MAAFISA AFYA KATA ZOTE KUKAGUA USAFI MANISPAA YA MOROGORO

   

MAAFISA AFYA KATA ZOTE KUKAGUA USAFI MANISPAA YA MOROGORO

Na:TATYANA CELESTINE

Kufuatia hali ya usafi katika  Manispaa ya Morogoro kuwa katika hali isiyo njema, Maafisa Afya kutoka kila Kata wamelazimika kukagua kila eneo kuhakikisha yanafanyiwa usafi hasa katika wiki  hii ya usafi wa mazingira hali ambayo  imeibua baadhi ya maeneo kuonekana kuwa nyuma katika kutekelezaji wa amri za Manispaa

Bofya kichwa cha habari kwa habari zaidi.......

 

 

 Kufuatia hali ya usafi katika  Manispaa ya Morogoro kuwa katika hali isiyo njema, Maafisa Afya kutoka kila Kata wamelazimika kukagua kila eneo kuhakikisha yanafanyiwa usafi hasa katika wiki  hii ya usafi wa mazingira hali ambayo  imeibua baadhi ya maeneo kuonekana kuwa nyuma katika kutekelezaji wa amri za Manispaa

Akiongea na SUAMEDIA Mjumbe wa Mtaa wa Reli Kata ya Kingo Manispaa ya Morogoro Alau Faya alipotakiwa kueleza ni kwa kiasi gani usafi katika eneo lake umefanikiwa, amesema hii imekuwa ni changamoto kwao kwani ingawa yeye ni mjumbe wa nyumba kumi lakini pia ni mjumbe katika kamati iliyoteuliwa ili kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kikamilifu lakini kadiri siku zinavyokwenda anaona watu hawatilii mkazo suala la usafi katika mazingira yao

Aidha ameongeza kuwa  wakazi wanatakiwa kufahamu wasiposhiriki katika usafi lazima hukumu itawafikia bila huruma “hakika zoezi hilo lazima lifanyike kikamilifu hasa katika kipindi hiki cha wiki ya usafi wa mazingira endapo hali itakuwa hivi mpaka afisa afya akipita lazima tutatozwa faini hakuna huruma katika hilo”alisema bi faya

Vilevile amewaomba wananchi kutambua usafi ni jukumu la wote hivyo haina haja ya kungoja mpaka afisa afya aje kuwakagua ndio waanze kufanya usafi katika mazingira yao akisisitiza zile kamati zilizoteuliwa kushughulikia mazingira kuhakikisha zinafanyakazi bila kungoja siku au wiki ya mazingira.

Katika hatua nyingine  mkazi wa Boma Road Manispaa ya Morogoro Mustaq Miyanji ameisifu Manispaa kwa kutenga watu kwa ajili ya kufanya usafi katika maeneo ya mijini hivyo amewashauri kuongeza watu waweze kufikia maeneo ya ndani kufanya usafi hii itasaidia kuweka mji kuwa safi.

“Sisi watu tunaoishi mjini tunaratiba ya kuchangia shilingi elfu tatu kila mwezi kwa ajili ya watu wanaokuja kutufanyia usafi  naona sasa umefika wakati wa manispaa kuzidi kutoa ajira hiyo kwa watu wengi zaidi ili waingie katika maeneo ya ndani kama kilakala, bigwa, kigurunyembe na kichangani kwa gharama ileile naamini mazingira yote yatakuwa safi huenda morogoro nayo itakuwa mfano”alisema miyanji

Katika hatua nyingine mkazi wa Kihonda Sekondari Manispaa ya Morogoro Immanuel Lukindo ameshauri taarifa hizi ambazo zinamlenga mtu mmoja mmoja katika jamii, manispaa ihakikishe inatumia njia ya vyombo vya habari ili taarifa hizo ziweze kumfikia kila mmoja kwa wakati maana wengine taarifa hizo hawapati hasa wale wafanyakazi ambao hawashindi nyumbani 

Zoezi hilo la usafi wa mazingira likibeba kauli mbiu ya “Tunza Mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi Tanzania” Mkoa wa Morogoro ukishirikiana na mikoa mingine ya Tanzania kwa pamoja wameungana kutokomeza uchafu katika miji na kwa lengo la kuifanya tanzania kuwa safi.

 

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner