Chanjo ya ugonjwa wa Mdonde inayojulikana kama MG/10/3C itadhibiti ugonjwa huo

Na Gerald Lwomile

Morogoro

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH imesema ina matumaini makubwa kuwa chanjo ya ugonjwa wa Mdonde iliyotafitiwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA itatatua changamoto ya ugonjwa huo ambao umekuwa ukiua kuku wengi na wakati mwingine kuleta hasara ya asilimia 100 kwa mfugaji.

Mdonde Dkt Msangi

Mkurugenzi wa Utafiti kutoka COSTECH Dkt. Bakari Msangi akizungumza na SUAMEDIA

Hayo yamesemwa leo Julai 24, 2019 na Mkurugenzi wa Utafiti kutoka COSTECH Dkt. Bakari Msangi wakati akifungua warsha ya wadau wa Mradi wa Ufugaji Kuku wa Asili ulio chini ya ufadhili wa tume hiyo

Dkt. Msangi amesema CHANJO YA UGONJWA WA MDONDE INAYOJULIKANA KAMA MG/10/3C iliyoanza kutafitiwa SUA mapema miaka ya 2000 ni chanjo ambayo itasaidia sana wafugaji wa kuku nchini kutoka na kutengenezwa na hatimaye kujaribiwa kutokana na vimelea vya ugonjwa huo kutoka kwa kuku wa hapa nchini.

….na unaweza kuona kabisa kwa mfano mradi huu tunaoufunga leo umeweza kuzalisha chanjo ambayo inaingia dukani sasa hivi ambayo inatokana na vimelea vya ugonjwa wa mdondo vinavyotokana na kuku wetu wenyewe,amesema Dkt. Msangi

Akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi mmoja wa waanzilishi wa mradi huo Prof. Madundo Mtambo ambaye pia ni Mkurugenzi  Mkuu wa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda Tanzania TIRDO amesema utafiti huo kimsingi ulimalizika muda mrefu lakini kilichokuwa kinangojewa ni taratibu za kuthibitisha chanjo hiyo

Mdonde Prof Madundo

  Mkurugenzi  Mkuu wa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda Tanzania TIRDO Prof. Madundo Mtambo akitoa ufafanuzi juu ya chanjo ya Mdonde

Amesema yeye kama Mkurugenzi wa TIRDO anaona kuna uhusiano mkubwa wa utafiti huo na maendeleo ya viwanda nchini kwani ili chanjo hiyo iingie sokoni ni lazima izalishwe kama zao la kiwanda na kufikisha matokeo ya utafiti kwa walaji

…lakini ili chanjo iweze kuwa chanjo lazima utafiti ufanyike nchi nzima ili kujua kama kweli  chanjo inafanya kazi …. lakini pia lazima upate kibali kutoka Wizara ya Mifugo na TFDA …kwa hiyo tunashukuru sana COSTECH kwa ufadhili katika mradi huu na tayari mamlaka zimethibitisha kuwa chanjo inafanya kazi na muda si mrefu itaingia sokoni. amesema Prof. Mtambo

Awali akimkaribisha Mgeni Rasmi Msimamizi wa mradi huo kutoka SUA Prof. Amandus Mhairwa amesema utafiti huu ni moja ya mafanikio makubwa kutoka SUA na utasadia katika kutatua kero za ugonjwa wa Mdonde kwa wafugaji wa kuku nchini

Mdonde Washiriki

Mgeni rasmi katika warsha ya ya wadau wa Mradi wa Ufugaji Kuku wa Asili Dkt. Msangi aliyekaa kulia akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa utafiti waliokaa na wadau wa mradi ( Picha zote na Nicholus Roman)

RAIS MAGUFULI KUWEKA JIWE LA MSINGI WA MRADI WA KUFUA UMEME WA MEGAWATI 2115 WILAYANI RUFIJI

Na: Farida Mkongwe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Ijumaa tarehe 26 mwezi huu anatarajiwa kuweka jiwe la

msingi wa mradi wa kufua umeme wa Megawati 2115 katika eneo la mradi lililopo wilayani Rufiji mkoa wa Pwani.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mkoani Morogoro Waziri wa Nishati Mh. Dkt. Medard Kalemani amesema tukio hilo la kihistoria kwa

Tanzania litaliwezesha taifa kuwa na umeme wa kutosha na wa uhakika ambao gharama yake itakuwa ni nafuu kwa watumiaji.

moWaziri wa Nishati Mh. Dkt. Medard Kalemani wa pili kushoto akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uwekaji wa jiwe la msingi wa Mradi wa kufua umeme

 “Kukamilika kwa mradi huu ambao utawawezesha watanzania kupata umeme kwa gharama nafuu kupunguza uharibifu wa mazingira,

kuweka mazingira sahihi na yanayotabirika katika Azma ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya miaka mitano inayolenga kujenga Uchumi wa Viwanda na

kufikia kipato cha kati ifikapo mwaka 2025”, alisema Dkt. Kalemani.

moo

Amesema mradi huo wa kufua umeme unaotokana na maporomoko ya maji ya Mto Rufiji unaoendelea kutekelezwa tangu mwezi Desemba mwaka

jana, kwa Afrika ni mradi wa nne kwa ukubwa kutokana na bwawa litakalojengwa kuwa na uwezo wa kuhifadhi maji kwa mita za ujazo bilioni  35.2

Waziri Kalemani amesema bwawa hilo litakuwa na urefu wa kilomita 100, upana kilomita 25 na kina mita 131 na kwamba litakuwa ni bwawa la 60

kwa ukubwa duniani kati ya mabwawa 70 yaliyopo kwa sasa. 

Awali akimkaribisha Waziri Kalemani, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven Kebwe amesema mradi huo utakapokamilika kwa kiasi kikubwa

utawanufaisha wakazi wa mkoa huo pamoja na kuimarisha shughuli za kiuchumi na kijamii kwa kuendeleza kilimo cha umwagiliaji, shughuli za uvuvi,

kukuza utalii na kuongeza ajira kwa watanzania. 

Mradi wa kufua umeme unaotarajiwa kukamilika mwezi Juni 2022 utatumia shilingi tirioni 6.5 pesa ambazo zinatolewa na Serikali.

 

ALICHOKIONGEA MAKAMU WA MKUU WA CHUO SUA PROF. RAPHAEL CHIBUNDA TCU 2019

Usiasahau kusbscribe upate taarifa mbalimbali kwa uhakika hapa

WANAFUNZI CHAGUENI KOZI KWA UMAKINI - PROF NDALICHAKO

Na Gerald Lwomile

Dar es Salaam

Serikali imewataka wanafunzi waliomaliza kidato cha sita nchini kuwa makini katika kuchagua kozi na kufanya udahili wa kujiunga na masomo ya juu ili kuepuka kukosa nafasi za kujiunga na vyuo hivyo kwa kukosa sifa pamoja na kuwa na ufaulu mzuri

NDALICHAKO

Prof. Ndalichako akifunga maonesho ya TCU 2019 (Picha na Gerald Lwomile)

Agizo hilo limetolewa na serikali kufuatia kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wanafunzi na wazazi baada ya baadhi ya watoto wakiwemo ambao wamepata ufaulu wa daraja la kwanza kukosa nafasi za kujiunga na masomo ya elimu ya juu

Akizungumza katika siku ya kufunga maonesho ya vyuo vikuu julai 20 jijini Dar es Salaam Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema kuna kozi zingine ambazo si rahisi mwanafunzi kuchaguliwa kutokana na ushindani na nafasi chache katika vyuo vikuu.

“…kwa hiyo unakuta mwanafunzi ana daraja la kwanza pointi tisa unakwenda kuchagua kusomea kozi ya mafuta na gesi ambayo inachukuwa wanafunzi kumi nchi nzima sasa kama wewe una pointi tisa mwenzio ana pointi tatu kwani yeye hawezi akatamani kusoma kozi unayoichagua...chagua kozi unayoweza kwenda kushindana” alisema Prof. Ndalichako.

IMG 7436 min 1

Maafisa udahili kutoka SUA wakifanya udahili wa wanafunzi

Akizungumzia ubora wa elimu nchini Mhe. Prof. Ndalichako amevitaka vyuo kuhakikisha havitegemei Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) pekee katika kuboresha elimu nchini na kuwa vitengo vya kusimamia ubora wa elimu vinatakiwa kufanya kazi hivyo kwa ufanisi

Awali akitoa taarifa ya maonesho hayo kwa mgeni rasmi Katibu Mkuu Mtendaji wa TCU Prof. Charles Kihampa amesema malengo ya manesho hayo ni pamoja na kutoa elimu kwa umma kuhusu fursa mbalimbali zinazopatikana katika vyuo vya elimu ya juu

Kihampa

Prof. Kihampa akitoa taarifa ya maonesho kwa washiriki

“… lakini pia ni kutoa fursa kwa Taasisi zinazoshiriki kujitangaza kuhusu majukumu yao na huduma wanazotoa, wananchi wengi wanafikiri Taasisi za elimu ya juu kazi yake ni kufundisha tu lakini Taasisi zetu pia zinatoa huduma za ushauri katika fani mbalimbali kuanzia fani za majenzi, afya na fani nyingine nyingi” alisema Prof. Ndalichako.

Maonesho ya mwaka huu yameshirikisha  zaidi ya vyuo 81 fofauti na mwaka jana ambapo ni taasisi 73 tu ndizo zilishirki huku  waliohudhuria walikuwa zaidi ya  elfu tano  huku mwaka huu pamoja na kutokuwa na takwimu sahihi lakini waliohudhuria wanakadiriwa kuwa zaidi ya elfu 6

Maonesho haya ya vyuo vikuu yaliyomalizika leo Julai 20 yalikuwa na kauli mbiu inayoonyesha umuhimu wa Vyuo Vikuu kufundisha kwa lengo la kuzalisha wanafunzi wenye ujuzi ambayo ni  “JUKUMU LA VYUO VYA ELIMU YA JUU KATIKA KUZALISHA UJUZI UNAOHITAJIKA KWA AJILI YA VIWANDA”

DR DEVO MARIAM

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza SUA Dkt. Devotha Mosha kulia akiwa Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano na Masoko SUA Bibi Mariam Mwayela kushoto wakisikilza hotuba katika ufungaji wa maonesho ya TCU (Picha na Gerald Lwomile)

Pamoja na kutoa kozi za sayansi ya kilimo lakini pia SUA inatoa kozi mbalimbali zisizo za kilimo

Na Gerald Lwomile

Dar es Salaam

Imeelezwa kuwa pamoja na ukweli kuwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kinatoa kozi mbalimbali za kilimo lakini pia chuo hicho kinatoa kozi katika fani mbalimbali tofauti na Kilimo kama Ualimu wa Masomo ya Sanyansi Mazingira pamoja na Maendeleo Vijijini.

udahili min min

Maafisa udahili wa SUA waliovaa fulana za kufanana wanaendelea na udahili wa wanafunzi katika viwanja vya mnazi mmoja Dar es Salaam (Picha na Gerald Lwomile)

Ufafanuzi huo umekuja kufuatia kuwepo kwa taarifa kwa wananchi wengi kuwa SUA imekuwa ikitoa kozi za kilimo pekee na wanafunzi wengi kushindwa kujua ukweli wa kozi zinazotolewa SUA

Akizungumza katika maonesho ya vyuo vikuu ambayo yanaendela katika viwanja vya mnazi mmoja Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mahusianao na Masoko SUA Bi. Mariam Mwayela alifafanua hayo wakati akizungumza na wanafunzi na wananchi mbalimbali waliofika katika maonesho hayo.

“….. maana imekuwa inaaminika kuwa SUA inatoa kozi za kilimo pekee, hapana mbali na kuwepo kwa kozi za kilimo lakini pia SUA inatoa kozi zingine ambazo mwanafunzi anaweza kusoma hata kama amesoma masomo ya sanaa yaani Arts”

Wakati huo Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda amewataka wanafunzi mbalimbali wanaotaka kusoma katika chuo cha SUA waendelee kutembelea katika banda la SUA wakati huu wa maonesho kwani zoezi la udahili pia linaendelea katika eneo hilo.

chibunda min min

Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Chibunda akizungumza na vyombo vya habari katika maonesho ya TCU (Picha na Tatyana Selestine)

Amesema mbali na wanafunzi hao kujionea teknolojia na ubunifu mbalimbali unaofanywa na chuo lakini pia watapata fursa ya kuchagua programu mbalimbali wanazotaka kusomea

“Tunatoa huduma za ushauri kwa wanafunzi na kuwaelekeza kuhusu kozi mbalimbali ambazo zinatolewa chuoni kwetu hivyo mwanafunzi anaweza kuchagua kozi ambayo anataka kusoma kutokana na ufaulu wake wa kidato cha sita”

Ikiwa ni siku ya nne tangu Maonesho haya ya Vyuo Vikuu kuanza muitikio wa wanafunzi na wazazi umekuwa ni mkubwa sana. Maonesho haya vyuo vikuu yanaendelea jiji Dar es Salaam hadi julai 20 huku yakiwa na kauli mbiu “JUKUMU LA VYUO VYA ELIMU YA JUU KATIKA KUZALISHA UJUZI UNAOHITAJIKA KWA AJILI YA VIWANDA”

Serikali inafurahishwa na hatua Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kusimamia Ithibati na Ubora wa Elimu

Na Gerald Lwomile

Dar es Salaam

Serikali imesema inafurahishwa na hatua zinazochukuliwa na Wizara ya Sayansi na Teknolojia katika kusimamia Ithibati na Ubora wa elimu unaotolewa na vyuo vikuu nchini vikiwemo vya umma na binafsi jambo linalosaidia kuwafanya wahitimu kuwa na soko la ajira ndani na nje ya nchi.

Hayo yamesemwa leo julai 17 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa uzinduzi rasmi wa maonesho ya vyuo vikuu wakati akizungumza na washiriki wa maonesho na wananchi katika viwanja vya mnazi mmoja jiji Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema uandaaji wa mitaala mbalimbali katika vyuo umeboreshwa kufuatia mafunzo yaliyotolewa na wizara hiyo na kuwa hatua zinachuliwa na vyuo mbalimbali vya kuhuisha mitaala na kuja na mitaala mipya ni jambo ambalo linainua ubora wa elimu nchini

waziri mkuu 2 min

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na washiriki wa maonesho ya vyuo vikuu katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam (Picha na Mariam Mwayela)

Waziri mkuu amesisitiza kuwepo kwa mitaala ambayo haiwaandai wahitimu kuajiriwa pekee lakini pia kuwepo na mitaala ambayo inawaandaa wahitimu kujiajiri, amesema kutokana na hali hiyo taifa litachochea hali ya ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu

“Bado nieendele kutoa wito kwa vyuo vikuu hapa nchini kuendelea kuhuisha mitaala ya elimu hiyo ili kutoa matokeo tunayoyatarajia”

Akitoa shukrani kwa Waziri Mkuu  baada ya kuzindua rasmi maonesho hayo Mwenyekiti wa Watendaji Wakuu wa Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu Vishiriki nchini ambaye pia ni Makamu wa  Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kutoa ushirikiano katika kuimarisha utendaji katika vyuo vikuu nchini.

Prof Chibunda min

 

Mwenyekiti wa Watendaji Wakuu wa Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu Vishiriki nchini ambaye pia ni Makamu wa  Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda akitoa neno la shukrani kwa serikali (Picha na Tatyana Selestine)

uboreshaji na upelekaji wa mikopo kwa wanafunzi katika vyuo vikuu nchini kwa kiasi kikubwa imeondoa tatizo la migomo katika vyuo vikuu nchini na kuwa Bodi ya Mikopo na Serikali kwa kiasi kikubwa vinatakiwa kupongezwa.

“Kwa niaba ya wasimamizi wa vyuo vikuu napenda kuishukuru sana serikali kwa hili ambalo tume wamelifanya la kumaliza uhakiki katika baadhi ya vyuo vikuu ambavyo vilikuwa vimefungiwa udahili na sasa vimeruhusiwa kuendelea na udahili tunaishukuru sana tume pamoja na serikali na nipende kutoa rai kwa tume kufanya uhakiki katika vyuo vikuu vilivyobaki” amesema Prof. Chibunda

Tazama Hapa Matokea Ya Kidato cha Sita 2019

Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) nchini Tanzania leo Alhamisi Julai 11, 2019 limetangaza matokeo ya kidato cha sita 2019.

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa na Katibu Mtendaji wa Necta mjini Unguja Zanzibar, Dk Charles Msonde amesema ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 97.58 mwaka 2018 hadi kufikia asilimia 98.32 mwaka 2019 ikiwa ni sawa na asilimia 0.74.

Dk Msonde amesema mtihani huo uliofanyika kati ya Mei 6 hadi 23 mwaka 2019, watahiniwa 91,298 walisajiliwa wakiwamo wasichana 37,948 sawa na asilimia 41.56 na wavulana 53,350 sawa na asilimia 58.44.

Amesema kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa wa shule walikuwa 80,216 na watahiniwa wa kujitegemea walikuwa ni 11, 082.
 
1.Kutazama matokeo ya Kidato cha Sita  <<BOFYA HAPA>>.

2.Kutazama Matokeo Ya Mtihani Wa Ualimu 2019  <<BOFYA HAPA>>

Subcategories

Page 6 of 51