WANAFUZI WA SEKONDARI WAASWA KUSOMA MASOMO YA SAYANSI

WANAFUZI WA SEKONDARI WAASWA KUSOMA MASOMO YA SAYANSI

Na: CONSOLATA PHILEMON

Wito umetolewa kwa wanafunzi wa sekondari kupenda kusoma masomo ya sanyansi kwa sababu bila sayansi na teknolojia maisha ya binadamu hayawezi kuwa rahisi na kufurahiwa.

Bofya kichwa cha habari kwa habari zaidi.......

MAFANIKIO NA CHANGAMOTO KATIKA TAFITI ZA SACIDS NGORONGORO MKOANI ARUSHA

MAFANIKIO NA CHANGAMOTO KATIKA TAFITI ZA SACIDS NGORONGORO MKOANI ARUSHA

Na:BUJAGA IZENGO KADAGO

Kumekuwepo na mafanikio na changamoto katika utafiti unaofanywa na mradi wa SACIDS kuhusu namna ya kukabiliana na mazonge katika maisha ya binadamu, mifugo na wanyamapori katika hifadhi ya Ngorongoro mkoa wa Arusha.

 Hayo yameelezwa na mratibu wa mradi wa SACIDS Prof. ESRON KARIMURIBO kutoka SUA alipokuwa akiwakaribisha wadau kujadili namna mradi ulivyotekelezwa hadi sasa katika warsha ya siku mbili inayofanyika jijini Arusha.

Bofya kichwa cha habari kwa habari zaidi.......

WAFUGAJI WAZINGATIE LISHE YA MIFUGO KUEPUKA MAGONJWA YANAYOZUILIKA

WAFUGAJI WAZINGATIE LISHE YA MIFUGO KUEPUKA MAGONJWA YANAYOZUILIKA

 Na:FARIDA MKONGWE

Wakulima na wafugaji wa ng’ombe, mbuzi na wanyama wengine wa jamii hiyo wametakiwa kuhakikisha chakula wanachokitumia kwa ajili ya malisho ya mifugo yao kinakuwa na virutubusho vya aina yote ikiwa ni pamoja na madini ili wanyama wanaofuga waondokane na tabia ya kuokoteza vitu ovyo hali ambayo inaleta madhara.

Wito huo umetolewa na mwanafunzi wa mwaka wa 5 anayesomea shahada ya tiba ya mifugo katika chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA bw. FREDY MAKOGA wakati walipokuwa wakifanya upasuaji kwa mbuzi aliyekula makokwa ya embe, mabunzi pamoja na takataka nyingine hali iliyosababisha mfumo wa chakula wa mbuzi huyo hushindwe kufanya kazi vizuri na hivyo mbuzi huyo kudhoofu kiafya.

Bofya kichwa cha habari kwa habari zaidi.......

WAKATI UCHAGUZI 2015 UKIKARIBIA WANANCHI MANISPAA YA MOROGORO BADO HATIHATI

 WAKATI UCHAGUZI 2015 UKIKARIBIA WANANCHI MANISPAA YA MOROGORO BADO HATIHATI

 Na:AMINA B. MAMBO

Wakazi wa Manispaa ya Morogoro wamekuwa wakitoa maoni tofauti  juu ya ahadi zinazotolewa na wagombea  mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu iwapo zitatekelezeka huku wengine wakisema kuwa hazitekelezeki kwa kuwa wamegeuza siasa kama sehemu ya malumbano na kuwageuza wananchi watoto  kwa kuahidi ahadi nzuri ambazo zinaishia midomoni mwao.

Bofya kichwa cha habari kwa habari zaidi.......

KATIZO LA UMEME NI KERO KWA WAFANYABIASHARA MKOANI MOROGORO

KATIZO LA UMEME NI KERO KWA WAFANYABIASHARA MKOANI MOROGORO

Na:AMINA B. MAMBO

Wafanyabiashara wa samaki katika Manispaa ya Morogoro wameendelea kuulalamikia Uongozi wa Tanesko kwa kitendo cha kuendelea kukata umeme kila siku bila taarifa maalum na kwamba tatizo hilo linasababisha hasara katika biashara zao.

Bofya kichwa cha habari kwa habari zaidi.......

WAKULIMA WAFURAHIA MATOKEO CHANYA YA UTAFITI WA KILIMO BORA CHA ALIZETI HUKO KILOSA NA MVOMERO

WAKULIMA WAFURAHIA MATOKEO CHANYA YA UTAFITI WA KILIMO BORA CHA ALIZETI HUKO KILOSA NA MVOMERO

Na:BUJAGA IZENGO KADAGO

Wakulima watafiti kutoka Wlaya za Kilosa na Mvomero walioshiriki katika Utafiti kupitia Mradi wa Uendelezaji Elimu ya Uzalishaji wa Alizeti, ili kuondoa umaskini, wamekiri kupata mabadiliko chanya katika kilimo chao cha alizeti.

Wakulima watafiti hao walishiriki katika mradi wa chuo kikuu cha sokoine cha kilimo, SUA, kupitia Mradi wa Epinav uliolenga kuboresha kilimo cha alizeti kwa kutumia mbinu bora za kilimo pamoja na mbegu bora za alizeti.

Bofya kichwa cha habari kwa habari zaidi.......

SUA KUJIUNGA NA WAVUTI YA SUA KUIMARISHA MAWASILIANO NA KIBIASHARA

  SUA KUJIUNGA NA WAVUTI YA SUA KUIMARISHA         MAWASILIANO NA KIBIASHARA

Na:TATYANA CELESTINE

Ili kuboresha ushirikiano, mawasiliano na kukua kibiashara Chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) sasa kinatakiwa kutumia email kwa mfumo wa Google cloud kwa kujiunga na wavuti ya SUA yenyewe kupitiagoogle Cloud.

Akizungumza wakati wakufungua warsha ya siku moja Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ProfesaYonika Mathew Ngaga amesema warsha hiyo inamalengo ya kutoa elimu kwawafanyakazi wa kila Idara katika Chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) kuhusu kuongeza uwezo na uwepo wa wavuti chuoni hapo kwakutumia SUA google Cloud

Bofya kichwa cha habari kwa habari zaidi.......

WANAFUNZI WANAOSOMEA MISITU WANUFAIKA OLMOTONYI

WANAFUNZI WANAOSOMEA MISITU WANUFAIKA OLMOTONYI

Na:GERALD LWOMILE

Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo kimesema kuwa wanafunzi wengi wanaosoma fani ya misitu nchini kwa kiasi kikubwa wamenufaika na Kituo cha Mafunzo ya Misitu Olmotonyi kilicho chini ya chuo kikuu hicho.

Akizungumza na SUAMEDIA Meneja wa Kituo hicho cha Misitu Olmotonyi Bw. Modest Mrecha amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa shamba hilo watafiti wengi katika Sekta ya Misitu nchini wamepita shambani hapo na kufanya tafiti mbalimbali.

Bofya kichwa cha habari kwa habari zaidi.......

WATANZANIA TUFUATE KANUNI ZA AFYA KUHEPUKA JANGA LA KIPINDUPINDU

WATANZANIA TUFUATE KANUNI ZA AFYA KUHEPUKA JANGA LA KIPINDUPINDU- DR LYAMUYA

 Na:TATYANA CELESTINE

Wakazi wa Mkoa wa Morogoro wametakiwa kuendelea kufuata taratibu na kanuni za afya ili kuepuka ugonjwa wa kipindupindu unaoonesha kuenea katika maeneo ya manispaa ya Morogoro.

Hayo yamesemwa na Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Rufaa mkoani Morogoro Dokta Ritha Lyamuya alipoongea na vyombo vya habari na kusema, wananchi wanatakiwa kuzidi kuchukua taadhari kutokana na kuwepo kwa ugonjwa huo

Bofya kichwa cha habari kwa habari zaidi.......

MAAFISA AFYA KATA ZOTE KUKAGUA USAFI MANISPAA YA MOROGORO

MAAFISA AFYA KATA ZOTE KUKAGUA USAFI MANISPAA YA MOROGORO

Na:TATYANA CELESTINE

Kufuatia hali ya usafi katika  Manispaa ya Morogoro kuwa katika hali isiyo njema, Maafisa Afya kutoka kila Kata wamelazimika kukagua kila eneo kuhakikisha yanafanyiwa usafi hasa katika wiki  hii ya usafi wa mazingira hali ambayo  imeibua baadhi ya maeneo kuonekana kuwa nyuma katika kutekelezaji wa amri za Manispaa

Bofya kichwa cha habari kwa habari zaidi.......

ZIMAMOTO KUSUASUA MKOANI MOROGORO

ZIMAMOTO KUSUASUA MKOANI MOROGORO

 Na:HUSNA YAHYA

Wakazi wa manispaa morogoro wamelalamikia huduma ya zimamoto kwa  kuchelewa kufika katika eneo la tukio hali inayosababisha  kuteketea kwa  mali na bidhaa mbalimbali  za wahanga wa matukio ya moto.

Bofya kichwa cha habari kwa habari zaidi.......

SUA YATATUA TATIZO LA UPANDAJI MALISHO YA MIFUGO KATIKA MAENEO YA MIJINI

SUA YATATUA TATIZO LA UPANDAJI MALISHO YA MIFUGO KATIKA MAENEO YA MIJINI

Na:BUJAGA IZENGO KADAGO

Wafugaji wanaoishi mijini sasa hawana sababu ya kuhofia kuendesha shughuli za ufugaji kutokana na nafasi finyu ya malisho baada ya chuo kikuu cha sokoine cha kulimo sua kukamilisha utafiti kuhusu malisho ya mifugo kwa kutumia reki.

WAKULIMA TUMIENI MBOLEA AINA YA MBOJI KUONGEZA TIJA KATIKA KILIMO

WAKULIMA TUMIENI MBOLEA AINA YA MBOJI KUONGEZA TIJA KATIKA KILIMO

Wakulima nchini wametakiwa kutengeneza mbolea aina ya mboji, mbole itakayowaletea tija kubwa katika kilimo chao kwa kupata mazao bora na mengi hususani katika ardhi iliyochoka au yenye rutuba hafifu katika maeneo mengi nchini.

SUA YANG'ARA, MAONESHO YA SABABASA DAR -ES -SALAAM

SUA YANG'ARA, MAONESHO YA SABABASA DAR -ES -SALAAM

Banda la maonesho la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ktk uwanja wa maonesho wa kimataifa wa biashara jijini Dar es salaam limekuwa kivutio kwa wananchi hususani wakulima

SUA YAPONGEZWA KWA USHIRIKI WA UIFADHI WA MAZINGIRA NCHINI

SUA YAPONGEZWA KWA USHIRIKI WA UIFADHI WA MAZINGIRA NCHINI

Na:BUJAGA I KADAGO

Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo, SUA, kimepongezwa kwa ushiriki wake katika uhifadhi wa mazingira nchini ambapo kimewezesha kuanzishwa kwa jukwaa la mazingira wilayani kilosa mkoani Morogoro

Bofya kichwa cha habari kwa habari zaidi.......

SUA YA KWANZA BARANI AFRIKA KUPATA RUZUKU KUBWA

SUA YA KWANZA KUPATA RUZUKU KUBWA BARANI AFRIKA

 Na:TATYANA CELESTINE

Imeelezwa kuwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ni cha kwanza barani afrika kupata ruzuku kubwa  kutoka shirika la kutoa misaada la watu wa marekani (usaid) misaada inayosaidia kuimarisha miundombinu na taaluma katika chuo hicho............................

 Bofya kichwa cha habari kwa habari zaidi.......

WAKAZI WA MOROGORO WATOA MAONI YAO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

WAKAZI WA MOROGORO WATOA MAONI YAO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

 Na:AMINA B. MAMBO

Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Morogoro  ambao ni wanachama wa  Chama Cha Mapinduzi wameonekana kuvutiwa na umati wa wananchi waliojitokeza kumpokea mgombea urais wa ukawa kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo chadema huku wakidai kuwa mkusanyiko huo unaonesha ni kwa kiasi gani wananchi wanahitaji babadiliko. 

Bofya kichwa cha habari kwa habari zaidi.......

Subcategories

Page 51 of 51