WAKULIMA TUMIENI MBOLEA AINA YA MBOJI KUONGEZA TIJA KATIKA KILIMO

 

                                                                                          

WAKULIMA TUMIENI MBOLEA AINA YA MBOJI KUONGEZA TIJA KATIKA KILIMO

Wakulima nchini wametakiwa kutengeneza mbolea aina ya mboji, mbole itakayowaletea tija kubwa katika kilimo chao kwa kupata mazao bora na mengi hususani katika ardhi iliyochoka au yenye rutuba hafifu katika maeneo mengi nchini.

 

 NA: BUJAGA IZENGO KADAGO

 

Wakulima nchini wametakiwa kutengeneza mbolea aina ya mboji, mbole itakayowaletea tija kubwa katika kilimo chao kwa kupata mazao bora na mengi hususani katika ardhi iliyochoka au yenye rutuba hafifu katika maeneo mengi nchini.

 

hayo yameelezwa na mtaalamu wa maabara mkuu bw. ELIA KAMWELA kutoka chuo kikuu cha sokoine cha kilimo sua alipokuwa akizungumza na wakulima waliotembelea banda la SUA katika maonesho ya kimataifa ya bishara jijini Dar es salaam ambapo amesema mbolea aina ya mboji ni mbolea sahihi kwa kilimo hususani kwa wakulima wa kawaida nchini ambao hawana uwezo mkubwa wa kununua mbolea za viwandani.

 

 amesema hata hivyo ni muhimu utayarishaji wa kitaalamu uzingatiwe wakati wa kutayarisha mbolea ya mboji ili mboji hiyo iweze kuwa bora yenye virutubisho vyote muhimu kwa udongo na kuwezesha udongo kuipatia lishe bora mimea inayopandwa katika shamba 

 

 Bw. KAMWELA  amesema sehemu kubwa ya mboji inatakiwa kuwa majani ya mimea lakini majani hayo yanatakiwa kuwa ni yale yaliyo na kirutubisho cha nitrojeni na majani haya ni yale ya jamii ya mikunde kama vile majani ya kunde, maharage, choroko, soya na karanga na sio majani mengine kama yale wanayokula mifugo.

 

 

 

 aina nyingine ya kuchanganyia katika mbolea ya mboji ni pamoja na mbolea ya minjingu, urea, NPK na samadi ambayo inatakiwa iwekwe kwa kunyunyizia katika mchanganyiko wako wa mboji na mbolea ya minjingu inasaidia kupatikana kwa madini ya phosiphorous, zinc na copper katika mbolea yako ya mboji.

 

 mtaalamu huyo mkuu wa maabara kutoka sua bw. KAMWELA amesema kuwa mboji inatakiwa pia kuwekwa mabaki yatokanayo na utengenezaji wa sukari maarufu kama molasisi kwani molasisi inasaidia sana katika uharakishaji uozeshaji wa mboji yako lakini kwa upande wa pili ni chakula murua kwa wadudu katika mboji ambapo wasipopata molasisi wanashambulia nitrojeni katika mboji na wanaweza kuipotezea mboji yako wingi wa nitrojeni.

 

   amesema kiungo kingine katika utayarishaji wa mbolea ya mboji ni majivu ambapo mkulima anatakiwa kuyamwaga katika mchanganyiko wake wa mboji na faida ya majivu hayo ni kusaidia kurekebisha uwiano wa tindi kali kwenye mboji yako

 

 Bw. KAMWELA amesema katika utayarishaji wa mbolea hiyo ya mboji mkulima anatakiwa kuupanga mchanganyiko wake huo aina moja juu ya aina nyingne ya mchanganyiko na mwisho yaani pale juu mkulima anatakiwa kufunika na udongo. amesema kiwango cha maji utakayomwagia shimo lako la mbolea ya mboji kitategemea hali ya unyevu wa majani na michanganyiko yako. iwapo majani na michanganyiko yako ina unyevunyevu kiasi basi mwagia maji kiasi na kama ni makavu basi mwagia maji mengi cha msingi maji yasichuruzike yawe ni yale yatakayosaidia mchanganyiko wako kuoza.

 

 amesema mbole hii ya mboji ikishaiva basi inafaa kutumiwa katika bustani na katika mashamba ya mazao mbalimbali kwa ajili ya kujipatia mazao bora na mengi kwa gharama nafuu na hivyo kusaidia kaya kupambana na tatizo la umaskini kupitia kilimo bora chenye tija

 

 

 

 

 

 

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner