viwavi

Kiwavi jeshi vamizi akishambulia mahindi

 

 WAKULIMA WAILILIA SERIKALI KURUHUSU GMO

Na: Farida Mkongwe

Mahindi ni moja ya zao la nafaka linaloongoza kulimwa na wakulima wengi hapa nchini na barani Afrika kwa ujumla. Kwa kiasi kikubwa mahindi hulimwa kama zao la chakula, lakini likilimwa vizuri linaweza kutumika kama zao la biashara iwapo mavuno yake yatakuwa mengi na mazuri.

Wakulima wa zao hili la mahindi ambalo kwa Tanzania ndiyo zao kuu la chakula wamekuwa  wakikabiliwa na changamoto mbalimbali yakiwemo mabadiliko ya tabianchi ambayo  yamesababisha ukame wa mara kwa mara , ukosefu wa mbegu bora za mazao na mifugo, visumbufu na magonjwa ya mimea na mifugo pamoja na Matumizi  ya teknolojia duni ambavyo kwa pamoja vimemsababishia mkulima kuwa na uzalishaji duni wa mazao.

Bofya hapa kwa Habari zaidi.......... 

     
 

MBEGU BORA  NDIO CHANZO CHA MAVUNO MAZURI

                                                      

Na:Calvin Gwabara

Matumizi ya mbegu bora za mazao yote ya kilimo ni miongoni mwa mambo ambayo yamekuwa yakihimizwa na kusisitizwa na watafiti, wataalamu wa kilimo na viongozi wa serikali ili kumuwezesha mkulima kupata mavuno bora na kumhakikishia tija kwenye kilimo.

 

Upatikanaji wa mbegu hizo kwa upande wa wakulima imeendelea kuwa changamoto kubwa kutokana na wakulima wengi hususani vijijini kushindwa kumudu gharama za kununua mbegu bora kila msimu na kwenda kupanda mashambani.

Bofya hapa kwa Habari zaidi.......... 

 

   

 

 

 MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI NA MATUMIZI SAHIHI YA ARDHI.

Na: Kizito Natharine Ugulumo

ARDHI ni rasilimali muhimu kwa maendeleo ya jamii katika kujiletea maendeleo kwa kuitumia  kuendeshea shughuli za maendeleo ikiwemo kilimo,ujenzi wa makazi,ufugaji na shughuli zingine hivyo kutokana na umuhimu wake baadhi ya viongozi  kwenye vitongoji na vijiji wamekuwa wakitumia  umuhimu wa mahitaji ya ardhi kwa jamii kujinufaisha kwa kugawa ardhi bila kuzingatia sheria ,sera na kanuni zilizopo za ugawaji ardhi.

Hali hiyo imekuwa ikipelekea kuibuka kwa migogoro ya ardhi  mara kwa mara katika maeneo mbalimbali nchini na kwamba miongoni mwa sababu zinazochangia migogoro hiyo ni baadhi ya viongozi wa vijiji na vitongoji  kutaka kuingia madarakani kwa kutaka kujinufaisha ni miongoni mwa sababu zinazochangia kishamili kwa migogoro ya ardhi nchini.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

 

 

   

 

PICHA NA MTANDAO

 

TAKWIMU ZA UGONJWA WA KIPINDUPINDU KWA MWAKA 2015-2016 

Na: Neema Shayo   

Kipindupindu ni ugonjwa hatari unaoambukizwa kupitia chakula chenye vimelea ambavyo kitaalamu hujulikana kama VIBRIO CHOLERAE’  vimelea hivi huishi katika maji yaliyochafuliwa na kinyesi au matapishi

Kaimu mkurugenzi huduma za Afya na usafi wa mazingira Wizara ya Afya Theophil Likangaga amesema kuwa takwimu za mwaka 2015-2016 zinaonesha kuwa katika mkoa Morogoro vijana wenye umri kati ya miaka 21-45 wamekuwa ni wahanga wakubwa wa ugonjwa wa kipindupindu huku wakifuatiwa na wenye umri wa miaka 46 na kuendelea.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........


                   

 

     
 

SEHEMU YA 10 : UFUGAJI WA SAMAKI HATUA KWA HATUA

                                           ULISHAJI SAMAKI

Na: FARIDA MKONGWE

Katika sehemu ya 9 ya mfululizo wa makala hii ya ufugaji wa samaki tuliangalia suala la vyakula vya samaki ambapo tulijifunza aina za vyakula vya samaki pamoja na tabia za ulaji wa samaki ambazo zimegawanyika katika makundi 3 ambayo ni samaki wanaokula nyama, samaki wanaokula mimea vipando na samaki wanaokula vyakula mchanganyiko. Pia tuliangalia muongozo wa mahitaji ya viinilishe vya samaki pamoja na viwango vinavyohitajika kwenye kila viinilishe.

Katika sehemu hii ya 10 ya mwisho tunaangalia ulishaji wa samaki na hapa inasisitizwa kuwa ili samaki waweze kukua na kuzaliana vizuri ni lazima samaki wapewe chakula kwa kufuata mpangilio na utaratibu unaoshauriwa na wataalamu.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

     

 

YAJUE MAMBO 11 KUHUSU IKULU YA MAREKANI(WHITE HOUSE)

Na:Susane  Cheddy

Kuna mambo mengi usiyoyajua kuhusu ikulu ya marekani ambayo pengine kwa msomaji anaweza kushangazwa akiyajua.Hivyo katika kusherehekea Sikukuu ya Rais baadhi ya watu waliweza kutoa mambo 11 kuhusu ikulu ya Marekani ambayo ina jumla ya vyumba 132 na imejengwa katika eneo la ukubwa wa mita za mraba 17,000. Mambo hayo ni haya yafuatayo:

Awali ilijulikana tu kama jengo la West Wing ni ofisi za watendaji. West Wing ilijengwa na Rais Teddy Roosevelt akiwa na lengo la kutenganisha makazi na sehemu za ofisi. Hata hivyo alipoingia madarakani Rais Taft akaamua kuunganisha jengo la ofisi la West Wing na majengo ya makazi akisema anataka kuhusika zaidi na shughuli zzote za White House.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

     
 

JINSI YA KUPIKA KABICHI ILIYOCHANGANYWA NA MAYAI

 

Na: HUSNA YAHYA

Kabichi ni aina ya mboga za majani ambayo hupikwa kwa  mapishi tofauti. Unaweza kupika kabichi yenyewe bila kuchanganya na chochote pia  unaweza kupika kwa kuchanganya na nyama, mayai au chochote unachoona kinafaa mboga yako itakuwa nzuri   na kuweza kuliwa na ugali, wali na hata kupikia pilau.

Leo  tutaangalia jinsi ya kupika kabichi iliyochanganywa na mayai, ambapo tunaanza na mahitaji pamoja na  hatua za kufuata katika upikaji wa kabichi iliyochanganywa na mayai.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

     

PICHA NA MTANDAO

 

SEHEMU YA 9: UFUGAJI WA SAMAKI HATUA KWA HATUA

                                           VYAKULA VYA SAMAKI

 

Na: FARIDA MKONGWE

Katika sehemu ya 8 ya mfululizo wa makala hii ya ufugaji wa samaki tuliangalia suala la masoko ambapo tuliona kuwa kuna aina 3 za masoko ambazo ni soko la awali, soko la kati na soko la kimataifa. Pia tuliona changamoto kubwa inayowakabili wafugaji wa soko la kati ambayo ni wanunuzi kuungana na kumpangia bei mkulima na ili kukabiliana na changamoto hiyo wafugaji wameshauriwa kuunda chama chao ambacho kitakuwa na uwezo wa kupanga bei na hivyo kutokubali bei watakayopangiwa na watu wa kati.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

     
PICHA NA MTANDAO  

SEHEMU YA 8: UFUGAJI WA SAMAKI HATUA KWA HATUA

                               HATUA YA 6: MASOKO

Na: FARIDA MKONGWE

Katika sehemu ya 7 ya mfululizo wa makala hii ya ufugaji wa samaki tuliangalia hatua ya 5 ambayo ilizungumzia uvunaji, usindikaji na uhifadhi wa samaki.

Katika uvunaji tuliona kuwa mfugaji anaweza kupunguza maji kwenye bwawa ili samaki waweze kuvuliwa kwa urahisi lakini pia kutokana na uhaba wa maji mfugaji anaweza asipunguze maji badala yake akavua samaki kwa kutumia nyavu yenye macho yanayokubalika kitaalamu. Kwa upande wa usindikaji na uhifadhi tuliona kuwa samaki wanaweza kuhifadhiwa kwa kutumia chumvi, moshi, kuwakaanga kwenye mafuta na kuwagandisha kwenye barafu.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

     
 

SEHEMU YA 7: UFUGAJI WA SAMAKI HATUA KWA HATUA

HATUA YA 5: UVUNAJI, USINDIKAJI NA UHIFADHI WA SAMAKI

Na: FARIDA MKONGWE

Katika sehemu ya 6 ya mfululizo wa makala hii ya ufugaji wa samaki tuliangalia hatua ya 4 ambayo ilizungumzia ulishaji na utunzaji wa samaki bwawani.

Katika hatua hiyo tuliona kuwa samaki  wanatakiwa wapewe chakula angalau mara 2 kwa siku, samaki wapewe vyakula tofauti kutegemeana na silka yao, mfugaji anatakiwa kukagua kiwango cha hewa kilichopo kwenye maji angalau mara 2 kwa wiki pia maji yanatakiwa yafanyiwe ukaguzi dhidi ya hewa chafu.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

   

 

PICHA NA MTANDAO  

UGONJWA WA KICHOCHO/BILHARZIA

Na: CONSOLATA PHILEMON

Kichocho ni ugonjwa unaosababishwa na minyoo midogo aina ya Schistosoma au Bilhazia ambayo huingia katika mwili wa binadamu kwa njia ya vitundu vya ngozi na kusababisha mwasho katika viungo mbalimbali vya mwili na kupelekea homa, mwili kudhoofu, kupungukiwa kinga mwilini na hatimaye mtu kupoteza maisha.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

   

 

PICHA NA MTANDAO  

KILIMO MSETO MKOMBOZI WA UMASIKINI

Na: CONSOLATA PHILEMON

Kilimo mseto ni aina ya kilimo kinachoweza kuhusisha upandwaji wa miti, mimea ya mazao na wanyama huku lengo likiwa ni utunzaji wa mazingira pamoja na kumuingizia mwananchi wa kipato.

Hapo mwanzo kilimo mseto kilifahamika kuwa kilimo cha miti na mimea ya mazao lakini kwa sasa kuna aina zaidi ya kumi na tano (15) za kilimo mseto ambazo zinazohusisha mchanganyiko wa Miti, Mazao na Mifugo yenye uhusiano uwezao kukaa katika mazingira na kuwiana.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

     
PICHA NA MTANDAO  

SEHEMU YA 6: UFUGAJI WA SAMAKI HATUA KWA HATUA

HATUA YA 4: ULISHAJI NA UTUNZAJI WA SAMAKI BWAWANI

Na: FARIDA MKONGWE

Katika sehemu ya 5 ya mfululizo wa makala hii ya ufugaji wa samaki tuliangalia hatua ya 3 ambayo ilizungumzia uandaaji na upandikizaji wa vifaranga au mbegu za samaki katika bwawa.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

     

 

RUSHWA SABABU MOJA WAPO YA UMASKINI TANZANIA

Na: ALFRED LUKONGE

Kwa mujibu wa shirika la kupima viwango vya Rushwa Duniani (WCB) mwaka 2013 Tanzania ilikuwa ni miongoni mwa nchi 14 vinara wa rushwa  inayopelekea kuwa chanzo kikuu cha umaskini na maendeleo ingawa kuna rasilimali nyingi.

Kutoka Ruvuma mpaka Dar es Salaam, Kutoka Mbeya mpaka Kigoma, rushwa imeendelea kudidimiza  maendeleo  ya watanzania na kuathiri maisha yao kiujumla. Ndiyo maana kila siku tunapigana vita ya uchumi, siasa na maendeleo ya  teknolojia pasipo kuona mabadiliko.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

   

PICHA NA MTANDAO

 

SEHEMU YA 5: UFUGAJI WA SAMAKI HATUA KWA HATUA  HATUA YA 3: UANDAAJI NA UPANDIKIZAJI WA VIFARANGA VYA SAMAKI

Na: FARIDA MKONGWE

Katika sehemu ya 4 ya mfululizo wa makala hii ya ufugaji wa samaki tuliangalia hatua ya 2 ambayo ilizungumzia uchimbaji wa bwawa la samaki. Katika hatua hiyo tuliona kuwa hakuna vipimo maalum vya ukubwa wa bwawa maana ukubwa wa bwawa unategemea eneo na malengo ya ufugaji, bwawa linatakiwa kuchimbwa upande mmoja uwe na kina au umbali wa  mita 1.5 na upande mwingine mita 1 na sentimita 20 kwenda chini, umbo la bwawa liwe mstatiri, kitako cha bwawa kiwe na mwinuko upande mmoja, kingo za bwawa zinatakiwa ziwe zimechongwa kuegemea nje ili kukinga bwawa lisibomoke wakati wa kujaza maji, na bwawa linaweza kuchimbwa kwa mikono au kwa mashine kutegemeana na uwezo wa mfugaji.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

   

 

                                  PICHA NA MTANDAO

 

 

WATANZANIA TUFANYE KAZI KWA BIDII

Na: MNGEREZA MNTAMBO

 

Kutokana na Kauli Mbiu ya Rais wetu Dr John Pombe Magufuli “Hapa kazi tu” leo nimeamua kuzungumza kuhusu kufanya kazi kwa bidii. Njia pekee ninayofikiria ya kujihamasisha kufanya kazi kwa bidii ni kujitambua kwamba unataka kuwa nani, baada ya hapo lazima ufanye maamuzi kutoka moyoni kwamba unahitaji kuwa mchapakazi.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

   

 

   PICHA NA MTANDAO  

ASILIMIA 80 YA WATU BARANI AFRIKA WANAUGUA UGONJWA WA SELIMUNDU

  Na:TATYANA CELESTINE