SUA YANG'ARA, MAONESHO YA SABABASA DAR -ES -SALAAM

 

  
                                                                                

SUA YANG'ARA, MAONESHO YA SABABASA DAR -ES -SALAAM

Banda la maonesho la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ktk uwanja wa maonesho wa kimataifa wa biashara jijini Dar es salaam limekuwa kivutio kwa wananchi hususani wakulima

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Banda la maonesho la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ktk uwanja wa maonesho wa kimataifa wa biashara jijini Dar es salaam limekuwa kivutio kwa wananchi hususani wakulima

 

 Hayo yamedhihirka kutokana idadi ya wananchi wanaotembelea banda la SUA kuuliza maswali mengi katika maeneo ya vipando, vyakula vilivyosindikwa sehemu ya udongo, misitu na mdahili wa wanachuo

 

 Aidha wananchi hao wamekuwa wakimalizia vipeperushi na majarida kuhusu aina mbambali za kilimo na ufugaji hususani kilimo cha miti matunda na bustani. Maswali yalielekezwa katika ufugaji nyuki , samaki na kuku wa asili

 

 Kuthibitisha hilo mtaalamu wa kitengo cha vipando Ndugu Hellena Mbije ameiambia SUAMEDIA kuwa katika siku mbili za maonesho tayari watu wanne wametoa oda ya kupatiwa miche mbalimbali ya matunda toka SUA

 

 Miongoni mwa wananchi waliotembelea banda la SUA katika uwanja wa sabasaba jijini Dar-Es-Salaam ni pamoja na mama huyu anyesema amekata kiu yake kuhusu kilimo cha miembe

 

 Aidha katika maonesho hayo walikuwepo wananchi walioridhika na kazi/elimu inayotolewa na SUA na hivyo wakatoa ushauri kwa uongozi wa SUA ili SUA iweze kutoa elimu yake jirani na watanzania wote

 

 Maonesho hayo ya kimataifa ya biashara yamefunguliwa ijumaa julai 3 na Rais Jakaya Kikwete na banda la SUA litakuwa wazi kwa elimu na kuhudhuria wananchi hadi mwisho wa maonesho hayo.

 

 

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner