SPOTI

 

 

TAZAMA HAPA MSIMAMO WA LIGI KUU VODACOM BARA MZUNGUKO WA KWANZA 2017-18

                        Bofya hapa kwa Habari zaidi.....

picha na mtandao

 

 

MALINZI NA WENZAKE KULA MWAKA MPYA MAHABUSU

Na: Tatyana Celestine

Kesi  ya  kutakatisha Dola za Marekani 375,418 inayomkabili aliyekuwa Rais wa shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na wenzake, imepigwa kalenda hadi Januari 11, 2018 baada ya upande wa Jamhuri kudai bado haujakamilika.

Hata hivyo, upande wa utetezi uliiomba  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,  Dar es Salaam, kuuamuru upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi wa kesi hiyo.

Bofya hapa kwa Habari zaidi.....

   

 

Tokeo la picha la mbaraka yusuph azam player

Picha na mtandao.

 

MBARAKA YUSUPH MCHEZAJI BORA WA MWEZI SEPTEMBA VPL

Na:Ayoub Mwigune

 

Mchezaji wa Azam FC Mbaraka Yusuph ndiye Mchezaji Bora wa   mwezi  Septemba mwaka huu kwa upande wa klabu hiyo.

 


Yusuph ametwaa tuzo hiyo baada ya kupigiwa kura nyingi na mashabiki wengi wa soka na kuwazidi wapinzani wake  aliokuwa akishindanishwa nao, kipa Razak Abalora na kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

   

 

Tokeo la picha la simba  vs ryon

Picha na mtandao

 

MAYANJA AKIRI SAFU YA USHAMBULIAJI YA SIMBA NI BUTU 

Na Rajabu Kimaro

Kocha msaidizi wa clabu ya Simba ya Dar es salaam Jackson Mayanja amesema kuwa klabu yake bado inakabiliwa na tatizo la umaliziaji katika safu ya ushambuliaji.

 

Kauli hiyo ya mayanja imekuja baada ya timu yake kulazimishwa sare ya kutofungana dhidi ya timu ya Mlandege ya zanzibar katika mchezo wa kirafiki ikiwa ni mwendelezo wa michezo yake ya kujiandaa na ligi kuu Bara pamoja na mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya mahasimu wao wakubwa timu ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa tarehe 23 mwezi huu.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........


 

     

Image result for taifa stars logo

Picha na mtandao.

 

STARS YAONDOKA LEO KWENDA KUIVAA AMAVUBI

Na:Ayoub Mwigune 

Timu ya taifa ya Tanzania inatarajia kuondoka leo kuelekea nchini Rwanda kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Rwanda, mchezo ambao unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi wa soka nchini ili kuona hatima ya timu hiyo ya Taifa star.

Kikosi hicho cha timu ya taifa ya Tanzania kitasafiri kwa usafiri wa ndege  ya AIR TANZANIA na kupitia jijini dar es salaam, kikitokea jijini mwanza ambako kiliweka kambi .

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

     

Image result for VODACOM PREMIER LEAGUE LOGO

Picha na mtandao

 

VPL RASMI MWEZI UJAO

Na:Ayoub Mwigune 

Ligi kuu ya vodacom Tanzania bara inatajia kuanza kutimua vumbi mwezi wa nane katika msimu mpya 2017/2018.

 

Kufuatia kukaribia kwa ligi hiyo timu ya singida united ambayo imepanda daraja msimu huu imezidi kujiimarisha baada ya hapo jana kufanikiwa kusajili nyota wawili wakimataifa.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

   

 

Image result for Mayanga

Picha na mtandao.

 

MAYANGA ATANGAZA KIKOSI STARS 

Na:Alfred Lukonge

Kikosi cha timu ya mpira wa miguu cha Tanzania 'Taifa Stars', kimesafiri kwenda jijini Mwanza kikiwa na ongezeko la wachezaji wapya saba.

 

Kati ya hao ambao Kocha Mkuu Salum Mayanga amewaita, wamo wale aliowatangaza juma lililopita ambao ni John Bocco, Kevin Sabato pamoja na kinda Athanas Mdamu ambaye anacheza Alliance ya Mwanza inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

   

 

Picha na mtandao  

TERRY ATUA BIRMINGHAM

Na:Ayoub Mwigune 

Klabu ya Birmingham City imempatia ofa ya mkataba mpya nahodha wa zamani wa timu ya Chelsea John Terry kuitumikia klabu hiyo amethibitisha   meneja Harry Redknapp. John terry  aliachana na  mabingwa hao wa Ligi ya Premia mwisho wa msimu uliopita baada ya kucheza  mechi 717 na kushinda mataji  13 katika  miaka 22.

 

Terry ni mchezaji wa tatu katika kikosi cha Chelsea, nyuma ya Ron Harris na Peter Bonetti kuchezea klabu hiyo mechi nyingi na ameshikilia rekodi za klabu hiyo kwa kuwa nahodha.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........


 

   

 

Picha na mtandao

 

 

 

 

 

AKILIMALI KUWANIA UENYEKITI YANGA

Na: Adam Ramadhan

Katibu  mkuu   wa  baraza  la   wazee  katika  klabu  ya   Yanga  Ibrahimu   Akilimali  ametangaza  kuwania   nafasi  uenyekiti  iliyoachwa   wazi   siku  za  hivi  karibuni   na   aliyekuwa   Mwenyekiti   wa   klabu   hiyo  Yusuph   Manji.

Mzee  Akilimali   amesema   kuwa   amefikia  uamuzi    huo  ili  aweze  kuleta  mabadiliko  makubwa   zaidi  akitumia  busara  zake  licha  ya  kwamba   yeye   hana utajiri wa ki billionea   kama   alivyokuwa  Yusuph   Manji   kwa  wanajangwani   hao.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

   

 

Picha na mtandao  

IRAN YAFUZU KOMBE LA DUNIA

Na:Ayoub Mwigune 

Iran imekuwa nchi ya pili kufuzu katika michuano ya Kombe la Dunia ya 2018 baada ya kuitandika timu ya taifa ya Uzbekistan 2-0 mjini Tehran.

Ushindi wao umewawezesha kufungua mwanya wa alama nane kati yao na wapinzani wao, ambao wapo   katika nafasi ya tatu kwenye orondha ya msimamo. 

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

 

 

   

 

Picha na mtandao  

MOHAMED HUSSEIN MCHEZAJI BORA VPL

Na:Ayoub Mwigune 

Na:Ayoub Mwigune

Mchezaji wa timu ya Simba SC, Mohamed Hussein amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Mei kwa msimu wa 2016/2017,Hussein aliwashinda wachezaji Haruna Niyonzima wa Yanga na Shabani Idd wa Azam FC. 

 

Katika mwezi Mei kulikuwa na raundi tatu ambazo Hussein alicheza kwa dakika zote 270 na kutoa mchango mkubwa katika kuisadia timu yake kubaki katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom.Pia alionesha nidhamu ya hali ya juu, hivyo kutopewa onyo la aina yoyote.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

   

 

Picha na mtandao.  

 

 

SIMBA YAINGIA KAMBINI KUIWINDA MWADUI

Na:Ayoub Mwigune 

KIkosi cha Simba kimeendelea na mazoezi yake kambini Dege Beach ikiwa ni kujiandaa na mechi yake ya mwisho ya ligi dhidi ya Mwadui ya Shinyanga   mchezo utakaofanyika katika uwanja wa taifa .

 

Baada ya mechi dhidi ya  Stand United na kuondoka  na ushindi wa mabao 2-1. wachezaji wa klabu ya SIMBA  walipewa mapumziko ya siku mbili na baada ya hapo, Jumatatu kazi ikaanza.

 

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........


 

   

 

Picha na mtandao  

KLABU ZATAKIWA KUPELEKA MAONI TFF

 

Na:Ayoub Mwigune

Na:Ayubu Mwigune

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limezitangazia klabu zote zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2017/18 na zile za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2017/18 kwamba kipindi hiki ni cha kuwasilisha maoni na mapendekezo mbalimbali kuhusu marekebisho ya kanuni za ligi husika.

TFF imeziagiza klabu zote – kwa nafasi walizonazo kama wanafamilia ya mpira wa miguu, kuwasilisha mapendekezo na maoni kuhusu marekebisho ya katiba kwa njia ya kuyatuma kupitia anwani za sanduku la Barua 1574, Dar es Salaam au yapelekwe  moja kwa moja  katika ofisi za Bodi ya Ligi au TFF.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

   

 

 

SIMBA TAYARI KUIKABILI MBAO

Na:Ayoub Mwigune 

Timu ya Simba  imewasili Mkoani Geita  ikitokea Kagera  kwaajili ya kuweka kambi ya siku nne kujiandaa na mchezo Dhidi ya Mbao Fc na Toto African  zote za Jijini Mwanza Mchezo ambayo itapigwa kwenye Dimba la CCM Kirumba.

Ikiwa Mkoani Geita Simba inatarajia kucheza mchezo wa Kirafiki na timu ya Geita Gold Sport Siku ya Jumatano mechi ambayo itachezwa kwenye  uwanja wa shule ya msingi  Waja.

 

Kwa Mujibu  wa Nahodha wa Kikosi cha Simba Jonas Mkude amewataka mashabiki kuendelea kuishabikia timu hiyo na kwamba watahakikisha wanafanya vizuri kwenye michezo  yao ambayo imebakia.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........


 

 

   

 

Picha na mtandao  

 

LIGI DARAJA LA NNE MKOANI MOROGORO YASHIKA KASI

Na:Ayoub Mwigune 

 

Ligi daraja la nne manispaa ya morogoro iliendelea tena hapo jana ambapo klabu ya mkundi united ilikuwa ikipambana dhidi ya  compassion mabapo  dakika 90 ziliweza kukamilika kwa sare ya 1-1 ambapo goli kwa upande wa mkundi lilifungwa na MARTIN ALOYCE  wakati kwa upande wa compassion goli lilikuwa la kujifunga kutokana na uzembe wa beki.

 

 

Ligi hiyo inatarajia kuendelea leo ambapo klabu SULTAN RANGERS itakuwa ikivaana na klabu ya MORO CITY huku zote zikiwa na alama saba katika kundi lao hivyo kufanya mchezo kuwa mgumu zaidi katika uwanja wa sabasaba katika manispaa ya morogoro.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

   

 

 Picha na mtando

 

 

AZAM YAELEKEZA NGUVU ZAIDI KWENYE MICHUANO YA LIGI KUU NA KOMBE LA FA

Na:Ayoub Mwigune 

 

Kocha Mkuu wa  klabu ya Azam FC, Aristica Cioaba,  ameweka wazi kuwa wameshasahau yaliyopita na nguvu zao kwa sasa wanazielekeza katika michuano ya Ligi Kuu na Kombe la FA, ili kuhakikisha wanapata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani.

Kocha huyo wa azam fc amesema kupitia  tovuti ya klabu hiyo kuwa asingependa kuzungumzia juu ya vurugu walizofanyiwa katika mchezo huo lakini ameelezea mchezo huo baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza huku akisema  timu yake ilionekana kutengeneza nafasi nyingi lakini ilishindwa kuzitumia kutokana na safu ya ushambuliaji  wake kutokuwa makini.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

     
        Picha na mtandao.  

STARS KUMKOSA ULIMWENGU

Na:Ayoub Mwigune 

Wakati kikosi cha timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, kikitarajiwa kuingia kambini leo Machi 19, 2017 kwenye Hoteli ya Urban Rose, Dar es Salaam, kikosi hicho cha Kocha Salum Mayanga, kitamkosa Thomas Ulimwengu kutoka na majeruhi.

 

Taarifa ambazo Mayanga amezipata kutoka Sweden ni kwamba Ulimwengu kwa sasa yuko chini ya uangalizi wa madaktari.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........


 

 

   

 

 

Picha na mtandao.

 

 

KLABU NANE ZATINGA ROBO FAINALI LIGI YA EUROPA

 

Na: Adam Ramadhan

Klabu  nane  kutoka  ligi  mbalimbali  zimefanikiwa  kutinga  katika  hatua  ya  robo  fainali  ya  michuano  ya EUFA EUROPA  ligi  baada  ya  hapo jana michezo kufanyika kukamilisha  mkondo  wa  pili  wa mechi hizo.

Katika orodha hii timu  mbili  kutoka  ligi  ya Ubelgiji zimefanikiwa kusonga mbele ikiwa ndio ligi pekee iliyotoa timu nyingi katika hatua hii, timu  ambazo  zimesonga mbele ni  pamoja na  KRC Genk, Anderletch, Manchester United, Ajax, Lyon, Shalke 04, Besiktas, na Celta Vigo.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

   

 

 

Picha na mtandao.

 

ATLETICO MADRID YATINGA ROBO FAINALI UEFA

Na:Ayoub Mwigune 

Klabu  ya Atletico Madrid imekuwa timu ya tatu ya Hispania kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuibuka na ushindi wa jumla wa mabao 4-2 dhidi ya Leverkusen ya UjerumaniAtletico waliingia pambano la marudiano katika uwanja wao wa nyumbani wakitambia ushindi wa ugenini wa mabao 4-2 walioupata wiki mbili zilizopita.

 

Klabu ya Bayern Leverkusen walianza pambano vizuri na kukaribia kupata goli baada ya dakika tano za nwanzo kufuatia Kampl kumchezesha  vizuri Kevin Volland aliyeipaisha shuti lake juu kidogo ya goli ,Atletco walijibu mashambulizi  dakika ya 15 lakini pia wao walikosa kufuatia Angel Correa kupanguliwa shuti lake na Bernd Leno.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........


 

 

   

 

Picha na mtandao

 

NGOLO KANTE APELEKA MSIBA MAN U

Na:Ayoub Mwigune 

Klabu ya Manchester united imekubali kichapo cha 1-0  kutoka kwa vinara wa ligi ya uingereza ,bao pekee la ushindi kwa Chelsea lilifungwa na Ngolo Kante kwa mkwaju mkali katika dakika ya 51. Manchester United walicheza kwa kipindi kirefu wakiwa  na upungufu wa mchezaji mmoja baada ya Ander Herera kuoneshwa kadi mbili za njano katika dakika ya 35

 

Mchezo ulibadilika baada ya Ander Herera kutolewa kwa kumchezea rafu Eden Hazard. Kipa wa United, David De Gea awali aliokoa mkwaju mkali wa Hazard.Kikosi cha Antonio Konte kilitumia mwanya wa kutolewa kwa Herera katika kipindi cha pili na Kante kufunga bao zuri kwa shuti la mbali.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

   

 

Picha na mtandao

 

MAYANGA ATANGAZA KIKOSI CHA WACHEZAJI 26 WA TAIFA STARS

Na:Ayoub Mwigune 

Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza kikosi chake cha wachezaji 26 kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki.

Stars inaweza kucheza na kati ya Zambia na Rwanda au timu nyingine kwa kuwa kumekuwa na taarifa tofauti.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

   

 

 Picha na mtandao

 

 

MBWANA SAMATA ANG’AA GENK IKIIBUKA NA USHINDI WA GOLI 5-2

Na: Adam Ramadhan

Mbwana Samata ameemdelea kufanya vizuri katika timu yake ya KRC Genk ambapo katika mchezo wao  wa kwanza wa Europa League hatua ya 16 bora dhidi ya KAA Gent ameendelea kuweka historia katika timu hiyo baada ya  kujiandikia mabao mawili katika ushindi wa mabao 5-2.

KAA Gent ambao watalazimika kuifuata KRC Genk katika mchezo wa marudiano March 16, 2017.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

   

 

Picha na mtandao.

 

BAYERN YAIFUMUA ARSENAL GOLI 5-1

Na:Ayoub Mwigune 

Arsenal wamezidi kuendelea na machungu kwenye mioyo ya mashabiki wao baada ya kukubali kipigo kingine cha mabao 5-1 na kuondolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Arsenal wameondolewa na Bayern Munich ambayo iliwafunga  Arsenal kwa idadi hiyo ya 5-1 mjini Munich. Leo imerudia ikiwa ugenini London.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........


  

     
  Picha na mtandao  

VPL KUENDELEA TENA HAPO KESHO

Na:Ayoub Mwigune 

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), inatarajiwa kuendelea    siku ya Jumatano ambapo, Young Africans itaalikwa na Ruvu Shooting kwenye mchezo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

Pamoja na   mchezo huo mmoja kwa siku ya Jumatano, ligi hiyo ambayo ni michuano mikubwa nchini, itaendelea mwishoni mwa wiki hii ambako kwa siku ya Jumamosi Machi 4, mwaka huu Simba itacheza na Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........


 

 

     

 

 

 

Picha na mtandao.

 

MAN U YATWAA UBINGWA WA EFL

 

Na: Adam Ramadhan

Klabu  ya  Manchester  United  imefanikiwa  kutwaa  kombe la  ligi  la ndani yaani  EFL baada  ya  hapo  jana kuweza  kuinyuka  klabu  ya  Southamtoni huku  Zlatan  Ibrahimovic  akiwa  shujaa  wa mtanange  huo.

Mchezo  huo  uliofanyika  katika  uwanja  wa Wembley  na  kushuhudiwa   na mashabiki zaidi ya  85 elfu timu  hiyo  ikiwacharaza  Southamptoni  Jumla ya  magoli 3-2 ,magoli  yakifungwa  na Zlatan Ibrahimovic  dakika  ya  19  na 87 huku Jese  Lingard  akifunga  dakika  ya 38.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

 

     

Picha na mtandao

 

 

AZAM YATOA HALI YA MAJERUI WAKE

Na:Ayoub Mwigune 

Benchi la ufundi la klabu ya Azam fc limeelezea hali  ya maendeleo ya  wachezaji wake wawili ambao walikuwa majeruhi kutokana na kuchanika misuli ya nyama za paja kuwa tayari wote wawili tayari wameshaanza mazoezi mepesi hali inayoonesha kwamba wanaendelea vyema .

 

Akizungumza na tovuti ya klabu hiyo Daktari wa timu hiyo MWANANDI MWANKEMWA amesema licha ya kuanza mazoezi hayo lakini nahodha wa timu hiyo JOHN  BOCO yeye atakuwa chini ya uangalizi na huenda wiki mbili zijazo akawa yupo fiti na kurejea uwanjani.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........


 

     

Picha na mtandao

 

LIVERPOOL KUIKARIBISHA LEEDS KOMBE LA LIGI HII LEO

Na:Ayoub Mwigune 

Klabu ya Liverpool ipo nyumbani hii leo kucheza dhidi ya Leeds katika michuano ya ligi ya shirikisho la soka Uingereza na tayari meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amethibitisha kwamba mchezaji wake toka Brazil Philipe Coutinho ataikosa mechi hiyo kutokana na kuwa majeruhi.

 

Meneja huyo amesema kwamba coutinho anatarajiwa kurejea  uwanjani mwezi januari 2017  na tayari meneja huyo amesema ataziba pengo la coutinho kwa kumpanga Young lad Ben.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

   

 

Picha na mtandao

 

ULIMWENGU KUTIMKIA ULAYA

Na: Adam Ramadhan

Mshambuliaji  wa  timu  ya  Taifa  ya  Tanzania  Thomas  Ulimwengu  amekiri kwenda  kuanza  maisha  mapya  ya Soka barani  Ulaya  baada  mkataba  wake  wa  kuitumikia klabu  ya  TP Mazembe  ya  Congo DRC  kumalizika.

 

Licha  ya  klabu  ya  TP Mazembe  kutaka  kumuongezea  mkataba  mshambuliaji  huyo  hakuwa  tayari  na sasa  akili  yake  yote  ameielekeza  Ulaya,  huku akisema kuwa tayari  vilabu kadhaa  vimeanza  kumuhitaji  japo  hakutaka  kuviweka  hadharani.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

     
 

ST.MARY’S  YAPONGEZWA                           

Na:Ayoub Mwigune na Halima Katala

Afisa michezo mkoa wa morogoro Neema Msithar  ameupongeza uongozi wa shule ya St.Marys mkoani Morogoro kwa kuwa na utaratibu wa kuandaa siku ya michezo ambayo inawashirikisha wazazi pamoja na walimu kwani siku hiyo imekuwa ni nyenzo ya kujenga uhusiano mzuri kati ya walimu pamoja na wazazi .

 

Akizungumza kwa niaba ya Afisa huyo wa michezo   mkoa, Afisa elimu wa manispaa ya Morogoro  bi. Imakulata Fungo alisema kuwa michezo inatakiwa ipewe kipaumbele kwani inachangia sana katika kuufanya mwili  uwe na afya njema na kuongeza uwezo wa kufikiri pia aliomba walimu wa michezo kuendelea kuwafundisha watoto michezo mbalimbali kwani kufanya hivyo kutawajengea wanafunzi hali ya kupenda shule.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

   

 

Picha na matandao

 

MAMELODI SUNDOWNS YATWAA UBINGWA WA AFRIKA

Na: Adam Ramadhan

Klabu   ya  Mamelodi  Sundowns   wametangazwa   na  shirikisho  la  soka  Afrika  (CAF)  kuwa  mabingwa  wapya wa  Afrika  kwa  ngazi   za  vilabu  mwaka  2016  baada   ya  kuifunga  na   kufungwa   katika  michezo  miwili  ya  fainali   ya  mashindano  hayo  dhidi  ya  Zamaleki.

 

Mchezo   wa  mkondo   wa kwanza   wa  fainali  hizo  ulichezwa  katika  mji   wa Atteridgeville  Afrika  ya  Kusini  ambapo  Mamelodi  Sundowns  waliibuka  na  ushindi  wa  magoli  3-0 dhidi ya  wageni  wao  Zamaleki, katika  mkondo   wa  pili  hapo   jana  jumapili Mamelodi   Sundowns  wakafungwa   1-0  dhidi  ya  wenyeji  wao  Zamaleki.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

   

 

Picha na mtandao

 

CHELSEA YAIADHIBU MAN U

Na: Adam Ramadhan

Klabu   ya  Chelsea  jana Jumapili 23 mwezi huu imeiadhibu  kipigo  kikubwa  cha jumla  ya  magoli 4-0 klabu  ya  Manchester  United  katika  mchezo   wa   ligi  kuu   ya  nchini  England, mchezo   uliofanyika  katika  uwanja  wa  Stamford  Bridge .

 

Mchezo  huo  ulimrejesha kocha  aliyetimuliwa  msimu  uliopita  Jose Mourinho wa Chelsea   lakini   kwa  sasa  akiwa  ni  mkufunzi   wa  Manchester  United  na   kuambulia   kipigo   kikubwa  kikiwa  ni kipigo  kikubwa  zaidi kukipata  tangu  alipofungwa  na  Barcelona  magoli   5-0  Novemba  2010  katika  La  liga.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

   

 

                                                                     

Picha na mtandao

 

Man U YAINYUKA FENEBARCE 4-1

Na: Adam Ramadhan

Michuano   ya  Ligi  ndogo   ya  mabingwa  barani   Ulaya  imeendelea  tena  usiku   wa  kuamkia  leo  ambapo michezo  mbalimbali  imepigwa  katika  viwanja  tofauti  huku  Paul  Pogba  aking’ara  na  timu  yake  ya  Manchester  united.

 

Manchester   United   wakiwa  katika  uwanja   wa  Nyumbani   wameweza  kuibuka  na  ushindi   wa  goli  4-1  dhidi  ya  Fenebarce  na  kujiweka  katika  mazingira  mazuri  katika kundi  A   huku  Feyernod  wakiifunga  Zorya  goli  1-0.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........


 

     

                                                                

                  PICHA NA MTANDAO

 

AZAM FC YACHEZEA KICHAPO

Na:Ayoub Mwigune     

       
Ligi kuu ya Vodacom iliendelea hapo jana kwa michezo mbalimbali ambayo ilichezwa katika viwanja tofauti ambapo katika mji wa Shinyanga Stand united waliweza kuiadhibu klabu ya Azam fc kwa 1-0 na kuwafanya kushika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi wakiwa nyuma kwa alama moja nyuma ya vinara wa ligi hiyo Simba SC.


Jijini Mbeya klabu ya Mbeya City ilishindwa kutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kukubali kichapo cha 2-0 kutoka kwa vinara wa ligi hiyo Simba sc ambapo safu ya ushambuliaji ya Simba ikiongozwa na Kichuya na Ajibu ilionekana kuwa mwiba mbele ya safu ya ulinzi ya klabu hiyo ya Mbeya city.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

     

                                                                                    Picha na mtandao

 

NYERERE CUP KUENDELEA LEO

Na: Adam Ramadhan


Mashindano ya soka  ya  Nyerere   Cup   yaliyoanza  wiki   iliyopita  mkoani  Morogoro  yataendelea  tena  leo  kwa  kuwakutanisha  mafahari  wawili  kutoka  kihonda  Mlunda FC na  Topsite FC  katika  uwanja  wa  sabasaba majira  ya  saa 10:00  alasiri.


Hapo  jana  michuano  hiyo  iliendelea  ambapo  Chamwino  market FC  walitolewa  kwa  penati  na  timu  ya  Mwere  FC  kufuatia  sare   ya   jumla  magoli  2-2  katika  dakika  90.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

   

                                                                          

 

 SWANSEA YATIMUA KOCHA

Na: Adam Ramadhan

Klabu   ya    Swansea   city   imemfuta   kazi    kocha   wake   Fransesco   Gudolini  kutokana  na  mwenendo   mbaya   wa  klabu   hiyo   katika  ligi   kuu   ya   Uingereza   na   nafasi   yake   kuchukuliwa  na  Bod  Bradley.

Kocha   huyo   amefukuzwa  baada  ya  timu  yake   kupata   alama  nne   katika   michezo   saba   ya  ligi  hiyo.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

 

 

                                                                       

 

 

SAMMATA HATARI ZAIDI DAKIKA  20 ZA MWISHO

Na:Adam  Ramadhan 

Mshambuliaji Mbwana Samatta kutoka Tanzania  anayeichezea  klabu  ya  KRC Genk  ya Ubelgiji  tayari  amefikisha  mabao sita ukijumlisha yale ya Ligi Kuu ya Ubelgiji pamoja na michezo ya ligi ya  Europa.

 

Sammata  amefunga mabao hayo sita, mawili ni ya Europa na manne ni ya ligi lakini inaonekana  Samatta ni hatari zaidi katika dakika za mwisho hasa  akiingia  wakati  wa  mabadiliko.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 


 

 

 

 

 

 

                                                   

 

 MO BEJAIA YAJINASIBU KUBEBA UBINGWA

 

Na: Adam Ramadhan

Mchezo  wa   fainali  wa  kombe  la  shirikisho  utazikutanisha  klabu  za  MO Bejaia ya Algeria na TP Mazembe ya DRC  ambapo  itapigwa  mechi ya ugenini na nyumbani katika fainali inayozikutanisha timu zilizotoka kundi moja katika michuano ya makundi.

Mohamed  Sabah  ni  moja  ya  wanakamati   wa  benchi  la  ufundi  la  klabu  ya  MO Bejaia  amesema  kuwa  kwa  sasa  klabu  ipo   vizuri   na  wanamatumaini  makubwa  ya  kufanya  vyema  watakapokutana  na  mabingwa   watetezi  wa  kombe  hilo klabu  ya   TP Mazembe.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

     

Picha na mtandao

 

KILIMANJARO QUEEN FAINALI LEO CHALENJI

 

Na: Adam Ramadhan

Timu ya Soka ya Wanawake Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens, leo inatarajiwa kuvaana na Kenya katika mchezo wa fainali wa Kombe la Chalenji kwenye Uwanja wa Ufundi uliopo Njeru, mjini Jinja huko nchini Uganda.

Timu hiyo ya Bara ilitinga fainali baada ya kuwatoa wenyeji Uganda katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa mwishoni mwa wiki, ikishinda 4-1 huku nayo Kenya kwa upande wake ikiitoa Ethiopia katika mchezo mwingine wa nusu   fainali.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

     
                                                   

WAFANYAKAZI WA SUA WAHIMIZWA KUSHIRIKI MICHEZO YA IDARA

Na: Adam Ramadhan

Wafanyakazi  wa  chuo  kikuu  cha Sokoine  cha  kilimo (SUA)  wamehimizwa  kujitokeza wingi na  kushiriki   katika  michezo   iliyoandaliwa  na  idara  ya  michezo  ya  chuo  hicho  kwa   mwaka   2016, ambapo  michezo  hiyo  inatarajiwa  kuanza  Septemba  21.

Akizungumza  na  wajumbe  waliohudhuria  kikao   cha  kuandaa  mashindano  hayo  Mwenyekiti   Lwoga  Ladslaus  ambaye  pia  kiongozi   wa  Idara  ya  michezo  chuoni hapo,  amesema  kuwa  michezo  hiyo  itatoa  fursa  ya   kujenga  mahusiano  na  kufanya  afya  kuwa  bora  kwa  washiriki.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

     

 

SAVIO YAPANIA KUFANYA MAKUBWA MICHUONI YA KANDA TANO AFRIKA


Na:Alfred Lukonge


Mchezaji nguli ambaye pia ni mkufunzi wa mchezo wa mpira wa kikapu Mohamed Yusufu wa timu ya Savio amesema kuwa ana uhakika na timu yake kuchukua ubingwa wa mashindano ya kanda ya tano ya Afrika yanayotegemewa kuanza Oktoba 1 mpaka 7 katika viwanja vya ndani vya Taifa jijini Dar es Salaam.

" Kwa mazoezi tunayofanya na utimamu wa kila mchezaji siku zinavyokwenda kuelekea mashindano nina imani mwaka huu mwali lazima abaki Tanzania" amebainisha Yusufu.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

  

 

     

 

 

 

 

Picha na mtandao
 

 

 WACHEZA SOKA GHALI DUNIANI


Na: Adam Ramadhan

Mchezo   wa  Soka  kwa  sasa  ndio   umekuwa  mchezo  wenye  gharama  zaidi  duniani  hasa  katika  manunuzi  ya  wachezaji, lakini  pia  ndio  mchezo  wenye  mashabiki  wengi  zaidi  ulimwenguni  kwa  sababu  umekuwa  na  mvuto  sana.


SUAMEDIA  inakuletea  orodha  ya  wachezaji   walionunuliwa  kwa  bei  ghali  zaidi  duniani  mpaka  sasa, Paulo  Pogba  amesajiliwa  kutoka  Juventus  kwenda  Manchester  United  kwa  ada paundi  milioni 89 na  kuwa  mchezaji  ghali zaidi  duniani  kwa sasa.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

     

 

 

MICHEZO KWA WAFANYAKAZI WA SUA KUANZA SEPTEMBA 12


Na: Adam Ramadhan

Wafanyakazi  wa  chuo  kikuu  cha Sokoine  cha  kilimo (SUA)  wamehimizwa  kujitokeza  na  kushiriki   katika  michezo   iliyoandaliwa  na  idara  ya  michezo  ya  chuo  hicho  kwa   mwaka   2016, ambapo  michezo  hiyo  inatarajiwa  kuanza  Septemba  12.


Akizungumza  na  wajumbe  waliohudhuria  kikao   cha  kuandaa  mashindano  hayo  Mwenyekiti   Lwoga  Ladslaus  ambaye  pia  kiongozi   wa  Idara  ya  michezo  chuoni,  amesema  kuwa  michezo  hiyo  itatoa  fursa  ya   kujenga  mahusiano  na  kufanya  afya  kuwa  bora  kwa  washiriki.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

     

 

UHAMIAJI YAIBUKA KIDEDEA

Na: Fadhila Kizigo    

Timu ya Netball  Uhamiaji imeibuka na ushindi katika michuano ya ligi daraja la kwanza iliyofanyika mkoani Morogoro huku  Naibu Waziri wa Habari ,Sanaa,Utamaduni na Michezo  Mh. Anastazia Wambura  akitoa wito kwa wanawake kushiriki michezo ya Netball.

Uhamiaji imeibuka kidedea kwa kufunga magoli 776 kati ya michezo kumi waliyocheza na kufanikiwa kuwa mshindi wa michuano hiyo wakifuatiwa na timu ya Polisi Morogoro.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

     

 

 

 HAMOUD AVUTWA KATIKA AKADEMI YA PSG


Na: Adam Ramadhan

Uongozi wa mabingwa watetezi wa Ligi ya Ufaransa, PSG umeamua kumvuta katika akademi ya klabu hiyo mshambuliaji chipukizi wa Tanzania, Haytham Saadun Hamoud mwenye umri wa miaka 17 ambaye ni mzaliwa wa jiji la Dar es Salaam.

Safari yake ya soka ilianzia katika mpango wa kuzalisha vipaji kwa klabu ya Mtibwa Sugar, baada ya hapo alielekea Oman ndipo wasaka vipaji wa PSG walipomuona

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

     
 

NGASSA RUKSA KUJIUNGA NA KLABU YOYOTE KABLA YA SEPTEMBA 6

Na: Adam Ramadhan

Baada  ya  Mrisho  Ngassa  kurejea  nchini  akitokea  Afrika  ya  Kusini  kumekuwa  na hali  ya  sintofahamu  kwa  baadhi ya  wadau  wa soka nchini   juu   ya  kujiunga  na  iwapo Ngassa anaweza  kujiunga  na klabu yoyote inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara.

 Lakini  Afisa  habari  wa  TFF  Alfred Lucas  amesema  kuwa  Ngasa  anaruhusiwa  kujiunga  na  klabu  yoyote  kabla  ya  Septemba 6 mwaka huu  kabla  ya dirisha  kubwa  la usajili la FIFA  kufungwa.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

     
         

MICHUANO YA NETBALL LIGI DARAJA LA KWANZA KITAIFA MKOANI MOROGORO.

 Na: Suzane Cheddy

 

Katika michuano ya kitaifa ya netiboli inayoendelea mjini Morogoro, timu ya Polisi Arusha imeibuka na ushindi wa magoli 59 kwa 56 dhidi ya timu ya Tumbaku Morogoro.

Akizungumza na SUA MEDIA mwenyekiti kamati ya ufundi taifa Asha Sapi amesema kuwa michuano imeanza vizuri kutokana na wachezaji wote kuonyesha ushindani katika uchezaji pamoja na nidhamu kwa waamuzi.

  Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

 

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner