa unaendeshwa na chuo kikuu cha sokoine cha kilimo sua kwa kushirikiana na wakala wa mbegu za miti tanzania ttsa na chuo kikuu cha sayansi za viumbehai umb cha norway kupitia programu ya epinav umelenga katika uhifadhi wa mazingira wilayani kilosa.

 

 kwa mujibu wa risala ya wadau katika hafla hiyo ya uzinduzi wa jukwaa la mazingira wilayani kilosa, kukamilika kwa mradi wa epinav kutapelekea wadau wote wanaohusika na uhifadhi mazingira ifikapo julai 2015 kujiunga na kuunda jukwaa la mazingira wilaya ya kilosa ili kuendeleza uhifadhi wa mazingira wilayani kilosa.

 

 akizindua jukwaa hilo la mazingira wilayani kilosa jumaki, kiongozi wa mbio za mwenge 2015 bw. Juma khatib chum alipongeza juhudi zilizofanywa na chuo kikuu cha sokoine cha kilimo sua katika kuwashirikisha wananchi wa kilosa kuhifadhi mazingira na kuwapongeza wanamazingira kilosa kwa kuitikia hilo kwani hatua katika kujiletea maendeleo.

 

 naye mwenyekiti wa jukwaa la mazingira kilosa mzee salehe kamwaya alimweleza kiongozi wa mbio za mwenge kuwa tayari kazi kubwa ya kuyarekebisha maeneo yaliyoathirika katika suala zima la uharibifu wa mazingira likiwa ni jukumu lao kuu.

 

 

 

 

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner