Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Mlingano kwa kushirikiana na wadau wengine wameanza utafiti wa kuwezesha zao la mkonge kuzalisha Mvinyo

Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Mlingano kwa kushirikiana na wadau wengine wa ndani na nje ya Tanzania wameanza utafiti wa kuwezesha zao la mkonge kutoa bidhaa ya Mvinyo katika zao la mkonge kutokana  na Tanzania kupata nyuzi pekee ambayo ni sawa na asilimia mbili ya bidhaa zinazotokana na zao hilo.

Mpango huo umebainishwa na Mkuu wa Kituo hicho Dkt. Catherine Senkoro wakati akizungumza na Waandishi wa habari kutoka kanda ya mashariki na watafiti wa kanda hiyo waliokuwa kwenye mafunzo kwa vitendo juu ya uandishi wa habari za sayansi yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na teknolojia COSTECH.
Dkt.Senkoro amesema kwa uasilia wa tafiti wanazofanya kituoni hapo hawajafanya zaidi utafiti huo lakini wanashirikina na watafiti wa chuo kikuu cha Dar es salaam,Bodi ya Mkonge na wengine kutoka nchini Marekani katika kuangalia namna ya kutumia mkonge uliozalishwa kituoni hapo ili uweze kutumika kuzalisha bidhaa mvinyo.
”Tafiti zilizofanyika dunia nzima ni lakini sisi cha kufanya ni  kuzichukua kuanza  kuishauri Serikai ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuona namna  ambavyo zitatumika na nchi iweze kuzalisha bidhaa zingine zaidi ya Nyuzi” Alisema Dkt. Senkoro.
Dkt. Senkoro amesema kuwa kupitia watafiti wa kituo hicho wameweza kuzalisha aina bora ya Mbegu ya Mkonge ambayo inatumika sasa duniani kote hasa China pamoja na teknolojia zingine za kuzuia magonjwa yanayosumbua kilimo hicho.
Kwa upande wake Mtafiti kiongozi wa zao la Mkonge kituoni hapo Bw. Gerson Mkolongwe amesema kuwa kwa sasa Tanzania inatumia asilimia mbili pekee na asilimia 98 inatupwa hivyo watafiti wanaangalia namna gani wanaweza kusaidia mkonge kutoa bidhaa nyingi.
Aidha Bw. Mkolongwe amesema mradi utasaidia wakulima wa mkonge katika kuongeza kipato pale ambapo Mkonge unakifikisha miaka 12 hadi 15 na kutoa lingoti kwani watawauzia watu wenye viwanda kwaajili ya kutengeneza bidhaa mbalimbali
Bw. Mkolongwe amesema utafiti unaonesha kuwa Mkonge uliozeeka unakuwa na Sukari nyingi  ambayo hutumika kutengeneza Kinywaji na kemikali aina ya Ithano hivyo mkulima atapata faida badala ya kuingia gharama za kuvunja shamba kama ilivyo sasa.
”Ule mradi ukifanikiwa yale mashina yaliyozeeka hayatupwa tena na wakulima wengi watajiunga kwenye kilimo cha mkonge kwakuwa faida itakuwa kubwa na itampunguzia gharama” Alisema Mkolongwe.
Kwa upande wake Mtafiti mkuu anayeshughulikia masuala ya makala na machapisho kutoka COSTECH Dkt. Bakari Msangi amesema kuwa tayari kwa sasa kuna mtambo wa kuzalisha umeme ambao unaingia kwenye greed ya taifa ambao unatokana na mabaki ya zao la mkonge na hiyo ni dalili njema kuwa wakulima nanchi itanufaika na zao hilo.
Vilevile kituo hicho kwa kushirkiana na kituo cha Nyumbu wamebuni mashine inayotembea na kuchubua Mkonge ili kupata nyuzi hapohapo shambani badala ya utaratibu wa zamani wa kuvuna na kuusafirisha umbali mrefu kwenda kwenye vituo vya kuchubua nyuzi.

Rais Magufuli  ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Malinyi  mkoani Morogoro

Rais Magufuli  ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Malinyi  mkoani Morogoro, Majura Mateko Kasika na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mussa Mnyeti.

MGAGG

WAFUGAJI WA NG'OMBE WA MAZIWA WAASWA KUTUMIA TAFITI ILI KUONGEZA TIJA

Na: Calvin E. Gwabara
Uongozi wa Kiwada cha kusindika maziwa cha Tanga Fresh  kimewashauri wafugaji  Kanda ya Mashariki na Tanzania kwa Ujumla kutumia matokeo ya tafiti mbalimbali za kisayansi za ufugaji wa Ng'ombe wa maziwa ili kuongeza tija.

 
Meneja Vyanzo vya maziwa wa kiwanda cha kusindika maziwa cha Tanga Fresh  Bi. Nadomana Nyanga  akiongea na Waandishi wa habari wa Kanda ya Mashariki na watafiti 


Wito huo umetolewa na Meneja Vyanzo vya maziwa wa kiwanda hicho Bi. Nadomana Nyanga wakati akiongea na Waandishi wa habari wa Kanda ya Mashariki na watafiti waliokuwa kwenye mafunzo kwa vitendo mafunzo ya namna ya kuandika habari za Sayansi,Teknolojia na ubunifu yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia  (COSTECH).

Bi.Nyanga amesema kiwanda hicho kinauwezo  wa kusindika lita 120,000 kwa siku lakini wanapata maziwa lita  30,000 hadi 50,000 za maziwa kwa siku,kiwango kisichokidhi mahitaji kutokana na uwezo mdogo wa ng'ombe kutoa maziwa.

Amesema sayansi ndio njia pekee ambayo ikitumiwa vizuri inaweza kusaidia kuongeza uzalishaji wa maziwa kwa kiasi kikubwa na hivyo kuondoa pengo kubwa la ukosefu wa maziwa huo ambao unapelekea wao kufuata maziwa kwenye mikoa mbalimbali ya nje ya Kanda ya mashariki hasa katika wakati wa kiangazi ambapo malisho huwa ya tabu.

Meneja huyo wa Vyanzo vya maziwa ameongeza kuwa wao kama kiwanda  wanashirikiana na Taasisi ya Utafiti wa mifugo Tanzania TALIRI  katika kuhakikisha wanapata malisho bora yaliyofanyiwa utafiti pamoja na aina bora za ng'ombe wanaotoa maziwa mengi tofauti na hawa wa asili.
“Ng'ombe wanapopitia kwenye mahangiko yaani (stress) wanapoteza uwezo wao wa kutoa maziwa bora hivyo ni muhimu wafugaji wakatumia ushauri wa watafiti katika kuhakikisha wanasimamia mahitaji muhimu ya mifugo hasa malisho,maji na afya" Alisisitiza Bi. Nadomana Nyanga.Kiwanda cha kusindika maziwa cha Tanga Fresh cha jijini Tanga
Amebainisha kuwa pia kiwanda kinahamaisha unywaji wa maziwa kwa watanzania kutoka na jamii kutokuwa na muamko wa unywaji maziwa kwani kwa Tanzania mtu mmoja anakunywa watstani wa lita 47 kwa mwaka wakati wenzetu majirani Wakenya mtu anakunywa lita 100 kwa mwaka hivyo ili kufikia huko lazima hamasa itolewe kwa jamii lakini pia uzalishaji uongezeke.


Katika hatua nyingine katika kuongeza maslahi na ubora wa maziwa amesema kiwanfa hicho cha Tanga fresh kinataka kuanzisha utaratibu wa kuwalipa wafugaji bei kutokana na ubora wa maziwa wanayozalisha kama nchi zingine duniani zinavyofanya.


"Zimbabwe wanawalipa wafugaji kwa kutokana na ubora wa maziwa hivyo sisi kama viongozi wa sekta kwenye maziwa nchini tunaona tuanze kufanya hivyo pia ili kuwahamasisha wafugaji kuzingatia mbinu bora za ufugaji ili ng'ombe wao watoe maziwa bora na yenye viwango” Alisisitiza Bi. Nyanga.


Akizungumzia changamoto hiyo ya uchache wa maziwa,tatizo la malisho Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti wa mifugo Tanzania ofisi ya Kanda ya Mashariki Dkt. Zabron Nziku amesema malisho duni ndio sababu ya uzalishaji mdogo wa maziwa kwa mifugo hivyo kituo chake kinafanya utafiti wa malisho bora ambayo wafugaji wakiyatumia yatasaidia kuongeza uzalishaji na kipato.

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti wa mifugo Tanzania ofisi ya Kanda ya Mashariki Dkt. Zabron Nziku akiongea na Waandishi wa habari wa Kanda ya Mashariki na watafiti walipotembelea kituoni kwake

Amesema tayari wanazo aina mbalimbali za malisho ya mifugo ambayo wanayafanyia utafiti katika kituo chake na yameonyesha kufanya vizuri lakini yapo ambayo tayari wafugaji wameshaanza kuyatumia kuwalisha mifugo yao baada ya kazi kubwa ya kukusanya aina bora za malisho nchi nzima na kuyachambua.


Dkt. Nziku amesema pamoja na malisho pia wanazo teknolojia rahisi za utunzaji wa malisho am,bazo wanawashauri wafugaji kuzitumia ili kuhifadhi malisho kwaajili ya kiangazi ambapo kunakuwa na uhaba wa malisho na kusababisha kushuka kwa uzalishaji wa maziwa.
"Tuna wafugaji ambao sasa wanatenga maeneo makubwa sana kwaajili ya kuzalisha chakula bora cha mifugo na kwakweli mahitaji ni makubwa sana hivyo niwashauri watanzania kuingia kwenye kilimo cha malisho ya mifugo maana soko lipo ndani nan je ya nchi” Alisistiza Dkt. Nziku.

Amesema Tanzania inashika nafasi ya pili kwa kuwa na ng'ombe wengi lakini uzalishaji wake wa maziwa kwa ngombe mmoja ni wastani wa lita 5 kwa siku wakati nchi zingine duniani ngombe mmoja anatoa maziwa lita 30 kwa siku na hivyo kuboresha maisha ya wafugaji.

Jamii imeshauriwa kuangamiza Mbu kwa viatilifu mseto 

Na: Calvin Gwabara

Jamii imeshauriwa kutumia dawa za kupulizia zenye mseto wa viatilifu kama njia Mojawapo ya kuangamiza Mbu waenezao Malaria ,Usubi na Dengue.

Wito huo umetolewa na Dkt. Patrick Tungu ambaye ni Mtafiti kutoka Taasisi ya utafiti wa magonjwaya binadamu (NIMR) kituo cha Amani Tanga wakati wa mafunzo ya Watafiti na Wanahabari kuhusu Uandishi wa habari za sayansi yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

Dkt. Tungu amesema kuwa dawa jamii imekuwa ikitumia Dawa za kuua Mmbu ambazo zina kiuatilifu kimoja tuu na hivyo kushindwa kuwaangamiza wadudu hao.

 WhatsApp Image 2019 09 12 at 9.43.04 AM

Amesema baada ya utafiti waliofanya kituoni hapo wamegundua kuwa ili kufanikiwa vizuri kuangamiza Mbu lazima kiautilifu zaidi ya kimoja kiwe kimechanganywa kwenye dawa hiyo.

Mtafiti huyo kutoka NIMR Tanga amesema Mbu kama walivyo wadudu wengine wanapopuliziwa dawa kwa muda mrefu huamza kuzoea dawa hiyo na hivyo kujijengea usugu lakini kwa kutumia dawa zenye Viatilofu mchanganyiko inasaidia kuwaangamiza.

 Capture mbu

“Dawa za kupuliza kupambana na wadudu kama Mbu zimekuwa zikitumika kwa madhumuni ya kuangamiza lakini zimekuwa zikiwafaa kwa muda mchache na kuendelea kupata maginjwa hayo yaenezwayo na Mbu” Alisema Dkt. Tungu.

Ameongeza kuwa pamoja na kutumia njia zingine za kuondoa mazalia yao lakini wanapokwenda madukani lazima waangalie dawa hizo ambazo zina changanyiko wa Viuatilifu.

Malisho duni chanzo cha tija ndogo kwa wafugaji wa ng'ombe wa maziwa

Na:Calvin Gwabara

Tafiti zinaonesha malisho duni ya mifugo ndiyo yanayopelekea kushuka kwa uzalishaji wa maziwa kwa wafugaji wengi nchini Tanzania.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa utafiti wa mifugo (TALIRI) Kilichopo Mkoa wa Tanga Dkt. Zabroni Nziku wakati akiongea na Waandishi kwenye Mafunzo ya Uandishi wa habari za Sayansi Teknolojia na Ubunifu kwa Wanahabari na Watafiti kutoka Kanda ya Mashariki yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na teknolojia (COSTECH)


IMG 20190912 WA0041

Mkurugenzi wa utafiti wa mifugo (TALIRI)Mkoa wa Tanga Dr.Zabroni Nziku katikati

Dkt. Nziku amesema katika tafiti iliyofanyika katika kituo hicho chake imeonesha wafugaji walio wengi wakiwemo wafugaji wa Mkoa wa Tanga wanashindwa kulisha mifugo yao chakula bora na hivyo kujikuta wanazalisha maziwa kidogo.

Amesema kwa wastani nchini Ng’ombe wa maziwa anazalisha lita 5 za maziwa kwa siku ikilinganishwa na nchi nyingine duniani ambazo Ng’ombe mmoja anatoa lita 30 kwa siku na hivyo kutoa tija kubwa kwa wafugaji.


Cow1

Hata hivyo Mkurugenzi huyo wa TALIRI kituo cha Tanga Dkt. Nziku amesema baada ya kugundua tatizo hilo amesema wameanza kutoa ELIMU kwa wafugaji kuanza kulima malisho ya mifugo na kuyatumia kwaajili ya kuyatumia wakati wa kiangazi ambapo malisho huwa ya tabu na ndicho kipindi maziwa huwa kidogo zaidi.

Amesema pamoja na kutoa elimu lakini pia wanafanya tafiti za kupata aina bora za malisho ya mifigo na kuwahamasisha wafugaji na Wakulima wengine kuanza kulima malisho kutokana na kuwa na faida kubwa lakini hayapatikani.

Dkt. Nziku amesema pamoja na kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya malisho lakini pia wanazalisha aina bora za mbegu za ng’ombe wa maziwa ambao wanatoa maziwa mengi ikilinganishwa na ng’ombe wa asili.

Kwa upande wake Afisa utafiti kutoka kituo hicho cha TALIRI Tanga Mariam Katarama amewashauri wafugaji pia kuaona fursa iliyopo ya ufugaji wa mbuzi wa maziwa kutokana na kuhitaji matunzo kidogo tofauti na ng’ombe lakini pia maziwa yake kuwa na faida nyingi.

Amesema ufugaji wa mbuzi ni rahisi na hauhitaji sehemu kubwa kama ilivyo kwa ng’ombe lakini pia wanaweza kutoa maziwa ya kutosha familia na mengine yakauzwa na kuongeza kipato na Lishe kwa jamii.

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ( COSTECH) imewakutanisha waandishi wa habari na watafiti kutoka Kanda ya Mashariki

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ( COSTECH) imewakutanisha kwenye mafunzo waandishi wa habari na watafiti kutoka Kanda ya Mashariki ili kuwajengea uwezo wa kufikisha matokeo ya Sayansi Teknolojia na ubunifu kwa walengwa.


IMG 7644Dkt. Emmanuel Nnko Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Makala na machapisho


Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufungua mafunzo hayo ya siku mbili kaumu Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya taarifa Emmanuel Nnko aliyemiwakilisha mkurugenzi Mkuu wa COSTECH amesema mafunzo hayo ni muendelezo wa jitihada za Tume za kuhakikisha Tafiti zinazofanywa nchini ili ziweze kuleta tija kwa jamii.


IMG 20190912 WA0040 1  Afisa Utafiti Mkuu Kiongozi anayeshughulikia Makala na Machapisho kutoka COSTECH Dkt. Bakari Msangi akiongea na waandishi wa habari mkoani Tanga.


Akifungua mafunzo hayo yaliyohusisha watafiti na waandishi kutoka Kanda ya Mashariki Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi za utafiti wa mifugo Tanzania (TALIRI) Dkt. Zabron Nziku amesema Matokeo ya utafiti ndiyo yanayoweza kusaidia Uchumi wa viwanda endapo yatawafikia walengwa na kuyatumia.

Amesema kuwa tafiti nyingi zinafanywa lakini zinaishia kwenye vituo vya utafiti na hivyo wananchi na wadau wa tafiti hizo kutonufaika nazo wakati zimetumia fedha nyingi.

Amepongeza programu hiyo ambayo inafanywa na COSTECH nchi nzima na kuwataka waandishi wa habari kuyafanyia kazi ili yaweze kusaidia jamii ya watanzania.
IMG 20190912 WA0036
Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kufungua mafunzo hayo Emmanuel Nnko kaimu Mkurugenzi wa Idara ya menejimenti ya Taarifa kutoka COSTECH aliyemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Tume amesema  mafunzo hayo ni muhimu kwani yanasaidia kuwaleta pamoja wansayansi na waandishi wa habari na kupanga mikakati ya namna wanavyoweza kushirikiana katika kusaidia jamii na Taifa kwa kubuni njia bora za kuwafikishia wadau matokeo ya tafiti hizo.

Amesema mafunzo hayo ni sehemu ya mafunzo kwa waandishi wa habari na watafiti ambayo yanafanyika nchi nzima ili kusaidia kufikia malengo kufanyika kwa tafiti mbalimbali zinazofanyika nchi nzima kwenye vituo na Taasisi mbalimbali.

Akizungumzia umuhimu wa mafunzo hayo Afisa Programu ya Mafunzo hayo kutoka COSTECH Bw. Merchades Rutechura amesema ni kupunguza gepu kati ya watafiti na watumiaji wa tafiti hizo nchini.

Amesema kuwa toka mafunzo hayo yaanze kwenye kanda mbalimbali kumekuwa na ongezeko kubwa la Makala,vipindi na habari za Sayansi,Teknolojia na Ubunifu na hivyo kusaidia jamii kujua ni wapi wanaweza kuzipata ili kuzitumia kwenye shughuli zao mbalimbali za uzalishaji na kuongeza tija.

Amewataka waandishi hao wa Kanda ya Mashariki inayojumuisha Mikoa  ya Dar es salaam,Pwani, Morogoro na Tanga kutumia kusanyiko hilo kujua miiko ya utoaji wa taarifa na kujenga mashirikiano na watafiti ili kuweza kuwatumia katika uandaaji wa vipindi vyao.

Akiwasilisha mada kuhusu Utafiti na umuhimu wa kutoa matokeo ya utafiti Afisa Utafiti Mkuu kiongozi anayeshughulikia Makala na Machapisho kutoka COSTECH Dkt. Bakari Msangi waandishi wa habari wana umuhimu Mkubwa katika kufanya kazi hiyo kwakuwa wanasikilizwa na kuaminiwa na jamii.

Dkt. Msangi amesema katika kazi yoyote kuna miiko na maadili yake hivyo waandishi wa habari nao ni lazima wajue miiko na maadili ya kuandika habari na kuandaa vipindi vya Kisayansi na ubunifu ili waweze kufanya kazi hiyo vizuri kwa maslahi ya taifa bila kuleta matatizo kwa mtafiti na mwandishi mwenyewe.

Amesema habari za kisayansi zinahitaji ubunifu kwenye kupeleka kwa walengwa kwa kuandika habari zenye lugha nyepesi, Ufupi na kwa kutumia njia ambayo inaweza kuwafikia walengwa katika eneo fulani iwe Redio,Televisheni au Magazeti.

Dkt. Msangi amesema kuwa mbali na kuwafikia wakulima na wafugaji lakini pia inasaidia kuwafikia watoa maamuzi kutumia

Watafiti wa Tanzania wamegundua mbinu ya kukabiliana na Mbung’o kwa wanyama

Na: Calvin Gwabara

Watafiti wa Tanzania wamegundua mbinu ya kukabiliana na Mbung’o wanaosababisha  vimelea vya was  Nagana kwa wanyama na vimelea vya Ugonjwa wa malale kwa binadamu.

IMG 7485

Mtafiti Deusdedit Malulu akiwasilisha mada yake kwa waandishi wa habari na watafiti kwenye mafunzo hayo jijini Tanga.

Haya yamebainishwa na Afisa Utafiti Mifugo kutoka Wakala wa Maabara za Veterinary Kituo cha Tanga Bw. Deusdedit Malulu wakati wa mafunzo ya uandishi wa habari za sayansi,teknolojia na ubunifu yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na teknolojia COSTECH yaliyowakutanisha waaandishi wa habari na watafiti kutoka kanda ya Mashariki.

Bwana Malulu amesema katika kutafuta njia mbadala ya kukabiliana na Mbung’o wamebaini mnyama aina ya Kuro hashambuliwi na mbung’o kama wanyamapori wengine na kubaini kuwa mnyama huyo anatoa harufu ambayo mbung'o  huogopa na hivyo kushindwa kumkaribia.
IMG 7582
Amesema baada ya utafiti wao maabara wamebaini kuwa harufu hiyo inauwezo wa kufukuza Mbung’o kwa zaidi ya asilimia 60 ikilinganishwa na teknolojia zingine zilizopo sasa.

Bwana Malulu ameongeza kuwa baada ya kutambua kemikali zilizopo kwenye harufu hiyo ya Kuro wakachanganya kemikali za aina hiyo ili kuizalisha maabara inayofanana na ile ya Kuro na kuwakinga na kushambulia na Mbung'o hao.

Mtafiti huyo amebainisha kuwa ili kuhakikisha harufu hiyo inawafikia walengwa kwa maana ya wafugaji na hivi sasa wanatengeneza kifaa maalum ambacho kitakuwa kinabeba harufu.

“Hivi sasa tunashirikiana na Kiwanda cha A to Z cha Jijini Arusha katika kutengeneza kibebeo hicho cha harufu hiyo kwa mifugo” Alisema Bwana Malulu.

Ameongeza kuwa hatua hiyo ya kubuni kibebeo inakwenda sambamba na hatua za kufanya usajili na majaribio katika maeneo husika

HABARI MPASUKO:Robert Mugabe amefariki dunia

Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe amefariki dunia.

images

Mmoja wa wanafamilia ameithibitishi, Robert Mugabe amefariki dunia akiwa na miaka 95.

Mugabe alikuwa nchini Singapore akipokea matibabu kwa muda mrefu.

Ameiongoza Zimbabwe kutoka 1980 mpaka 2017, alipong'olewa madarakani na makamo wake kwa msaada wa jeshi.

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa tayari amethibitisha kupitia mtandao wa twitter juu ya taarifa za kifo hicho.

"Kamarada Mugabe alikuwa ni mwanga wa mapinduzi, mwana umajui wa Afrika ambaye aliyatoa maisha yake katika ukombozi na kuwawezesha watu wake. Mchango wake kwa taifa letu na bara (la Afrika) hautasahaulika..." ameandika Mnangagwa.

Taarifa zaidi zitaendelea kukujia.

TANAPA YAMPA TUZO MTAFITI WA SUA KWA UTAFITI BORA WA WANYAMAPORI

Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi TANAPA,  Bw. Godwell Ole Meing’ataki amekishukuru  Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo,SUA kwa mchango
mkubwa wanaoutoa kwa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi  TANAPA,Bw. Ole Meing’ataki akimkabidhi tuzo   Prof. Rudovick Kazwala kutoka Ndaki ya Tiba ya
wanyama na sayansi za afya yaChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo,SUA
 
Kamishna Ole Meing’ataki ameyasema hayo katika hafla fupi ya kukabidhi tuzo kwa   Prof. Ludovick Kazwara kutoka Ndaki ya Tiba ya wanyama na sayansi za
afya ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo,SUA iliyofanyika chuoni hapo.
Akikabidhi tuzo hiyo Kamishna Msaidizi wa uhifadhi  TANAPA,Bw. Ole Meing’ataki amekipongeza Chuo pamoja na Uongozi  kwa kupata tuzo hiyo, Pia kwa
mapokezi waliyofanya ambayo yameweka alama ya ushirikiano na umoja katika utendaji kazi nchini.
Amesema Tuzo hizo zinazotambulika kama TANAPA TOURISM AWARDS na ndio mara ya kwanza kutolewa zikiwa na vipengele mbalimbali
ikiwemo  cha kushindania Utafiti uliofanyika kwa muda mrefu ambao umebeba taarifa nyingi zilizosaidia katika Utalii. 
Amesema  kipengele hicho ndicho ambacho   Prof. Rudovick Kazwala ameibuka kinara kutoka kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, SUA. 
Akipokea tuzo hiyo Prof. Kazwala amesema amefurahi sana  kupata tuzo hiyo na hivyo kushauri wadau na wananchi kulinda hifadhi na vivutio mbalimbali
vya Taifa ili vizazi vijavyo viweze kunufaika na rasilimali hizo.
Amesema Tuzo hiyo ni ishara kwamba Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kina mchango mkubwa katika kusaidia uhifadhi wa wanyama na vivutio
vingine vya taifa.
Pia mshindi huyo wa tuzo hiyo  ameomba tafiti zinazolenga kuboresha afya za Wanyamapori na mimea zipewe kipaumbele ili kuweza kuleta tija kwenye
uhifadhi na  utalii nchini.
Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu kamishna huyo Makamu wa Mkuu wa Chuo Prof. Raphael Chibunda amesema tuzo hiyo ni heshima kwa
Mtafiti mwenyewe lakini pia ni hehima kwa Chuo.
Amewapongeza TANAPA kwa kutoa zawadi hizo kwa watu waliochangia kwenye kazi mbalimbali za kutunza na kuhifadhi utalii wa Tanzania kwani inaongeza
chachu ya watafiti na watu wengine kushiriki kwenye kutunza maliasili hizo za taifa.

Prof. Kazwara  ni mtafiti mzawa aliyebobea  ambaye amefanya tafiti ndani ya hifadhi za wanyamapori hasa  tafiti zinazolenga afya za wanyamapori nchini amepata tuzo hiyo kutokana na mchango wa tafiti hizo kwenye masuala ya utalii nchini. 

Uteuzi aliofanya Rais Magufuli jioni ya September 2, 2019

magufulib

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Fredrick Cassian Kahimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Kahimba umeanza 31 Agosti, 2019.

Kabla ya uteuzi huo, Prof. Kahimba alikuwa Profesa Mshiriki na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Utawala na Fedha), Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Mkoani Morogoro.

Prof. Kahimba amechukua nafasi hiyo iliyokuwa wazi.

Subcategories

Page 1 of 50