WANAFUNZI WANAOSOMEA MISITU WANUFAIKA OLMOTONYI

     

WANAFUNZI WANAOSOMEA MISITU WANUFAIKA OLMOTONYI

Na:GERALD LWOMILE

Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo kimesema kuwa wanafunzi wengi wanaosoma fani ya misitu nchini kwa kiasi kikubwa wamenufaika na Kituo cha Mafunzo ya Misitu Olmotonyi kilicho chini ya chuo kikuu hicho.

Akizungumza na SUAMEDIA Meneja wa Kituo hicho cha Misitu Olmotonyi Bw. Modest Mrecha amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa shamba hilo watafiti wengi katika Sekta ya Misitu nchini wamepita shambani hapo na kufanya tafiti mbalimbali.

Bofya kichwa cha habari kwa habari zaidi.......

 

 

Ameongeza kuwa shamba hilo la miti ambalo linamilikiwa na Chuo hicho limekuwa likitoa mafunzo kwa vitendo kwa wanasayansi hao wa Sekta ya Misitu jambo ambalo mbali na kuwasaidia wanafunzi lakini pia linaleta faida kubwa kwa taifa.

Akizungumzia kituo hicho kinavyonufaisha taifa amesema kuwa wanafunzi wanaomaliza masomo yao na kupata mafunzo ya vitendo katika kituo hicho huchua elimu hiyo na kuipeleka sehemu mbalimbali jambo ambalo linawasaidia wananchi kujua kwa undani kuhusu sekta ya misitu.

Aidha ameongeza kuwa mbali na kutoa elimu kwa vitendo tafiti mbalimbali zimefanyika na zimekuwa zikilinufaisha taifa kwa ujumla.

Kituo cha mafunzo cha Olmotonyi kilicho chini ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo ambacho kina hekta mia nane na arobaini za misitu na kimekuwa kikizalisha mazao yatokanayo na misitu ambapo mapato yake husaidia kuendesha kituo hicho.

Katika hatua nyingine Bw. Mrecha amesema kuwa kituo hicho cha mafunzo kimekuwa kikipata ufadhili kutoka shirika la misaada la Norway NORAD.

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner