BURUDANI

 

VIJANA WATAKIWA KULINDA AMANI

Na:Ayoub Mwigune

Muandaji wa tamasha lililowakutanisha waimbaji wa nyimbo za injili nchini Tanzania John Jackson ambaye ni balozi wa vijana katika kanisa la FPCT  amewasihi vijana kuhakikisha wanadumisha na kulinda amani ya nchi  pamoja na kumtumikia mungu ,ili waweze kufanikiwa duniani na mbinguni .

Hayo ameyazungumza katika tamasha la muziki wa injili lililofahamika kama The Big PRAISE CONCERT ambalo lilifanyika katika kanisa la FPCT kurasini jijini  Dar es laam na kuelezea kuwa lengo lake la kuandaa tamasha hilo ni kuwakutanisha waimbaji wa nyimbo za injili pamoja wadau wote wanaohusika katika muziki huo.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

   

 

 

 

MIKAKATI YAPANGWA KUKUZA MUZIKI WA MOROGORO

Na:Alfred Lukonge

Mipango na mikakati inaendelea kupangwa kwa wadau wa burudani kwenye vyombo vya habari, watayarishaji wa muziki pamoja na wasanii wa muziki wa kizazi kipya mkoani Morogoro kuangalia ni jinsi gani wanaweza kukuza muziki huo mkoani hapo.

 

Akizungumza na SUAMEDIA mwenyekiti wa mpango huo Abel Kidunda amesema kuwa lengo la kuanzisha umoja huo ni kuondoa matabaka kwa wadau wote wanaohusika na muziki wa kizazi kipya mkoani Morogoro.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........


 

   

 

Picha na mtandao  

BARNABA KUTOA ALBAMU MPYA MWEZI WA TANO

Na:Adam Ramadhan

Muimbaji  na  mtayarishaji  wa  muziki  wa Bongo fleva  nchini Tanzania Elias Barnabas  alimaarufu  kama Barnaba Classic  amesema  kuwa  albamu  yake  mpya itatoka kabla  ya mwezi  wa  tano  huku  akiorodhesha baadhi ya wasanii watakaokuwepo  katika nyimbo  zinazopatikana katika albamu hiyo.

Akizungumza  kwa  njia ya  simu katika kipindi  cha njendani kinachorushwa  na  Suafm, muimbaji  huyo  amesema albamu  yake itaitwa nanenane huku akiwa ameshirikisha wasanii kadhaa kama Maua Sama, Juma Musa alimaarufu kama Jux, Sunday  Mjeda alimaarufu  kama Linex  na wengineo.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

   

 

 

KWAYA YA SHEKINA GLORY YAZINDUA ALBAMU “ NANI KAMA MUNGU”

Na: Allen Sparta

Kwaya ya Shekina Glory imefanya uzinduzi wa albamu yao ya kwanza  katika kanisa la  Canaan Christian Worship Center, albamu hiyo inayoitwa “Nani kama  Mungu” imezinduliwa rasmi na Askofu mkuu wa kanisa hilo Zephania Ryoba.

Akizungumza na SUAMEDIA  Mshauri  Mkuu wa kwaya hiyo Dr. Tundui amesema kwaya hiyo ilianzishwa mwaka 2012 na ilikua ikitoa huduma katika makanisa mbalimbali na wamefanikiwa kurekodi nyimbo zaidi ya ishirini na sasa wameweza kutoa albamu yao ya kwanza.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........


 

 

   

 

 

CHANZO CHA MUZIKI WA MOROGORO KUFELI CHABAINIKA

Na: Alfred Lukonge

Ubinafsi, dharau na kutokukubali kujifunza kutoka kwa wengine miongoni mwa watayarishaji wa muziki mkoani Morogoro imebainika kuwa  ndio sababu kubwa inayosababisha  muziki wa mkoa huo kutokusonga mbele ingawa kuna vipaji vingi.

 

Akizingumza na SUAMEDIA mtayarishaji wa muziki kutoka studio ya Uptown Records Japhet Kutona maarufu kama King Niver amesema kuwa ili muziki wa Morogoro uweze kusonga mbele ni lazima mawazo ya mtu mmoja yachanganyike na  mwingine ili kiweze kutoka kitu kizuri, hivyo ushirikiano miongoni maprodyuza ni muhimu kama kweli wana nia ya dhati ya kuendeleza muziki wa mkoa huo.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

     
                                       

KWAYA YA UINJILISTI KKKT MABIBO FARASI YAPANIA KUFANYA MAKUBWA


Na: Alfred Lukonge

Dar es Salaam

Mwenyekiti wa  kwaya ya uinjilisti KKKT Usharika wa Mabibo Farasi jijini Dar es Salaam Mwl. Sayuni Moses  amesema kuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo ya kwaya nyingi ni uhaba wa kinababa walioamua kujitolea kwa dhati katika kumwimbia Mungu.

Mwl. Sayuni amesema hayo alipozungumza na SUAMEDIA hivi karibuni na kubainisha kuwa “ changamoto  kubwa tunayokutana nayo kwenye kuiendeleza huduma hii ni upungufu wa akinababa wanaotakiwa kuimba sauti ya tatu na nne jambo linalopelekea ladha za sauti hizo kukosekana katika kwaya yetu”.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

     
                                                        

ILI KUSHINDA MAJARIBU WANADAMU AWANA BUDI KUMTAFUTA MUNGU KWA JUHUDI ZOTE

 


Na: ALFRED LUKONGE


Imeelezwa kuwa wanadamu awana budi kumtafuta Mungu kwa juhudi zote ili waweze kuyashinda majaribu yote ya dunia kama kweli wanataka kuuona ufalme wa mbingu.

Hayo yamesemwa na mwanamuziki wa nyimbo za injili Japhet Makoye anayesomea masuala ya kilimo chuoni SUA alipozungumza na SUAMEDIA na kubainisha kuwa “ nimeamua kuimba nyimbo za injili ili nipate kufanya mahubiri kwa njia ya uimbaji nikiwa na  nia ya kuwakomboa wanadamu”.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

 

     
                                                      

WASANII WATAKIWA KUACHA KUAMINI KUWA  KAZI NZURI LAZIMA IFANYIKE STUDIO FULANI

Na: ALFRED LUKONGE

Wasanii chipukizi katika mji wa Morogoro wametakiwa kuacha kasumba mbaya iliyojengeka miongoni mwao ya kuamini kuwa ili utoe kazi nzuri ni lazima uende kwenye studio fulani kwani kazi nzuri inaweza kutoka sehemu yoyote.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

     
                                                    

KAMA UNATAKA KUENDELEZA KIPAJI USIOGOPE KUJARIBU- FASHION

Na: ALFRED LUKONGE

Imeelezwa kuwa kama msanii ana kipaji hata siku moja asiogope kujaribu pamoja na kutokata tamaa kama kweli anataka kuendeleza kipaji chake

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

 

     
 

WASANII WATUMIE SANAA YAO KUIMARISHA AMANI TANZANIA

Na: ALFRED LUKONGE

Wito umetolewa kwa wasanii wachanga katika fani ya kuigiza kuwasilisha fikra zao za jinsi watanzania wanavyoweza kuishi kwa amani pasipo kujali itikadi ya vyama vyao ili kutunza amani ya nchi.

Bofya hapa kwa Habari zaidi.......

   

 

   

CELINE DION APATA MSIBA MZITO

Na: ALFRED LUKONGE

Mume wa mwanamuzuki nguli wa pop duniani Celin Dion, Bw. Rene Angelil amefariki dunia hii leo akiwa na umri wa miaka 73.

 

Bofya hapa kwa Habari zaidi.......

 

   

 

 

 

MASHABIKI WAPENDE VYA NYUMBANI KWANZA

 Na: ALFRED LUKONGE

Wapenzi wa muziki wa dansi katika mji wa Morogoro wameshauriwa kuacha kasumba ya kujitokeza kwa wingi siku zinapokuja bendi kutoka Dar es Salaam kwani kwa kufanya hivyo ni kudidimiza maendeleo ya muziki wa dansi katika mji huo.

Bofya hapa kwa Habari zaidi.......

     
 

 

 

TAHOSA KUWAKARIBISHA MWAKA WA KWANZA

Na: ALFRED LUKONGE

Shirikisho la wanafunzi wanaosoma elimu ya kilimo cha bustani Tanzania (TAHOSA) Jumamosi ya tarehe 12/12/2015 waliandaa tamasha la michezo kuwakaribisha  wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliojiunga na shahada ya elimu hiyo katika chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) mkoani Morogoro.

Bofya hapa kwa Habari zaidi.......

   

 

 

   

 

 

WANAMUZIKI WASHAURIWA KUPIGA MUZIKI WA MOJA KWA MOJA

Na: ALFRED LUKONGE

Japhet Lulaka Nguli wa kupiga magitaa ya aina zote mkoani Morogoro amesema wanamuziki  wa Tanzania wametakiwa kupiga muziki wa live  ili kukuza vipaji vyao ili waweze kupenya kwenye soko la kimataifa.

Bofya hapa kwa Habari zaidi.......

   

 

 

 

WANAMUZIKI CHIPUKIZI KUNA MENGI YA KUFANYA ILI KUFIKIA SOKO LA MUZIKI DUNIANI

Na: ALFRED LUKONGE

Mwanamuziki chipukizi katika muziki wa kizazi kipya anayesoma mwaka wa tatu Shahada ya Sanaa ya Maendeleo vijijini katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) mkoani Morogoro Ally Said maarufu kama C dady amesema wasanii wengi wa Tanzania wana vitu vingi vya kufanya ili waweze kupenya kwenye soko la muziki duniani.

Bofya hapa kwa Habari zaidi.......

   

 

 

    

MIMBA YAMFANYA KIM KARDASHIAN KUUKACHA UWANAMITINDO

Na: TATYANA CELESTINE

Mwanamama mwenye umri wa miaka 35 Kim Kardashian, ambaye anajishughulisha sana na mitindo ambaye kwa sasa amebakisha mwezi mmoja kuweza kupata mtoto wa pili amesema ameamua kuacha kwa muda mambo ya fasheni kutokana na mabadiliko ya mwili wake

Bofya hapa kwa Habari zaidi.......

 

 

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner