ZIMAMOTO KUSUASUA MKOANI MOROGORO

   

ZIMAMOTO KUSUASUA MKOANI MOROGORO

 Na:HUSNA YAHYA

Wakazi wa manispaa morogoro wamelalamikia huduma ya zimamoto kwa  kuchelewa kufika katika eneo la tukio hali inayosababisha  kuteketea kwa  mali na bidhaa mbalimbali  za wahanga wa matukio ya moto.

Bofya kichwa cha habari kwa habari zaidi.......

 

 Hali hiyo imejitokeza hivi karibuni katika mtaaa wa tumbaku manispaa ya morogoro baada ya nyumba moja kuungua  moto na kuteketeza mali zilizokuwapo ndani ya nyuma hiyo kutokana  na magari ya  zimamoto kuchelewa kufika  ingawa walipewa taarifa mapema.

 Akizungumza na sua media  bi khadija sadiki  ambaye n imkazi  wa eneo hilo la tumbaku amesema kuwa taarifa ilitolewa mapema kwa zimamoto lakini walichelewa kufika na hata walivyofika hawakuwa na maji ya kutosha hali iliyosababisha moto kuendelea kuteketeza mali zilizokuwamo ndani.

Mmoja  wa wafanyakazi wa shirika hilo la zima moto  ambaye haikuwezekana kupata  jina lake mara moja, baada ya kubanwa na wananchi kwa kuulizwa kwa nini hali hiyo imejitokeza,aliomba radhi na kusema kuwa hali hiyo inasababishwa na ubovu wa magari yao ya kuzimia moto.

Suamedia ilifika katika ofisi za zimamoto manispaa ya morogoro  kwa dhumuni la kupata maelezo zaidi kuhusu tatizo hilo lakini ilishindwa kupata maelezo ya kina baada ya kuzuiliwa na afisa mmoja wa kikosi hicho akidai kupatiwa kitambulisho kwanza ndipo amruhusu mwandishi kuonana na bossi wa zimamoto.

Hata hivyo juhudi za suamedia zinaendelea ili kupata msimamo wa kikosi hicho cha zimamoto manispaa ya morogoro ili kujibu tuhuma zilizotolewa na wananchi hao.

 

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner