SUA YATATUA TATIZO LA UPANDAJI MALISHO YA MIFUGO KATIKA MAENEO YA MIJINI

SUA YATATUA TATIZO LA UPANDAJI MALISHO YA MIFUGO KATIKA MAENEO YA MIJINI

Na:BUJAGA IZENGO KADAGO

Wafugaji wanaoishi mijini sasa hawana sababu ya kuhofia kuendesha shughuli za ufugaji kutokana na nafasi finyu ya malisho baada ya chuo kikuu cha sokoine cha kulimo sua kukamilisha utafiti kuhusu malisho ya mifugo kwa kutumia reki.

Na:Bujaga Izengo Kadago

Utafiti huo umewezesha sasa kuzalisha nyasi kwa ajili ya mifugo mikubwa na midogo kwa kutumia reki ambapo unaweza kuzipanga kwenda juu kwa kadiri ya mahitaji yako ya nyasi katika eneo dogo tu nyuma ya nyumba yako.

Hayo yamebainishwa na  profesa a     aboud kutoka idara ya sayansi ya wanyama ya chuo kikuu cha sokoine cha kilimo sua wakati alipotambulisha utafiti huo kwa wananchi waliotembelea banda la sua katika uwanja wa maonesho ya wakulima nanenane mjini morogoro.

Kutokana na mafanikio ya utafiti huo sasa mfugaji anaweza kuzalisha  nyasi za kutosha kulisha ng’ombe wa maziwa, mbuzi, sungura, kuku na wanyama wengine walao nyasi kwa wafugaji ikiwa ni pamoja na wafugaji wa mijini ambao walikuwa na changamoto  ya kupata nyasi za malisho kwa ajili ya mifugo yao.

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner